Goodbye my friend

Goodbye my friend

hivi hapa duniani kweli hakuna vifo vya kizembe?
ni kweli kuwa vifo vyote ni mipango ya Mungu tu?

hicho kifo siyo mipango ya mungu ni mipango yake na mwenye mke wakishirikiana na shetani
 
Nasikitika nimepata taarifa za kunishtua cha kifo cha rafiki yangu tulikuwa sote kitambo udsm, amefariki baada ya kuwekea sumu kwenye beer, mshikaji alishaoa ila inasemekana alikuwa anatoka na mke wa mtu na mwenye mke alishamuonya,tafadhalini mabibi na mabwana heshimuni mahusiano yenu, Nimesikitika sana,mkewe ni mtu mzuri sana hata siwezi kuongea nae at the moment, nilikuwa kazin nimeamua kurudi nyumbani kichwa hakifanyi kazi.

pole sana ndugu sokwe, kifo hicho ni somo kwa tuliobakia kwani Mungu amesema ktk kitabu cha MITHALI 6:32-35 'Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi.......' hatuna budi kufahamu kuwa neno la Mungu ni kweli, tazama sasa jamaa yako amepoteza si tu nafsi yake bali na roho yake, Mungu Atusaidie
 
Asante kwa nasaha zako ndugu shimilimana.
 
tujifunze siku zote kuwa kila kisicho chako ni hatari ni hatari kuchukua. sasa we wachukua vya wenzio halafu unatembea mtaani kwa amani kabisa na baa unakaa unakunywa?

mungu amlaze roho yake mahali panapostahili. pole mleta mada kwa kuondokewa na rafiki yako.
 
Inasikitisha ila we all have choices in life, there's always going to be consequences for our action,good or bad.
 
POLE sokwe mungu amuweke marehemu panapo stahili.
 
Last edited by a moderator:
pole ndugu lakini nmeshanga hiyo habar huku dodoma mtaa mmoja kuna kijana amefariki na kisa ni kma hiko yeye amefariki jana na alikua askari
 
Hapana sio Dodoma jamaa kwao tabora, labda matukio yamefanana tu.
 
Pole kwa msiba ni funzo kwa tuliobakia. Tuekee picha nasi tumjue pengine tumesoma nae UDSM.
 
Kwani ukitaka kununua shamba inakuwaje? Muhusishe mjumbe wake na akuonyeshe referee watatu wenye mali zisizohamishika.
haya mambo unadanganywa sijui sikusikia simu yako, simu ilikuwa mbali (as if nyumbayake ina kilomita za mraba tatu kama maiko jakisoni), ooh nilizima simu. Nani anataka kutapeliwa. Ukimdate wiki tatu na hawezi kukukaribisha kwake tupa kuleeee
hiyo ndio balaa......hata sisi tunapata shida sana kujua kama mmeoa......Dah...pole sana sokwe......mapenzi yameshakuwa shubiri sasa haya..........
 
Hapana haitakuwa busara kutaja jina lake hapa, ila alikuwa mhandisi kwenye mgodi shinyanga, nilizungumza nae Kama siku 5 zilizopita tumeongea mengi kuhusu maisha na kuonyesha ni mwenye furaha na ndoa yake na career yake, nikamuahidi kwenda kuwatembelea nikianza likizo, inauma sana, Asante preta! Mzima lakini?

ilikuwaje huo mstari ulinipita........am doing great.....thanks.........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom