VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Inapendekezwa kuwa wale 'Vijana Wakakamavu Wajasiriamali wa CCM' almaarufu kama Green Guards wasivae tena sare zao zinazofanana na zile za Jeshi la Polisi. Mapendekezo hayo yanatoka katika Kitengo cha Propaganda cha CCM Ofisi Ndogo za Lumumba,Dar es Salaam.
Mapendekezo hayo yanafuatia kikao cha kitengo hicho kilichofanyika jioni ya leo. Pia,inapendekezwa kuwa Green Guards wasiwe wanapiga 'salute' kama ile ya majeshi kuanzia sasa badala yake aina mpya ya salamu itatumika.Lakini,bado aina hiyo mpya ya salamu haijaainishwa.
Lengo hasa la mapendekezo hayo ni kuuaminisha umma kuwa CCM haina na haijawahi kuwa na kikundi/kikosi cha ulinzi wa chama na hivyo kuchagiza mapambano dhidi ya CHADEMA waliodhamiria kuimarisha Red Brigade. Mapendekezo hayo yatapelekwa katika ngazi za juu ili kuweza kuamuliwa zaidi na kufanyiwa kazi pale ambapo yatapitishwa. JF itajua juu ya hilo pia.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam