Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
KUTOKA MAKTABA YA MZEE KISSINGER: PICHA YA KARNE YA 20 YA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Jana tulipokwenda kumsalimia mwalimu wetu Mzee Kissinger nilimgusia kuhusu picha aliyonipa miaka mingi nyuma ya Mzee Mshume Kiyate akimvisha Julius Nyerere Rais wa Tanganyika kitambi mwezi February 1964.
Hii ilikuwa baada ya maaasi yaliyotokea tarehe 20 January Tanganyika Rifles (TR) walipoasisi na ikabidi Mwalimu akimbie kutoka Ikulu akajifiche mahali pasipojulikana.
Kwa kiasi cha siku tatu hakuna aliyejua Nyerere yuko wapi.
Nyerere alirudi Ikulu baada ya maasi kuzimwa na Jeshi la Wanamaji wa Kiingereza.
Mwalimu katika hotuba yake alisema kitendo kile kilikuwa fedheha kubwa kwa Tanganyika.
Lakini Mwalimu Nyerere alijificha wapi?
Peter Mwimbo aliyekuwa Mlinzi wa Rais katika kitabu cha maisha yake anasema walijificha Kigamboni na aneleza namna alivyomtorosha Mwalimu.
Nilipata kuzungumza na marehemu Mzee Kitwana Kondo ambae alikuwa Ikulu wakati ule.
Maelezo ya Mzee Kitwana Kondo kwangu mimi yanapishana na ya Peter Mwimbo.
Lakini mshtuko mkubwa wa kisa hiki cha maficho ya Julius Nyerere niliyapata kwa Bi. Mwajame Dossa Aziz mtoto wa Dossa Aziz aliyekuwa rafiki mkubwa wa Nyerere miaka hiyo.
Bi. Mwajame amenieleza kuwa baba yake alijenga handaki shambani kwake Ruvu kama tahadhari endapo Nyerere atalazimika kujificha kujiokoa.
Nyerere na Dossa mara kwa mara walikuwa wakienda kwenye shamba hili kwa mapumziko mafupi.
Siku ya maasi Dossa alipopata taarifa kuwa Nyerere baada ya maasi hajulikani alipo yeye haraka alikwenda Ruvu kukagua lile handaki lao.
Dossa kutwa nzima hakuweza kupatika hadi usiku alipokwenda kwenye nyumba yake ya Mtoni kwa Aziz Ali kwa mama yake kuwajulia hali.
Yeye alikuwa akiishi Ruvu na mkewe Bi. Nagla Stein chotara wa Kijerumani.
Hapo Mtoni mama yake alimbana Dossa kutaka kujua usalama wa Nyerere kwani alipita asubuhi kumuaga mama yake kuwa anakwenda kumtafuta Nyerere na wao walimsihi asiende mjini kwani jiji zima la Dar es Salaam lilijaa askari kila kona wakipekua watu na magari.
Dossa alikataa kusema lolote kuhusu Nyerere kama amemuona au la alichowahikikishia ni kuwa Nyerere yuko hai.
Mimi nilizungumza na Mzee Dossa nyumbani kwake Ruvu mbele ya Ally Sykes aliyenipeleka kwake.
Mzee Dossa aliniambia kuwa siku ya maasi alitoka kwenda kumtafuta Nyerere akiendesha Land Rover yake na ndani alikuwa na bunduki yake kanitajia kuwa ilikuwa ''Five Repeater," yaani bunduki hiyo ikipiga risasi tano mfululizo kwa mkupuo mmoja.
Bi. Mwajame anasema baba yake akistahika sana Dar es Salaam na askari wote waliomsimamisha njiani hawakupekua gari yake wakimtambua ni yeye wabafungua njia anapita.
Turudi kwa Prof. Kissinger.
Kissinger alinieleza kuwa baada ya Mwalimu kurejea madarakani TANU ilifanya mkutano mkubwa Viwanja Vya Jangwani.
Baraza la Wazee wa TANU lilikuwa lishavunjwa toka mwezi March 1963 na Mzee Mshume alikuwa Mjumbe.
Mzee Mshume alitoka nyumbani kwake na kitambi.
Alipokutana na Nyerere baada ya kumpa pole kwa yaliyomfika alikichukua kile kitambi akamvisha Nyerere kama kielelezo cha mapenzi yake kwake na mapenzi ya wananchi wenzake.
Picha hii ya Mzee Mshume Kiyate akimvisha Julius Nyerere kitambi haikupata kuoenakana popote baada ya kuchapwa katika gazeti mwaka wa 1964 ikawa kama vile haipo imepotea.
Siku Prof. Kissinger alipokamilisha darasa lake kwangu la historia ya maasi ya TR akaniambia, ''Mohamed picha ya Mzee Mshume na Nyerere ninayo Insha Allah nitakupa.''
Picha yenyewe ndiyo hiyo hapo chini.
Hiyo ndiyo picha ya Karne ya 20 kutoka Maktaba ya Mzee Kissinger.
Picha nyingine ni kaburi la Mzee Mshume Kiyate lililopo Kunduchi kwa hisani ya Alwi Mngazija.
Meya wa Dar es Salaam Kitwana Selemani Kondo alimpa Mzee Kiyate Mshume mtaa kwa kutambua mchango wake kwa TANU, Mwalimu Nyerere na familia yake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Sasa inafikia miaka 40 wenye mamlaka wamekataa kuweka kibao chenye jina la Mshume Kiyate Mtaa wa Tandamti aliokuwa akiishi.