God's time is a myth, The strategy of redundancy

God's time is a myth, The strategy of redundancy

Kwanza, kudai kwamba Uislamu unazungumzia “pono na bikra 72 tu” ni hoja dhaifu sana (strawman argument). Qur'an ina aya zaidi ya 6,000 zinazozungumzia tawhidi, maadili, haki, uchumi, elimu, sayansi ya kutafakari maumbile, na uwajibikaji wa mwanadamu. Kupunguza dini nzima kwenye simulizi moja ni ama ujinga au upotoshaji wa makusudi.

Pili, kusema “Allah hayupo” si hoja ya kisayansi bali ni msimamo wa kifalsafa. Sayansi huchunguza jinsi vitu vinavyofanya kazi, si kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kitu. Hata nadharia ya Big Bang haijibu chanzo cha uwepo , inaeleza mwanzo wa upanuzi wa ulimwengu unaoonekana. Swali la chanzo cha sheria za fizikia na uwepo wa kitu badala ya utupu bado lipo.

Unaposema Qur’an haizungumzii Big Bang, hiyo si kweli kabisa. Aya inayosema mbingu na ardhi zilikuwa kitu kimoja kisha zikatenganishwa haidai kuwa ni kitabu cha fizikia, bali ni ishara ya asili ya ulimwengu kuwa na mwanzo mmoja. Hata wanasayansi wakubwa kama Georges Lemaître — aliyependekeza nadharia ya Big Bang alikuwa padre. Hivyo kuamini Mungu na kukubali cosmology ya kisasa si vitu vinavyopingana.

Swali lako “kama Allah ndiye mwanzilishi wa muda na maada, nani aliyemwanzisha Allah?” lina tatizo la kimantiki. Kama muda ulianza na uumbaji, basi kuuliza “kabla ya Mungu” ni sawa na kuuliza “kaskazini mwa North Pole ni wapi?” — ni swali lisilo na muktadha. Kwa ufafanuzi wa kitheolojia, Allah si kiumbe ndani ya muda; Yeye ndiye sababu isiyosababishwa (Necessary Being). Huwezi kumuweka Muumba ndani ya mfumo aliouumba.

Kuhusu utumwa na ukoloni, historia haiko upande wako kama unavyodhani. Nchi zilizofanya biashara ya utumwa kwa kiwango kikubwa zilikuwa za Ulaya za Kikristo kisha zikaja kuzalisha falsafa ya Secular humanism baada ya mapinduzi ya kielimu. Lakini kabla ya hapo, Uislamu uliweka mfumo wa kupunguza na kuondoa utumwa kwa njia ya hatua kwa hatua karne nyingi kabla ya Ulaya kuamka. Leo hakuna mfumo mkamilifu; hata mataifa yanayojitangaza kuwa ya “human rights” bado yana vita, ubaguzi na unyonyaji wa kiuchumi.

Hoja ya msingi hapa ni hii, kutokubaliana na dini hakufanyi dini iwe ya kijinga. Na kuamini sayansi hakumaanishi lazima ukatae uwepo wa Mungu. Sayansi inaeleza mechanism. Dini inaeleza meaning.

Ukosoaji wenye nguvu unahitaji uelewa sahihi wa unachokikosoa. Vinginevyo, kelele zinabaki kelele na si hoja.
Kusema ukweli kwamba mnafundisha vijana wa kiume kujiandaa na show ya Ponografia watakayocheza na bikra 70 iliyoandaliwa na Allah Mungu wa Maadili, inawezaje kuwa Strawman Aurgment?

Wewe unaamini kuwa Allah is the necessary being, hiyo ni Imani yako, yaweza kuwa kweli au yaweza kuwa Uwongo, Sasa unachopaswa kufanya ni uthibitishe beyond reasonable doubt kwamba Allah ndiye mwanzilishi na kwanini mwanzilishi asiwe ni Brahma, Yawheh, Baal, Mazda, El, Krishna, nk.
 
Uhakika kimsingi ni hali ya kutokuwa na shaka. Ni hisia inayotokea akilini mwako.
Si lazima uwe ukweli. Unaweza kuwa na uhakika wa uongo, na unaweza kuwa huna uhakika wa jambo ambalo kwa kweli ni la kweli.

Kwa ufupi kabisa: Ukweli ni hali ya kuwa sahihi au kupatana na uhalisi (reality).
Uhakika wa uongo!!

Hii ndio nimesikia kwako.😂

Utakuwaje na uhakika wa uongo?

Wewe unajichanganya sana. Una mix mafaili.
 
Uhakika wa uongo!!

Hii ndio nimesikia kwako.😂

Utakuwaje na uhakika wa uongo?

Wewe unajichanganya sana. Una mix mafaili.
Uhakika ni hisia tu za kutokuwa na mashaka, uhakika na ukweli ni vitu viwili tofauti. Mfano watu wengi huwa hatuna mashaka na wale tunaowatambua kuwa ni wazazi wetu ingawa hatujafanya DNA ili kupata ukweli ila huwa tuna uhakika kuwa hawa ndio wazazi wetu, lakini inaweza isiwe kweli.

Mara ngapi mtu anaweza kusema kwa uhakika kafanya kitu fulani ila kumbe sio kweli amechanganya tu mafaili hajafanya hicho kitu, au labda mtu kutokuwa na uhakika(mashaka) kama alifunga mlango wake wakati anatoka kwake, lakini kumbe ukweli ni kwamba aliufunga huo mlango ila kasahau na kufanya kutokuwa na uhakika.

Kwahiyo ukweli ni kitu ambacho kinabaki kuwa kama kilivyo hakibadiliki kwa wewe kuwa na uhakika au kutokuwa na uhakika, kwa sababu uhakika ni hali ya kutokuwa na mashaka tu na si kwamba ndio ukweli wenyewe.
 
SAsa kama sio 100% navyenyewe vinajinasibu 100% (hata wale wa inspired) si mgogoro huo tayari unaanza


Hao wasioamini mauchawi si watakua wanapingana na vitabu vyenyewe.

concept nzima inaweza kusound bila vitabu ofcourse kama miaka hiyo ya zamani , ila kwasasa kwa declaration ya vitabu inakua ngumu kuviweka mbali na ndo lawama zinapoanzia hapo.

Ndo maana kuna watu wanaswma hii framework yenyewe yote inashida huwezi wapa watu mgogoro wa fikra, alafu wakianguka upande wapili wanaenda kula kiberiti. --- jambo hili bila hata vitabu , ila wakija wenye quatations huwaambii kitu
Sasa mkuu hayo unayouliza na kuelezea ndio huonyesha hivyo vitabu sio maneno ya Mungu au unaonyesha tu migogoro iliyopo kwenye hivyo vitabu?
 
Sasa mkuu hayo unayouliza na kuelezea ndio huonyesha hivyo vitabu sio maneno ya Mungu au unaonyesha tu migogoro iliyopo kwenye hivyo vitabu?
wadau waliobobea kwenye kupambana na madhaifu ya vitabu wapo wengi tu hata humu jamvini , na huwa hawapewi majibu ya kueleweka mkuu .

hiyo migogoro mara nyingi uenda kuchallenge sifa za muumba , natumai umenipata mkuu.

wewe labda nikuulize swali huo upande uliopo wewe , wa upande wapili ata kama wanania njema wanafika mbinguni?
 
wadau waliobobea kwenye kupambana na madhaifu ya vitabu wapo wengi tu hata humu jamvini , na huwa hawapewi majibu ya kueleweka mkuu .

hiyo migogoro mara nyingi uenda kuchallenge sifa za muumba , natumai umenipata mkuu.

wewe labda nikuulize swali huo upande uliopo wewe , wa upande wapili ata kama wanania njema wanafika mbinguni?
Mkuu Mungu anaelezwa kwa sifa nyingi tu kwenye hivyo vitabu, shida ya hiyo challange inahusu Mungu mwenye sifa tatu tu(upendo,ujuzi,uwezo wote) ila tofauti na hapo hiyo challange inakuwa haina maana.


Tatizo wengi humu wanajiingiza kwenye ukanaji Mungu kimkumbo, mtu anatumia nguvu chache mno kufikia hitimisho la kukana kuwepo Mungu ila anaenda kutumia nguvu kubwa katika kupinga kuwepo Mungu.
 
Nilipo sikia wana mwachia Mungu yale matukio ya October ndio ni nikajua hakuna kitu kinaendelea tena
ni kauli ya kijinga sana,ni uvivu wa kufikiri namna ya kutoka kwenye mkwamo nikisikia mtu kaongea hivyo huwa najua hamna kitu hapo
 
Mkuu Mungu anaelezwa kwa sifa nyingi tu kwenye hivyo vitabu, shida ya hiyo challange inahusu Mungu mwenye sifa tatu tu(upendo,ujuzi,uwezo wote) ila tofauti na hapo hiyo challange inakuwa haina maana.


Tatizo wengi humu wanajiingiza kwenye ukanaji Mungu kimkumbo, mtu anatumia nguvu chache mno kufikia hitimisho la kukana kuwepo Mungu ila anaenda kutumia nguvu kubwa katika kupinga kuwepo Mungu.
framework ya mbinguni ipo complicated mkuu hujo kwenye abrahamic , walio amini wapo sahihi na wasio amini wapo sahihi pia

Mbona mkumbo wa kwenye kuamini huuongelei unakomaa tu kwa wasio amini.

mtu toka utotoni anaingizwa kanisani au msikitini (na hizi pande zote kila mtu anasema mwenzake anaenda kula kiberiti) --- wewe kama hadi hapa huoni shida ni wewe mkuu,

Huyo mtoto hata kama wazazi wake hawajali hii system ya shule sehemu nyingi dini ni kama mandatory , kama huna upande chukua upande ratiba za shule ziendelee


Kuona waliokataa tu ndo wanakataa kwa mkumbo hapa huwezi kua sahihi, humo makanisani au misikitini mbona wengi tu wanaenda kama desturi tu.

kila mtu anajua sababu zake zilizomfikisha conclusion aliyofikia, hizi discussion ninkuchangamsha genge tu,
 
Wakati waongo wanaandika bibilia hawakujua kama kulikuwa na sayari zingine tofauti na Dunia 😂. Teknolojia inawaumbua.

Wao walichokuwa wanakijua ni mbingu (juu mawinguni) na Dunia (nchi) maana vilikuwq vinaonekana.

Ndiyo maana kwenye bibilia sijawahi kukutana na msamiati kama zuhura, zebaki, sumbula n.k.

Nyambafu sana wale wazee walioleta habari mungu.
Wangese Sana Kwa kweli 🙌😄
 
Nguvu ipo tena kubwa sana watu hawajui tu
Hapo Sasa mnachanganya mambo Nyinyi m amzungumzia mungu mwenye hizo nguvu kuwa ni kama kiumbe mean while atheist tuna amini kwamba hiyo nguvu Ina ya support mambo yote duniani na angani ni Nguvu ya asili tu Ipo hapo
 
So, If God knew right from the beginning that humans would one day sin, Don't you see his work of creation is imperfect?

Why a perfect God creates imperfect humans who can sin?

If there's freewill, why can't you use it to go back in time?

If truly freewill exists, Can you use it to go back in the year 1980?

If everything was created perfectly, Who tempted Satan to Sin?

If God created everything perfectly, What tempted Satan to sin?

Remember that your scriptures say everything was created perfectly.
Muue 🤣
 
Vitu vingine majibu yake yameandikwa unapata uvivu gani kusoma maandiko?

Kasome maandiko yana majibu yote haya!

Huyo shetani hakuwa mwanadamu aliumbwa perfectly akaingia tamaa mwenyewe ya kuchukua nafasi ya Mungu! Ndiomaana alitupwa pampja na jeshi lake lote! Akaona haitoshi akawadanganya adam na eve bustanini , matokeo ya hiyo dhambi ya asili ndiyo tunayaishi leo!

Hiyo free will haihusiani na wewe kugeuza mchanga maji! Free will
Ni uwezo wa kuchagua matendo! Sio miujiza ya kuamua ukaishi hewani au baharini, sijui kurudi 80s thats crazy lol
So my dear dhambi ya adamu na Hawa wewe Ina kuhusu nini !? Unataka kuniambia mfano ikitokea Mjomba wako akavunja Sheria na kufungwa gerezani inapaswa na family yake yote ifungwe !?

Kama ikitokea ndugu wa family ya Mjomba wako nayenyewe ikafungwa kwaajili ya makosa ya Mjomba wako Utaridhika na maamuzi hayo ya kisheria !? Hauoni kwamba waliotoa hiyo hukumu watakuwa wametoa huku Kwa kupitia Sheria kandamizi!??


Huyo Mungu wenu mbona ana onekana ana matatizo kichwani !? Kwanini uwahukumu watu wengine Kwa makosa ambayo hawajawahi kuyafanya !? Ina maana basi mungu anashindwa Akili hata na watendaji wa hizi mahakama za serikali ya ccm !!!

Huyo Mungu ni wavisasi hapaswi kuabudiwa
 
hahaa nikikuuliza ulipataje majibu utasema ulipata ndoto/maono/ufunuo

Jiulize kwanini matatizo hayaishi maishani mwako...

Twende kwenye mada ya uzi, watu wengi sana wacha Mungu wanakufa bila kujibiwa maombi yao.

Visingizio ni vingi mara Mungu hakupi unachotaka bali unachostahili, mara mipango yake haichunguziki, sasa kwanini aliwaambia muombe naye atawapa?

Ukifikiria unaona haya mambo ni uongo tu.
🤣🤣
 
kwani tamaa ndiyo inatufanya sisi kuonekana tuko imperfect
Mungu muweza wa yote alishindwa Nini kukuumba ukiwa Hauna tamaa !? Huo uweza wake wa yote uko wapi kama alishindwa kukuumba ukiwa Hauna Tamaa !?

Wafia dini bwana mna drama sana
 
Back
Top Bottom