Hivi inakuaje mtu kufanya hivi?

Killing machine

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,430
1,648
Leo nilikuwa nimetoka ofisini Sasa kwa bahati mbaya kifurushi changu Cha mwezi kikawa kime niishia

Na Kibaya zaidi ninapo kwenda siwezi kwenda bila kuwa na mda wa maongezi

Nikaona ni vema nichukue vocha kwanza kabla Sija Anza safari yangu ya kwenda huko ninako taka kwenda

Eneo letu la kazi pembezoni Kuna sehemu ni grocery lakini pia Wana m.pesa na Huwa wanauza na voucher pia

Sasa nikafika pale nikawa kuta vijana baadhi wanapata vinywaji vyao pale nikawa salimia Kisha Nika agiza voucher

Wakati najiandaa kutoa Hera Kuna kijana mmoja miongoni mwa wale walio kuwa wame kaa pale Wana kunywa

akaniambia kwa kujiamini we brother ninunulie pombe."

Nika muuliza Mimi?

Akajibu ndio wewe hapo."

kwa sauti ya kukaza"

Sasa nika mtazama nikagundua Kwanza amelewa tayari japo so sana

lakini pili mda anao kunywa pombe ni mda wa kazi hakustahiri kuwa pale mda ule kwa kijana anaye jitafuta

badara yake alipaswa awe kazini au kutafta kazi ili kuitafta hatima yake ya jioni anapo ludi nyumbani

Nikajisemea moyoni kwamba angeniomba Hera ya kula alikiwa sahihi lakini pombe na kwa Hari hii aliyo nayo spaswi kumpa

Basi nika mjibu kwamba Sina Hera aisee Niko vibaya boss wangu,..

Chaajabu na cha kushangaza akadakia kwa sauti kubwa akaniambia afu we bigi nilikuwa nakuheshimu kumbe ni k...u...m...kabisa eti?""

Una vaa smart Hera hata ya pombe moja huna matako wewe"una nini wewe huna hata Mia hapo?

Aiseeh. Nilijikuta nime lipukwa na hasira za gafra

pembeni Kuna brother mmoja alikuwa ameshika chupa ya soda huku aki mshangaa yule jamaa

Nilitamani niichukue Ile chupa nimnyooshe kisawa sawa yule jamaa lakini nikaona si busara kwani jamaa amelewa itaonekana nilipigana na mlevi

na watu wote mle ndani walikuwa wameduwaa kwa mshangao

na istoshe na mfahamu fahamu kwani anashinda eneo la jirani na ofisini kwangu

Nilicho kifanya Nika waza haraka haraka nikaona huyu acha nimalizane nae kwa hakiri siwezi kimwacha hivi hivi huyu boya

Nika muuliza kwa upole kwamba Je! unataka nikuonyeshe nilicho nacho?

Akajibu kwa jazba na kujiamini ndio nionyeshe tuone unanini wewe?""

Nikachomoa wallet nikatoa shilingi lakimoja nikamuuliza umeniita k. Sindio?

unaweza kunionyesha hata robo au theruthi ya kiasi hiki au hata alfu mbili ya kisungura hicho unacho kunywa ?

Akabaki ametoa jicho tuu huku akitazama Hera nilizo kuwa nimezi shika kwa macho ya uroho

nikamwangalia nikaona huyu boya kalowa tayari

Nika muuliza Tena kwa upole nikasema Sasa ndugu yangu unaniitaje Mimi k...u..m...a. wakati huna hata alfu mbili mfukoni af mtoto wa kiume?

Nikakuta kazu baa na Ana Anza kujiregeza Kama mtoto wakike ambaye yupo tayari kutoa tunda

Nika mtazama Nika kaa kwenye kiti Kisha nika mwambia.

Sasa nilikuwa na haraka lakini naona leo acha tupige story kwani hatu fahamiani vizuri au sio?
Akaitikia fresh big Mani kwa sauti ya puani.

Nika muuliza hiyo pombe Bei gani kwani mpaka tunafikia hatua ya kutuka Nana boss wangu?

akadakia buku mbili tuu big Mani"

nika mwabia Tena kwa upole unaone Kama una hamu Sana na pombe mwanangu au sio?

Akajibu Sana brother" nikaona hazija mkaa sawa bado huyu.

Nika mwambia yule brother mwenye Ile ofisi naomba umpe huyu jamaa visungura kumi af namimi hapa nipe maji ya bariidi tuendelee kupiga story na jamaa yangu hapa

Yule mhudumu akamuuliza yule jamaa huku akimkazia macho eti eti nikupe visungura kumi uta maliza ?

jamaa likajibu lete hizo namaliza mwenyewe na hakuna mtu kugongea nilijuatu atani nunulia nikimchokonoa huyu big mani huku liki cheka cheka

Nika mwitikia au sio mi mwenyewe nilijua unatania tu haukuwa siliasi huku nikimkenulia meno kinoko

Basi Akaletewa pombe zake bwana na mimi Nika mwambia jitahidi umalize ukishindwa utazilipia mwenyewe lakini huku nikiwa nime mkazia sura kidogo

Likaitikia mbona Cha mtoto hiziii.basi nikasema sawa

akapiga yakwanza kufika ya tano nikakuta jamaa Ana Anza kulegea hata story nnazo mpigisha anashindwa kujibu

Haukupita mda Sana Yule mhudumu akatoka nje

Ile ana Rudi hajakaa hata dakika mbili akaja mtendaji ananiambia nimeskia habari yako bwana killing machine

Naomba Kama mtendaji wako na tuna heshimiana msamehe kijana huyu

asije aka umaliza mwendo kesho serikali ikatu dai mtu wao

Nika mwambia yule mtendaji amuulize amekubari kushindwa/katosha?

jamaa akaitikia kwa kunyenyua kichwa mzee akasema Basi mwache

Skuongea kitu wakuu zaidi ya kuwaambia vijana wengine waendelee kunywa zilizo Baki

Nika mtuma na kijana mmoja akanunue maziwa mabichi Lita moja wamnyweshe ndugu yangu iwapo Hari yake itaendelea kuwa mbaya zaidi Kisha nikaishia zangu

Sasa mpaka Sasa najiuliza huyu jamaa kwanini alifanya vile kwangu?

Je watu Kama Hawa Huwa wana jiamini Nini kufanya hivyo?

Ningeomba Kama Kuna wataaram wa mambo kama haya watufafa nulie kidogo

kwamba kwanini mtu ana mchukia/au kumzoea mtu ambaye hajawai hata kupiga nae hata story?

Na kingine nikwamba..

Kiukweli kahera kangu kame niuma Ila hata moyo wangu naona umejawa na tabasamu mwanana humu ndani kwangu..,,

Niwatakie jioni njema wakuu zangu 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom