Iron Lady
JF-Expert Member
- Mar 4, 2008
- 4,071
- 1,363
Bwana Nicolas,
Naomba nipingane na wewe juu ya hoja yako hii "we have no power to decide anything in this world,wenye power ndio wanasema nasi tunafuata". Mtanzania inaelekea unajiweka mwenyewe kwenye nafasi ya chini sana duniani. Hakuna mtu anayekulazimisha uchukuwe nafasi hiyo. Nami nakushauri kwamba uachane na nafasi hiyo ktk uringo huu wa kimataifa. Kama wanakupangia mambo nawe ni mtu wa kufuata tu basi nakuombea sana ujiokoe na mnyororo huo. Cha kufanya ni hiki: Jiulize swali kwa nini wanipangie na kwa nini sina "power"? Nakwambia hivi, ukitaka kuwa na power utapata power yako, jambo kubwa ni uamuzi wako mwenyewe. Pia usipotaka kupangiwa mambo na jirani yako ni hatua nzuri. Hatua inayofuata ni kuanza kujipangia mwenyewe. Ukifanya hayo, hutaona mtu anakuingilia...ndiyo kwanza atakuheshimu sana maana unajitegemea na unaonyesha utashi wako. Mtanzania simama wima na chukua nafasi yako kama mtu mwenye hadhi na uwezo sawa na wengine duniani. Just act! Kama nimekuudhi, basi unisamehe. Ila napenda kuona kwamba mtanzania anajisikia yupo sawa na watu wengine wowote duniani, na anatambua uwezo wake na jinsi ya kuutumia.
mtafungwa wachache sana tunajua kuwa tunaweza kusema no kwa baadhi ya mambo lakini serikali yetu ndio wanaosaini mikataba mbalimbali na kutuwakilisha katika mambo mabalimbali. kwani uongo kuwa tanzania ni nchi ya kukubali tu vitu,labda tubadilishe mfumo ndio tutaweza kuwa na hiyo power usemayo, hata hivyo katika mahusiano ya kimataifa sisi ni nani tuna nini? haya ni maswali rahisi ya kujiuliza je ni sera gani ya umoja wa mataifa tuliyopinga ukishakuwa ni sehemu ya umoja wa mataifa china anaweza kusema jambo kwani anaweza kisimama kifua mbele na kuhoji na kupinga na kufanya kila kitu.
narudia tena no power ni international community no right to decide or argue.
nikizungumza tanzania najumuisha pia serikali na haswa serikali kwani ndio watunga sera wawakilishi wa wananchi na wao ndio wasema ndio wakubwa, lakini mtu mmoja mmoja anaweza kujiamini lakini bado kutokana na mambo yalivyo akapata wakati mgumu kufanya anayoyataka kutokana na mambo ambayo serikali tayari imeshaharibu.
tunaweza kuwa na power in east africa community kwani karibu tunalingana kiuchumi ila katika dunia we are yet to have the power.