~~!!gubu!!~~ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~~!!gubu!!~~

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Mar 11, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwa nnavyoelewa mimi neno ''gubu'' hua linatumika kuongelea ile hali ya mtu kukumbushia makosa au kutosahau kwa maana nyingine.Wanaosemwa kwa kua na gubu mara nyingi ni wanawake.Wanaume hawachoki kabisa kuongelea ni kiasi gani hawapendelei/hawafurahishwi na hii tabia.

  Binafsi sipendi hilo neno kwasababu halitendei haki watu wanaokosewa kila mara alafu akijaribu kukuonyesha kwamba hata jana ulifanya vile vile unaanza kukwambia ana gubu!!!Kama ambavyo unapomuomba mtu msamaha unategemea na unataka kusamehewa ndivyo ambavyo na wewe unatakiwa usirudie makosa.Ukikosa tena unaomba msamaha na unayemwomba ana haki ya kukuonyesha ni jinsi gani unaabuse msamaha anaokupa kila mara.

  Ni kweli kwamba binadamu hatujakamilika ndo maana tunakosa na kukosa tena na tena....kwa hayo hayo mapungufu ndo inashindikana kusahau kabisa yaliyopita na kukumbushana mara kwa mara.
  Naamini kwamba jana inajenga leo....ulichokosea jana unajifunza ili usirudie tena leo....ulichofanya jana kama ni kizuri kinafanikisha furaha ya leo nk.Hata swala la mafanikio....ukikumbuka kitu kilichokuangusha jana ni rahisi zaidi kukikwepa mbeleni kwahiyo watu wakubali kusemwa na kukumbushwa pale inapobidi maana safari ya mabadiliko ndivyo inavyoanza...KWA KUKUMBUKA!!!!

  Ila katika kila kitu kunahitajika kiasi.Don't exaggerate things....kidogo acha kibaki kua kidogo!!!
   
 2. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  asante lizzy lakini nafikiri ni vizuri unaposema umesamehe usamehe bila kukumbushia mwenzio alitenda nini jana hapa kunakuwa hakuna msamaha wa kweli,kama umeamua kusamehe samehe kama hapana iwe ivo sio mume amekosea jana unasamehe halafu akikosea wiki ijayo unaanza kukusanya makosa yote ya miaka yenu ya ndoa.hii hufanya mtu hata kama ana nia ya kujirekebisha asifanye ivo maana huwa tunakusanya makosa ya kuku na bata wakati mmoja kitu ambacho si sawa.

  karama hii hutupa Mwenyenzi Mungu pekee ukimuomba kweli atakupa maana si rahisi kusamehe kama tunavoandika lakini yote yawezekana.
   
 3. CPU

  CPU JF Gold Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  My dia
  Ni kweli kusemwa hakukwepeki sometimes ila mtu mzima kuna approach tofauti nadhani.
  Mfano, mtoto unaweza ukamsema na kumkumbusha kwamba amerudia kosa straight foward bila kupindapinda.
  Kwa staha ya utu uzima huna haja ya kumueleza upya alivyorudia kosa, coz hata yeye mwenyewe atajitambua karudia kosa bila hata wewe kusema chochote, labda iwe kwa wale watu watukutu.
  Lakin kama mimi uanze kunieleza upya stori ya mimi nilivyokukosea kipindi cha nyuma wakati hata hata mimi nina kumbukumbu niliwahi kufanya hivyo, haunijengi kihisia badala yake unanikwaza zaidi.
  Acha nijihukumu mwenyewe nione nilivyorudia kosa coz ukianza kukumbushia mkasa mzima wa nyuma utanikwaza na hivyo naweza kutengeneza hoja ya kujitetea kwamba unania ya kunishambulia
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tatizo unaweza ukamsamehe mtu leo halafu kesho au kesho kutwa akarudi kosa hilo hilo akijua tu kwamba akija kwako akikuomba msamaha utamsamehe
   
 5. M

  Mundu JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Waswahili walisema "kusamehe ni kusahau". Kusamehe si kukumbushia makosa ya zamani yanapotokea upya! Na ikifanyika hivyo, basi hakuna msamaha wa dhati. Kuwa na gubu si lazima ukumbushe ama kugomba kwa jambo hilo hilo kila wakati.
  Hata kununa kwa jambo hilo hilo kila wakati ni gubu pia. Na mara nyingi tabia hujenga mazoea; na mazoea huunda hisia, na hisia hupelekea mtu kutenda jambo, kukemea ama kugomba bila ya kufikiria! Kisa tu, anajenga dhana kuwa mtu huyu ndivyo alivyo.

  Mara nyingi ili kuyashinda mambo haya, wenzi hupaswa kutumia mazungumzo na kuongea kwa taratibu tena wakati mwingine kabisa baada ya jambo kutokea..na hapo utagundua kuwa kumbe leo, mwenzio gari iliharibika ndio maana kachelewa kurudi nyumbani. Wakati jana alichelewa kwa kuwa alikuwa Bar. Kwa wenzangu namie wenye gubu, yeye atafikiria tu (hisia) kuwa mwenzake kapitia tena Bar leo, ndo mana kachelewa!

  Let's talk.
   
 6. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  finest kama Mungu asingekuwa anakusamehe ww ungekuwa hapo ulipo?? akikukosea msamehe tu lkn usianze kukumbushia mambo ya juzi ooh ulifanya jana ukafanya leo tena umerudia!!!

  i hate, i hate wanaume wenye gubu heri nibakie single hivi hivi!!!!
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hatujakamilika ndo maana sisi ni wanadamu na sio Mungu!Tukianza kusema kila kitu kama Mungu ange...hiki au kile nadhani hamna ambae angepña huo mchanganuo!Huwezi kua mtu wa kukosea wengine kila siku alafu uchukie kuonyeshwa ulivyo!
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sijakataa Susy Je? Leo mumeo akikuletea mwanamke ndani ya nyumba yenu utamsamehe kwa vile Mungu kasema tusamehe, tunaangalia makosa ya kusamehe sio kusamehe kwa kuwa Mungu kasema tusamehe unaweza kujikuta unasemehe mtu halafu wewe ndio unaingia kwenye matatizo
   
Loading...