Mnaoishi na wenza mnawezaje kuvumilia mapungufu yao?

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
10,087
15,958
Wakuu huyu shemej yenu siku hiz anaishi hapa kwangu

Ilibid nimruhusu sabab kuna tukio nilifanya sasa kujipendekeza kwake tena nikaona nimtunuku shauku yake ya siku zote ya kuish namim, hata kama hatujarasimisha mahusiano.

Tatizo linakuja huyu binti kakulia maisha ya pesa pesa kwao sasa ananipa shida mnoo. Zamani alikua anakuja anakaa week mbili au week anaondoka.. hayo mapunguf yalikuepo ila niliona labda kawaida ila sasa amezidi huyu binti Ngoja niorodheshe hapa

1. Akipika kuunguza chakula ni kawaida mnoo.. hadi moshi ndani(gas inalika tuu +kuunguza menu iliyobajetiwa)
2. Binti anaweza chemsha maj kwenye jiko ya gas had yanakaukia.. aisee
3. Binti anaweza pika kuku.. samak.. uyoga.. wali.. chips ...mayai..kwa mlo mmoja.. (i think ni upotevu wa resources)
4. Huyu binti hazimag taa za nje ya nyumba hata siku moja.. ila anajua sana kuomba msamaha..
5. Unarudi unakuta kawasha kiyoyoz halaf madirisha yako waz.. na milango mingne had ya jikon iko wazi
6. Binti chupa za vinywaj hazikai yaan .. na ananepeana kwelkwel hapa na anajua mmi na ubonge ni paka na panya
7. Ukikuta anafua sasa. Hayo maji yanavyomwagwa.. yaan ile timer ya mashine inazungukaaa weee hata mara 5-7.. anafua siku nzima.. (umeme hajali) etc

Sasa liliofanya niandike huu uzi.. pa1 na maudhi yoote, jana nmerud nmeleta unga wa ngano 25 kg na sembe 25kg. Mimi napenda sana chapat za maj, sasa ndo akanipikia jana na leo asubuh.

Wakati anapika akawa anasema mbona leo chapat znangangania chini ahh sasa mi nkawa sielewi ndo kwenda kule namuuliza vip.. et .. nahis nimechanganya unga wa sembe na ngano kwenye mfuko wa ngano.. yaan jana sjui alichota unga kuhamishia kwenye containers sasa wakat anarudishia badala kurudisha kwenye wa sembe kaweka kwenye wa ngano.. so kwa maana hyo unga wote wa ngano ni wa kutupa sabab una sembe ndan. imagine that wakuu

Najua mtasema nna gubu.. poa tu.. ila aisee kuish na mtu inataka moyo mnoo.. nmemkaripia hapa.. et analia kakimbilia ndani
 
Muelekeze tu atakaa sawa Kama unampenda maybe Ni wale watoto wamesoma Sana boarding au hajafundishwa kwao
Habadiliki.. ni wa mda mref. Anaweza kaa week mbili hajakupiga tukio halaf week ya tatu anakupiga tukio anasema samahan alijisahau
 
Back
Top Bottom