GONGO yauwa watu 7 kigogo mbuyuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

GONGO yauwa watu 7 kigogo mbuyuni

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by GP, Jul 12, 2012.

 1. GP

  GP JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  habari ya kushangaza kidogo, watu 7 wafariki na wengine wapo hoi wamelazwa hospitalini kwa kunywa pombe haramu ya GONGO!,
  hiii gongo iliwekwa nini wakuu?, mavi au?
   
 2. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Acha wafe! Kwani hawajui kuwa niharamu? Mshahara wa dhambi ni mauti.Hivyo mimi sishangai.
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hapana mkuu, hizi pombe za kienyeji haziangaliwa vizuri kwa mapana. Nikimaanisha kuwa, kama tungekuwa serious na vitu vyetu kuanzia hizo pombe za kienyeji tungekuwa tumeshaziboresha kwa kuzipunguzia baadhi ya contents ambazo ni sumu/hatari kwa afya ya binadamu pamoja na usindikaji mzuri na packaging yake ili kuongeza ajira pamoja na pato la ndani. Lakini kwa kuzipuuza hizi pombe tunadharau vitu vyetu vya asili na kukimbilia vya wazungu. Gongo haina tofauti na Vodka, konyagi, Gordons, John-Walker Black/Red label, etc isipokuwa packaging tu. Ukienda Asia, watu wanatukuza pombe za kienyeji kuliko hizi bia na zimefanyiwa research hazina madhara.
   
 4. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  wapumzike pema peponi,amen
   
 5. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sisi hapa kwetu ukiachilia lubisi kuna pombe ya gongo ambayo inanywewa sana na madhara yake nadhani sio makubwa sana maana karibia ni sawa na Konyagi au whisk zingine.
  Lakini wakuu tusisahau pia kuwa uwezo wa mwananchi kununua bia ambayo nasikia sasa ni Tsh. 2,000/- unazidi kushuka kutokana na kuporomoka kwa uchumi wa taifa huku mfumuko wa bei ukielekea tarakimu tatu, so, kimbilio ni hizo pombe na sababu ya mahitaji kwenda juu, watengenezaji wanachakachua nao!

   
 6. cement

  cement JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele wakuu

  Toka juzi hadi jana kumekuwa taarifa hii ya habari ya mpaka jana jumla ya watu saba wameshafariki akiwemo muuza gongo mwenyewe akiongea na vyombo habari kamanda wa Polisi kinondoni amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na uchunguzi unaendelea japo mpaka ss hawezi sema lolote kwani hadi muuza pombe mwenyewe amefariki jana.

  hii nimara ya kwanza kutokea kwa tukio la namna hii Dar,kuanzia jana hiyo hiyo baadhi ya matangazo yameanza kutolewa kwa kuwatangazia kuwa yoyote aliye tumia pombe ile ajitokeze ili apewe huduma ya kwanza japo zoezi linakuwa gumu watu wanaona aibu mpaka wanapozidiwa!

  Pombe hy inasadikiwa kuwa ilichanganywa na spiliti na Jiki ya kufuria  my take
  pombe hii ni hatari walio kunywa wajitokezeeeeeeeeeeeeeeeee wasijifiche...
   
 7. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Mkuu mtu anahisi anataka kufa you think ataona aibu kujieleza? hao siku yao ilifika tu...
   
 8. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Duh! Ngoja nijitokeze litakalo kuwa na liwe
   
 9. cement

  cement JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ahahhaa sema wadu wanaogopa wanaona aibu jana mmoja kabebwa yuko hoi hadi itv walimuonesha taarifa ya habari ss watu wanasema wako wengi sana waliokunywa!!
   
 10. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ndo maana kuna baadhi ya members siwaoni humu, RIP wana Jei eF mliotangulia.
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  jana nimeona watu wanavyobebwa wakiwa hoi nimesikitika kweli. Kumbe dar bado kuna sehemu gongo inapatikana?
   
 12. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 852
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Huu unywaji wa pombe hii ("HARAMU???"), kwa kweli umekithiri! Nashangaa ni kwanini serikali pamoja na kuiita haramu, lakini hjaichukui hatua madhubuti za kuidhibiti au kuwadhibiti wauzaji na wanywaji pia.
  Maeneo ninayoishi huku Mwenge karibu kabisa na kambi ya JWTZ kikosi cha Ujenzi, kumekithiri unywaji wa pombe hiyo! Wahusika (Polisi, Serikali za mitaa, nk.) wanafahamu yote haya lakini hawashituki hata!
  Labda wanasubiri (kama kawaida yao) yatokee maafa kama ya Kigogo ndo watalifanyia kazi!
  Chonde Chonde wahusika; Nguvu Kazi inazidi Kuangamia!
   
 13. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tumezoea kusikia matukio kama hayo kutoka slums za Kibera kando kidogo ya Nairobi. nasikia mmoja wao alidai wawashe taa akidhani zimezimwa kumbe ndio macho kwa heri. Shusha bei ya bia tuokoe watu
   
 14. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hao ni kuwapa uwezo na kuwatengenezea sheria ambazo zinalinda interests za pande zote. Zidhani kama hizo pombe zikifanyiwa marekebisho zitakuwa ni haramu tena. Tutaanza kusikia hadi ikulu wanakunywa Gongo au Professor mzima anapiga gonga sababu zitakuwa hazina madhara tena. Mfano: wanaweza kuongezea nutrients ambazo ni mhimu kwenye miili ya wanadamu. Lakini kwa sababu kila kitu tunaimport, utasikia oooh ni hatari mara haifai kumbe watu wanapoteza ufisasi sehemu. Ndiyo tunaipinga hii serikali isiyoona tuko katika karne ya ngapi.
   
 15. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  M2 wangu nackia iliwekewa spirit na jiki we kilichotokea anajua marehemu.
   
 16. cement

  cement JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli hata me nimeshangaa sana kama jiji la Dar tena katikati pombe ya namna hii bado inapatikana!!
   
 17. GP

  GP JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  sehemu zote dar zenye mambo ya kiswazi hata ushuani gongo inapatikana!.

  mkuu dar gongo inapatikana kwa WINGI wala usishangae!,
  mi naishauri serikali ipunguze bei ya bia, vinginevyo watu wengi sana watatedi.
  mama mmoja aliyeathirika na tukio hilo akiwa kitandani hospitali anasema eti alichanganya gongo glass mbili na bia, jamani jamani, jamani GONGO + BIA kweli tutapona?? tena demu huyo!.
   
 18. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hii pombe ya gongo ifanyike namna ya kuruhusu TBS kuitembelea huko wanakotengenezaga!

  Yaelekea ilikuwa kali sana!


  Poleni wafiwa wote!
   
 19. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  vipi, hili tukio nalo limepoteza watu karibia kumi tena makao makuu ya nchi, Dar es Salaam; Mheshimiwa Kova hajaliundia tume ya uchunguzi????
   
Loading...