Gorge Mwakalinga ahamia CHADEMA

Gorge Mwakalinga ahamia CHADEMA

Kutoka Mbeya, George Mwakalinga aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Mwakyembe la Kyela mkoani Mbeya, amehamia CHADEMA Muda sio mrefu.

Ni vizuri pia kupata wasifu wa huyu mtu; je, anafahamika kiasi cha kuwa "breaking news". Alikuwa na uzito gani kisiasa na kiuongozi? Na ataongeza thamani gani CHADEMA wakati huu? Sidhani kila (mtu binafsi) anayehamia CHADEMA ni "habari".
 
yani watu kuhamia upande wenu haimaanishi ndio ushindi au ndio kukubalika. Angalieni watu mnaowapokea kuanzia mgombea wenu wa urais ni watu wa namna gani katika jamii?. Wengi wao ni mafisadi na walioshindwa katika kura za maoni na kukimbilia kwenu.

twahil;
Mbona umepotea njia kihivyo?? Hiyo nayo ni sababu ya kuandika humu kweli?? Mshangao wetu ni kwamba, wakiwa huko ccm kwenyu ati ni watu swafiii tena wana udhu. Wakilogwa tu wakihamia upande mwingine, imekuwa nongwa. Hao ni mafisadi, hao ni makapi, hao ni mamluki.... toka lini ccm mkawa washauri wa Chadema???? Ngoja myapate mafuriko hayooooo, hakika mtalia kilio cha mbwa kidomo juu. Msiogope, hata waje woote, tutawapokea tu, siku ikifika wakijona vibaya, warudi huko kwenyu au lile tawi dogo mliloshiriki kuanzisha kama njia ya kupunguza kura za upinzani ACT.
 
CDM inaelekea kugeuka CCM B kwani tutashindwa kutofautisha kati ya vyama hivyo viwili kipi ni kipi. Watu ni wale wale waliocheza segere wakati wa kupitisha katiba pendekezwa iliyopelekea kuundwa kwa UKAWA. Kama kweli wangekua na nia ya dhati ya uchungu kwa taifa letu wangeionyesha kwenye bunge la katiba kama alivyofanya mwanasheria wa Zanzibar. Hao wengine ni watafuta ulaji tu wala sio wanamageuzi.
 
sasa naomba kufahamishwa kiasi cha pesa kinachotakiwa na Tcra ili kuiruhusu kyela fm kuendelea na matangazo , mimi na marafiki zangu tuko tayari kulipa .
 
Dan, huyu ndugu yangu wa damu alikuwa ni CCM hasa yaani wa damu na tayari kufia CCM.......

Nimepata habari kuwa tayari kashapewa ticket ya kugombea kwa kupitia UKAWA......

Kweli mwisho wa CCM ni mwaka huu.....

Kura za maoni aliishia kupata kura elfu 4 huku Mwakyembe akiondoka na kura elfu 15.

Kama Chadema wamempa ugombea basi ni dhahiri kuwa ugombea Chadema unauzwa kwa pesa maana waliishafanya kura za maoni Chadema,na majina matatu yalipatikana.

Sasa kama Chadema inawakata wagombea wake watatu waliokipigania Chama miaka yote kwa ajili ya kapi linalodandia treni keenye uchaguzi baada ya kushindwa kura za maoni CCM basi Chadema kweli haiwatendei haki watu wake.

KWa wasioijua Chadema Kyela ebu jikumbusheni

https://www.jamiiforums.com/uchaguz...a-safari-ya-uhakika-kyela-chini-ya-ukawa.html

https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania/890632-mwanyamaki-aitisha-ccm-kyela.html

Huyu alishinda kura za maoni Chadema, kakipigania chama miaka yote anahangaika kuijenga Chadema Kyela, leo hii mnaokota mtu wa CCM mnawatosa hawa watu, kweli Chadema angalieni sana.Hii sio haki.
 
sasa naomba kufahamishwa kiasi cha pesa kinachotakiwa na Tcra ili kuiruhusu kyela fm kuendelea na matangazo , mimi na marafiki zangu tuko tayari kulipa .

Umeishamtosa mtu wako uliyekuwa unampigia kampeni sikuzote humu?kweli Chadema pesa mbele kuliko misingi.
 
Ni vizuri pia kupata wasifu wa huyu mtu; je, anafahamika kiasi cha kuwa "breaking news". Alikuwa na uzito gani kisiasa na kiuongozi? Na ataongeza thamani gani CHADEMA wakati huu? Sidhani kila (mtu binafsi) anayehamia CHADEMA ni "habari".

Wasifu wake muulize JF Member anayeitwa Mtanzania,anamjua vizuri sana
 
Lazima mjiulize hao wanaohama ni kwa maslahi ya wananchi au ya kibinafsi? Kumbuka wote waliohama wakiongozwa na EL wanatoa sababu za kuwa hawakutendewa haki katika kupata madaraka, hakuna aliyesema kahama ili kusaidia wananchi.
Atasaidiaje wananchi akiwa kwenye lichama la wanyonyaji Ccm? Amekuja kwa makamanda ili kuongeza jeshi nguvu
 
CDM inaelekea kugeuka CCM B kwani tutashindwa kutofautisha kati ya vyama hivyo viwili kipi ni kipi. Watu ni wale wale waliocheza segere wakati wa kupitisha katiba pendekezwa iliyopelekea kuundwa kwa UKAWA. Kama kweli wangekua na nia ya dhati ya uchungu kwa taifa letu wangeionyesha kwenye bunge la katiba kama alivyofanya mwanasheria wa Zanzibar. Hao wengine ni watafuta ulaji tu wala sio wanamageuzi.

Kwani magufuli na mwenza wake walifanya nini kunusuru katiba ya wananchi? ukawa tulisimama na wananchi na tunakaribisha wote waliolemewa na mizigo ya ccm.UKAWA ndiyo habari ya mujini
 
Alikatwa?

Haa ha ha unauliza kirungu polisi?malaya wa kisiasa uwa wanahama baada ya kukatwa;

JIKUMBUSHE

WAZIRI wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela anayemaliza muda muda wake, ameshinda kura za maoni katika jimbo hilo akiwabwaga wagombea wenzake tisa waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kyela, Eva Degeleki alisema Dk Mwakyembe aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 15,516 akifuatiwa na George Mwakalinga aliyeambulia kura 4,905.
 
Kura za maoni aliishia kupata kura elfu 4 huku Mwakyembe akiondoka na kura elfu 15.

Kama Chadema wamempa ugombea basi ni dhahiri kuwa ugombea Chadema unauzwa kwa pesa maana waliishafanya kura za maoni Chadema,na majina matatu yalipatikana.

Sasa kama Chadema inawakata wagombea wake watatu waliokipigania Chama miaka yote kwa ajili ya kapi linalodandia treni keenye uchaguzi baada ya kushindwa kura za maoni CCM basi Chadema kweli haiwatendei haki watu wake.

Hawaji cdm kutafuta vyeo kwani tulishamaliza kura za maoni.wanakuja kuongeza nguvu ili mabadiliko ya kweli yapatikane
 
Ni vizuri pia kupata wasifu wa huyu mtu; je, anafahamika kiasi cha kuwa "breaking news". Alikuwa na uzito gani kisiasa na kiuongozi? Na ataongeza thamani gani CHADEMA wakati huu? Sidhani kila (mtu binafsi) anayehamia CHADEMA ni "habari".

Nimemkumbuka huyu jamaa wale wakongwe wa JF watakuwa wanamkumbuka huyu jamaa alikuwa anajulikana kama MTANZANIA Hapa JF.Hajawekwa tu hapa ni mtu maarufu sana na Siasa za uko Mbeya na ni mmiliki wa redio Kyela FM.Ni kiongozi mzuri sana atawasaidia sana chadema Kyela kujijenga.Huyu atamshinda Mwakyembe pamoja na pesa zake za Mabehewa Mabovu hizi pesa ndo zilitumika kununua wana ccm
 
yani watu kuhamia upande wenu haimaanishi ndio ushindi au ndio kukubalika. Angalieni watu mnaowapokea kuanzia mgombea wenu wa urais ni watu wa namna gani katika jamii?. Wengi wao ni mafisadi na walioshindwa katika kura za maoni na kukimbilia kwenu.
Kura zipi hii onayolalamikiwa kila eneo
Haya magoli ya mikono mnayofungna?
 
Hawaji cdm kutafuta vyeo kwani tulishamaliza kura za maoni.wanakuja kuongeza nguvu ili mabadiliko ya kweli yapatikane

Ndio uijue Chadema yako, kura za maoni ziliishafanyika,na washindi walipatikana, lakini Chadema imempa ugombea huyo George Mwakalinga, hivyo kaambiwa atangaze sasa kuingia Chadema ili tangazo la kuwa mgombea lifanyike akiwa tayari Chadema.

Ndio mjue chama chenu sasa kipo sokoni, ukiwa na pesa tu ata kama hukuwepo kura za maoni basi unateuliwa tu kuwa mgombea.
 
Back
Top Bottom