God's time is a myth, The strategy of redundancy

Hakuna sehemu nimekwambia contradictions hutoa jibu kwamba hakuna kitu hicho.

Nimesema hivi...👇

Tutajuaje kwamba hiki hakipo kwasababu ni kweli hakipo au kipo ila umekosekana tu uthibitisho wa ku prove kipo?"
Kuhusu tutajuaje kama kitu hakipo kweli nishakujibu.
 
Ndiyo maana maswali mengine huwa sioni umuhimu wake hapa.
mwanzo nilikuambia watu wa aina yenu ni ngumu kukabiliana nao kwa hoja.

wewe unapokwama ni kuchukulia hiyo mnaita atheism ni kama kundi lenye mawazo sawa , atheism kwa ninavyoelewa mimi wanaktana sehemu moja ambayo haina shaka , ni kwamba kaja huyu na imani/dini yake na anasema huu ndo ukweli - wao wakiangalia wakiona kuna vitu havimake sense wanaona hapa kuna utapeli.

wawe na uhakika au wasiwe na uhakika wa kwamba hayupo - it doesn't matter as long as mtu akija na habari za imani yake ya kuanza kuwaeleza njoeni huku inabidi huyo mtu awe na hoja za kutosha na za kukidhi maswali yao (maswali yawe yana makesense au lah - ila wanatakiwa wajibiwe) unless useme tu ni just gambling kwamba aisee ujumbe umeshausikia ukikaidi unaenda kula kiberiti.

anayetakiwa kutoa uthibitisho pasinashaka yule anayesema kitu hiki kipo hivi na vile

mkuu kama wewe unafikra huru kama usemavyo fatilia kisa cha huyu jamaa Daniel everett

alienda maporini huko amazon, kueneza dini kwa makabila ya misituni, lakini akaondoka kaacha dini na akabobea kama msomi wa mambo ya lugha kapambana hadi na theory za kina choamsky kwenye mambo hayo ya lugha baada ya kugundua kitu kwenye lugha ya hilo kabila la piraha

sasa kama wewe ni fikra huru youtube kuna kama vimakaa fulani anaelezea ilikuaje lile kabila badala ya yeye kuwapa dini likamfanya yeye aache dini hadi kupeana talaka na mkewe maana wote walikua watu wa kueneza dini --- kisa cha huyo jamaa tusikichukue kama ndo authority ya kupinga dini , ila kama wewe unasema huwaelewi atheist na unafikra huru naamini utapata mwanga wa kuelewa their perspective --- alafu sasa wewe kama muumini utajipima kama unaweza wapa muongozo au lah katika framework ya imani iliyopo

katika kitu nimekuelewa vyema mku ni concept ya kuitendea haki "imani" kama ilivyo maana yake
 
Iko hivi ikiwa wewe una amini katika Mungu mmoja huyo wakwako yaani maanake hapo umechagua kuwa Monotheist, na kwakua umewakataa miungu mingine yote kama Zeus, Jupiter, Thor, El, Baàl, nk. Mpaka hapo wewe tayari ni Atheist wa Asilimia letsay 95.

Nini kinakutofautisha wewe na Atheists wenye asilimia 100?

Atheists
wa Asilimia 100 wao wamekataa Miungu yote uliyoikataa wewe, pamoja na huyo mmoja wako unayemuanini.

Dhana pekee ambazo zinazoweza kuwashawishi Atheists juu ya Uungu/UMungu ni kama zile za Deists, Pantheists, Agnostics.

Kuna wakati watu wanadhani Agnostics wapo ule upande wa Dini kama Ukristo, Uislamu, Uyahudi, nk.

Agnostics wote kwa Asilimia kubwa huwa ni maEX wa Dini fuata mkumbo i.e Ukristo, Uislamu, Uyahudi, nk. Wanashawishika zaidi na dhana ya Uungu/Mungu kutoka kwa Deists, na Pantheists.

Hitimisho

Wakristo hukataa madai ya Uislamu.
Waislamu hukataa madai ya Ukristo.
Wayahudi hukataa yote mawili.

Na kila kundi hukataa miungu ya kale au ya tamaduni nyingine.

Atheists wanakubaliana na kila dini katika kukataa miungu mingine — isipokuwa wanaenda hatua moja zaidi kwa kukataa hata huyo Mungu wa mwisho aliyebaki.

Kwa hiyo, tofauti kati ya muumini na atheist si katika kitendo cha kukataa miungu, bali katika idadi ya miungu iliyokataliwa.
Atheists si kwamba anakataa miungu au aina fulani ya Mungu tu bali anapinga dhana nzima ya Uungu na hiyo ndio sababu inayomfanya kukataa hiyo miungu yote au chochote kile kitakachoitwa mungu. Kwahiyo wapo tofauti sana na muumini.

Kwahiyo mkuu hao watu wawili tofauti zao ni kubwa na si ndogo. Muumini anaweza akawa anaamini huyo Mungu mmoja kwa sababu kazaliwa na kukulia akimtambua huyo Mungu mmoja tu ila Atheist yeye kafuta kabisa dhana ya uungu hivyo hawezi kukuelewa ukizungumzia tu kinachoitwa Mungu/miungu.
 
mwanzo nilikuambia watu wa aina yenu ni ngumu kukabiliana nao kwa hoja.

wewe unapokwama ni kuchukulia hiyo mnaita atheism ni kama kundi lenye mawazo sawa , atheism kwa ninavyoelewa mimi wanaktana sehemu moja ambayo haina shaka , ni kwamba kaja huyu na imani/dini yake na anasema huu ndo ukweli - wao wakiangalia wakiona kuna vitu havimake sense wanaona hapa kuna utapeli.

wawe na uhakika au wasiwe na uhakika wa kwamba hayupo - it doesn't matter as long as mtu akija na habari za imani yake ya kuanza kuwaeleza njoeni huku inabidi huyo mtu awe na hoja za kutosha na za kukidhi maswali yao (maswali yawe yana makesense au lah - ila wanatakiwa wajibiwe) unless useme tu ni just gambling kwamba aisee ujumbe umeshausikia ukikaidi unaenda kula kiberiti.

anayetakiwa kutoa uthibitisho pasinashaka yule anayesema kitu hiki kipo hivi na vile

mkuu kama wewe unafikra huru kama usemavyo fatilia kisa cha huyu jamaa Daniel everett

alienda maporini huko amazon, kueneza dini kwa makabila ya misituni, lakini akaondoka kaacha dini na akabobea kama msomi wa mambo ya lugha kapambana hadi na theory za kina choamsky kwenye mambo hayo ya lugha baada ya kugundua kitu kwenye lugha ya hilo kabila la piraha

sasa kama wewe ni fikra huru youtube kuna kama vimakaa fulani anaelezea ilikuaje lile kabila badala ya yeye kuwapa dini likamfanya yeye aache dini hadi kupeana talaka na mkewe maana wote walikua watu wa kueneza dini --- kisa cha huyo jamaa tusikichukue kama ndo authority ya kupinga dini , ila kama wewe unasema huwaelewi atheist na unafikra huru naamini utapata mwanga wa kuelewa their perspective --- alafu sasa wewe kama muumini utajipima kama unaweza wapa muongozo au lah katika framework ya imani iliyopo

katika kitu nimekuelewa vyema mku ni concept ya kuitendea haki "imani" kama ilivyo maana yake
Mkuu nimekuelewa nitafuatili huo mkasa wa huyo jamaa.

Tukirudi hapo kwenye watu wasioamini Mungu nakubali kabisa kuwa wanatofautiana, wapo ambao wamekosa imani(lack of belief) inawezakuwa hawajafikiwa kabisa habari za kuhusu Mungu, na kuna ambao wanapinga dhana nzima ya uwepo wa Mungu kwa maana hawa wengi wao waliwahi kuwa waumini wa Mungu na dini ila wakaacha kuamini na wamekuwa wapingaji/wakanushaji.

Sasa kwa mtazamo wangu sidhani kama hao wanaweza kukutana sehemu moja kama ulivyoeleza, mtu ambaye aliwahi kuwa muumini wa dini maandiko kayasoma na alikuwa anakubali uwepo wa Mungu halafu akaamua kukana yote hayo huyu mtu hata kujadiliana nae ni tofauti na yule wa aina ya kwanza.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Allah, alikuwa wapi kabla ya uislamu kuenea na kwanini Kila waislamu walipofanya maovu ya kupindikia katika vita karne ya saba walisema "Allah Akbar"?.
Kwanini Allah aliruhusu Muhamad amuingilie mtoto wa miaka 9, na wakati huo leo hii ionekane ni kinyume na maadili kumuingilia kimwili mtoto wa miaka 9?
Ilikuwaje Allah akamuumba Nguruwe halafu akaruhusu atumike kama kitoweo, halafu baadae akawakataza watu wasitumie kama kitoweo?

A philosophical paradox on moral relativism only establish the basis for improving our understanding of morality out of dogmatic stance of Islam, Christianity, and judaism.

Reported Executions in Early Islamic Biography — Is This a Moral God (All done under the order of the bloodmonger called Muhammad)​

  1. Banu Qurayza (627 CE) – After the Battle of the Trench, adult males of the tribe were executed following a judgment Muhammad affirmed as consistent with God’s decree (reported in early sources such as Sirat Rasul Allah).
  2. Abdullah ibn Khatal – Ordered executed during the Conquest of Mecca for murder and apostasy.
  3. Ka'b ibn al-Ashraf – Assassinated after being accused of inciting war against the Muslim community.
  4. Uqba ibn Abi Mu'ayt – Executed after the Battle of Badr due to prior persecution and continued hostility.
  5. Abdullah ibn Sa'd ibn Abi Sarh – Reportedly marked for execution for apostasy at the Conquest of Mecca (later pardoned after intercession).

These reports, preserved in early Islamic historiography, are traditionally framed as acts of wartime justice or enforcement of divine law. Critics, however, raise the ethical question: if these actions were divinely sanctioned, does this reflect a moral God? The answer depends entirely on one’s moral framework—whether morality is understood as divine command, historical-contextual justice, or universal human rights independent of revelation.

Kwanza, Allah hakuanza kuwepo karne ya saba. Jina “Allah” lilitumika na Waarabu hata kabla ya Uislamu, na hadi leo Wakristo Waarabu wanatumia neno hilo hilo kwa Mungu. Uislamu haukudai kuanzisha Mungu mpya bali kurejesha imani ya Ibrahim (Abraham).

Pili, hoja ya “vita vya karne ya saba” iwekwe kwenye muktadha wa kihistoria. Dunia nzima ya kale ilikuwa ya vita vya kikabila na kifalme. Ukisoma Biblia, Mungu wa Biblia anaamuru mauaji ya makabila mazima (1 Samweli 15), kuteketezwa kwa miji, na hata watoto. Kanisa chini ya Kanisa Katoliki liliendesha Vita vya Msalaba na Mahakama ya Inquisition zikaua maelfu kwa jina la Mungu. Je, hapo pia si “Mungu wa maadili”?

Tatu, kuhusu ndoa ya Muhammad na Aisha — maadili ya ndoa za kale yalitofautiana na leo. Hata katika Biblia, wasichana wadogo walipewa ndoa mapema (mfano Rebeka kwa Isaka). Hakuna ustaarabu wa kale uliokuwa na kipimo cha “umri wa miaka 18” kama cha leo. Kutumia vigezo vya karne ya 21 kuhukumu karne ya 7 ni upendeleo wa kihistoria (anachronism).

Nne, kuhusu adhabu na mauaji yaliyotajwa (kama Banu Qurayza), hata katika Biblia kuna visa vya adhabu kali kwa usaliti wa kivita. Swali la “Je, Mungu ni wa maadili?” hutegemea kama unaamini maadili yanatoka kwa Mungu au kwa binadamu. Kama ni kwa Mungu, basi Biblia ina visa vigumu. Kama ni kwa binadamu, basi dini zote zinapaswa kupimwa kwa mizani hiyo hiyo — si Uislamu pekee.

Mwisho: ukikataa Uislamu kwa sababu ya vita vya kale, basi kwa uaminifu huo huo ukatae pia Ukristo na Uyahudi kwa historia yao ya damu. Huwezi kutumia Biblia kushambulia Qurani wakati Biblia yenyewe ina historia ya vita, utumwa, na hukumu za kifo kwa amri ya Mungu.

Hiyo ndiyo hoja ya msingi , ama ukubali muktadha wa kihistoria kwa wote, au uwahukumu wote kwa kipimo kimoja.
Kama dini ni mbaya kwa sababu ya historia ya vita , basi Ukristo na Uyahudi zina historia hiyo pia.
Kama Mungu wa Biblia ni wa maadili lakini wa Qurani si wa maadili basi soma Biblia vizuri.
Kama maadili ni ya kisekula basi maadili hayo yamebadilika mara nyingi (utumwa ulikuwa halali kisheria Ulaya hadi karne ya 19).

Historia ya mwanadamu imejaa damu — iwe chini ya msalaba, chini ya nusu mwezi, au chini ya itikadi zisizo na Mungu. Tatizo si jina la Mungu, bali ni mwanadamu.
 
Atheists si kwamba anakataa miungu au aina fulani ya Mungu tu bali anapinga dhana nzima ya Uungu na hiyo ndio sababu inayomfanya kukataa hiyo miungu yote au chochote kile kitakachoitwa mungu. Kwahiyo wapo tofauti sana na muumini.

Kwahiyo mkuu hao watu wawili tofauti zao ni kubwa na si ndogo. Muumini anaweza akawa anaamini huyo Mungu mmoja kwa sababu kazaliwa na kukulia akimtambua huyo Mungu mmoja tu ila Atheist yeye kafuta kabisa dhana ya uungu hivyo hawezi kukuelewa ukizungumzia tu kinachoitwa Mungu/miungu.
Labda hao unaowasungumzia wewe ni indoctrinated atheist, dogmatic atheists, etc. lakini Informed Atheists are open-minded on the intellectual understanding of the concept of God from Agostocism philosophy, Deism Philosophy, Pantheism Philosophy, Cultural Christianity, Liberal Christianity, Jewish Humanism, Liberal Islam, Cultural Islam, etc.
 
Kwanza, Allah hakuanza kuwepo karne ya saba. Jina “Allah” lilitumika na Waarabu hata kabla ya Uislamu, na hadi leo Wakristo Waarabu wanatumia neno hilo hilo kwa Mungu. Uislamu haukudai kuanzisha Mungu mpya bali kurejesha imani ya Ibrahim (Abraham).

Pili, hoja ya “vita vya karne ya saba” iwekwe kwenye muktadha wa kihistoria. Dunia nzima ya kale ilikuwa ya vita vya kikabila na kifalme. Ukisoma Biblia, Mungu wa Biblia anaamuru mauaji ya makabila mazima (1 Samweli 15), kuteketezwa kwa miji, na hata watoto. Kanisa chini ya Kanisa Katoliki liliendesha Vita vya Msalaba na Mahakama ya Inquisition zikaua maelfu kwa jina la Mungu. Je, hapo pia si “Mungu wa maadili”?

Tatu, kuhusu ndoa ya Muhammad na Aisha — maadili ya ndoa za kale yalitofautiana na leo. Hata katika Biblia, wasichana wadogo walipewa ndoa mapema (mfano Rebeka kwa Isaka). Hakuna ustaarabu wa kale uliokuwa na kipimo cha “umri wa miaka 18” kama cha leo. Kutumia vigezo vya karne ya 21 kuhukumu karne ya 7 ni upendeleo wa kihistoria (anachronism).

Nne, kuhusu adhabu na mauaji yaliyotajwa (kama Banu Qurayza), hata katika Biblia kuna visa vya adhabu kali kwa usaliti wa kivita. Swali la “Je, Mungu ni wa maadili?” hutegemea kama unaamini maadili yanatoka kwa Mungu au kwa binadamu. Kama ni kwa Mungu, basi Biblia ina visa vigumu. Kama ni kwa binadamu, basi dini zote zinapaswa kupimwa kwa mizani hiyo hiyo — si Uislamu pekee.

Mwisho: ukikataa Uislamu kwa sababu ya vita vya kale, basi kwa uaminifu huo huo ukatae pia Ukristo na Uyahudi kwa historia yao ya damu. Huwezi kutumia Biblia kushambulia Qurani wakati Biblia yenyewe ina historia ya vita, utumwa, na hukumu za kifo kwa amri ya Mungu.

Hiyo ndiyo hoja ya msingi , ama ukubali muktadha wa kihistoria kwa wote, au uwahukumu wote kwa kipimo kimoja.
Kama dini ni mbaya kwa sababu ya historia ya vita , basi Ukristo na Uyahudi zina historia hiyo pia.
Kama Mungu wa Biblia ni wa maadili lakini wa Qurani si wa maadili basi soma Biblia vizuri.
Kama maadili ni ya kisekula basi maadili hayo yamebadilika mara nyingi (utumwa ulikuwa halali kisheria Ulaya hadi karne ya 19).

Historia ya mwanadamu imejaa damu — iwe chini ya msalaba, chini ya nusu mwezi, au chini ya itikadi zisizo na Mungu. Tatizo si jina la Mungu, bali ni mwanadamu.
Ok, iko hivi Mkuu, mimi ni Secular Humanist. Sikubaliani na mafundisho ya kidogma ya Christianity, Islam, wala Judaism. Ninaamini kwa ushahidi wa muda mrefu kwamba Sayansi na Hoja zenye mantiki ndizo mkombozi wa kweli wa ubinadamu.

Kwanza, ni kweli vita na fujo vilikuwepo kabla ya ujio wa dini, lakini dini ziliendeleza na kuhalalisha utamaduni wa vita katika nyakati tofauti za historia. Ukiangalia mgogoro wa Israel na Palestina, swali la kujiuliza ni nini hasa chanzo chake kikuu; jibu liko wazi kwamba mgogoro huo umejikita sana katika mvutano wa kihistoria na kidini juu ya mji wa Jerusalem, ambao una uzito mkubwa katika imani za Uyahudi na Uislamu. Hapa tunaona namna imani za kidini zinavyochanganyika na siasa na kuendeleza migogoro isiyoisha.

Pili, ni kweli ndoa za utotoni zilikuwepo kabla ya ustaarabu wa kisasa, lakini ustaarabu tunaouzungumzia leo umejengwa juu ya misingi ya haki za binadamu, si juu ya maandiko ya kidini. Msingi wa “Human Rights Charter” unatokana na falsafa ya kisekula inayotanguliza utu na usawa wa binadamu bila kujali dini. Ukiangalia takwimu za nchi zinazoongoza kwa ndoa za utotoni kama Somalia, Sudan, Afghanistan, Iran na Iraq, nyingi ni jamii zenye wafuasi wengi wa Uislamu. Hoja yangu ni kwamba pale ambapo tafsiri za kidini zinapopewa uzito kuliko misingi ya haki za binadamu, ustaarabu wa kweli unacheleweshwa kwa sababu mila na mifumo ya kale huendelea kuhalalishwa kwa kigezo cha dini.

Tatu, tunaposema Sayansi ndiye mkombozi wa dunia hatusemi kwa hisia bali kwa ushahidi. Kupitia chanjo, Sayansi imepunguza au kuondoa magonjwa yaliyokuwa yanaua mamilioni ya watu ndani ya muda mfupi. Kupitia teknolojia ya mawasiliano, watu walioko mabara tofauti wanaweza kuwasiliana papo hapo; bila Sayansi hilo lisingewezekana. Katika usafiri, mababu zetu walitembea umbali mrefu kutafuta chakula au huduma, lakini leo unachagua namna ya kusafiri kulingana na uwezo na hitaji lako. Sayansi imeleta mapinduzi katika afya, mawasiliano, uchukuzi na sekta nyingi nyingine, na uzuri wake hauhitaji kuabudiwa; unaitumia, inanufaisha maisha yako, na matokeo yake yanaonekana kwa vitendo.

Nne, hoja kwamba atheists ni wabishi au hawana uelewa si ya kweli. Kwa kiwango kikubwa, atheists wengi wamejifunza dini, sayansi, falsafa, siasa na tamaduni kwa kina kabla ya kufikia msimamo wao. Tofauti kuu iko kwenye mzigo wa uthibitisho; anayedai ndiye anayepaswa kuthibitisha. Ukidai nyoka alizungumza, Yesu alitembea juu ya maji, au Muhammad alipaa kwenda mbinguni, unapaswa kuleta ushahidi. Kwa upande wetu, ushahidi ndio msingi wa kuamini; tunaamini dunia inazunguka jua kwa sababu kuna ushahidi wa kisayansi, tunaamini dunia ina umbo la duara kwa sababu kuna ushahidi, tunaelewa mvua inavyonyesha na tetemeko la ardhi linavyotokea kwa sababu Sayansi imeeleza na kuthibitisha mifumo hiyo kwa majaribio na uchunguzi.

Mwisho, jambo la msingi zaidi kama binadamu ni kuhakikisha tunakuwa chanzo cha furaha na si mateso kwa wengine bila sababu ya msingi. Imani ni haki ya mtu binafsi, lakini inapopelekwa hadharani na kuanza kudai mamlaka juu ya maisha ya wengine bila ushahidi, huzalisha migogoro na mvutano. Wakati huo, kuulizwa maswali si chuki bali ni sehemu ya uwajibikaji wa hoja; na kama madai hayawezi kuthibitishwa, jamii ina haki ya kuyapima kwa mizani ya mantiki na ushahidi.

Kama tatizo ni mwanadamu, nani alimuumba Mwanadamu, Je si yeye mnayedai yakuwa ni mjuzi wa yajayo yani mjuzi wa vyote?
 
Labda hao unaowasungumzia wewe ni indoctrinated atheist, dogmatic atheists, etc. lakini Informed Atheists are open-minded on the intellectual understanding of the concept of God from Agostocism philosophy, Deism Philosophy, Pantheism Philosophy, Cultural Christianity, Liberal Christianity, Jewish Humanism, Liberal Islam, Cultural Islam, etc.
Sizungumzii hao indoctrinated atheist bali hao wengine, sijajua wewe ukiangalia hoja za atheists unaona nini ila kwa upande wangu mbona ipo wazi kabisa katika hoja zao katika kukana dhana nzima ya Uungu.
 
Kwani mkuu unaposema, Mungu unamaanisha nini?
 
hahaa nikikuuliza ulipataje majibu utasema ulipata ndoto/maono/ufunuo

Jiulize kwanini matatizo hayaishi maishani mwako...

Twende kwenye mada ya uzi, watu wengi sana wacha Mungu wanakufa bila kujibiwa maombi yao.

Visingizio ni vingi mara Mungu hakupi unachotaka bali unachostahili, mara mipango yake haichunguziki, sasa kwanini aliwaambia muombe naye atawapa?

Ukifikiria unaona haya mambo ni uongo tu.
Tulia wewe
 
Haya basi toa wewe jibu tuone katika hilo uliloniuliza kama sijajibu nazunguka zunguka.
Hatuwezi kujua kwamba hiki hakipo kwasababu ni kweli hakipo. Au kipo lakini umekosekana uthibitisho wa kuthibitisha kipo.

Ndio maana ukianza kudai kitu kipo, ina maana unajua kweli kipo, na unaweza ku prove kweli kipo. Unatakiwa kuthibitisha kweli kipo.

Sasa ukishindwa ku prove hicho unachodai kweli kipo, unabaki kusema kipo kwa vile hakuna uthibitisho wa kutokuwepo kwake. Hapo unakuwa umehamisha madai yako kwa mtu mwingine. Ume shift, The burden of proof.

Unataka yule anayekataa ndio athibitishe, wakati uliyeanza kudai uwepo wa kitu hicho ni wewe. Na umeshindwa kuthibitisha.

Anything asserted without evidence can be dismissed without evidence.

Chochote kinachodaiwa bila ushahidi kinaweza kutupiliwa mbali bila ushahidi.

Kwa sababu hatuwezi kujua kitu hakipo kwa sababu ni kweli hakipo, Au kipo lakini umekosekana tu uthibitisho wa ku prove kipo.

Kwa hiyo wewe unayeanza kusema kitu kipo ndio utoe uthibitisho wa kitu hicho.

Ukishindwa kutoa uthibitisho wa kitu hicho unachodai kwamba kipo, ina maana unachokidai kipo, hakipo.

Ndio maana umeshindwa kuthibitisha kipo.
 
Mkuu nimekuelewa nitafuatili huo mkasa wa huyo jamaa.

Tukirudi hapo kwenye watu wasioamini Mungu nakubali kabisa kuwa wanatofautiana, wapo ambao wamekosa imani(lack of belief) inawezakuwa hawajafikiwa kabisa habari za kuhusu Mungu, na kuna ambao wanapinga dhana nzima ya uwepo wa Mungu kwa maana hawa wengi wao waliwahi kuwa waumini wa Mungu na dini ila wakaacha kuamini na wamekuwa wapingaji/wakanushaji.

Sasa kwa mtazamo wangu sidhani kama hao wanaweza kukutana sehemu moja kama ulivyoeleza, mtu ambaye aliwahi kuwa muumini wa dini maandiko kayasoma na alikuwa anakubali uwepo wa Mungu halafu akaamua kukana yote hayo huyu mtu hata kujadiliana nae ni tofauti na yule wa aina ya kwanza.
Sawa mkuu,
mimi katika kitu naunga mkono bila kupepesa macho ni kwamba vile vitabu vya imani 2 za kutoka middle east vina matatizo
 
Ok, iko hivi Mkuu, mimi ni Secular Humanist. Sikubaliani na mafundisho ya kidogma ya Christianity, Islam, wala Judaism. Ninaamini kwa ushahidi wa muda mrefu kwamba Sayansi na Hoja zenye mantiki ndizo mkombozi wa kweli wa ubinadamu.

Kwanza, ni kweli vita na fujo vilikuwepo kabla ya ujio wa dini, lakini dini ziliendeleza na kuhalalisha utamaduni wa vita katika nyakati tofauti za historia. Ukiangalia mgogoro wa Israel na Palestina, swali la kujiuliza ni nini hasa chanzo chake kikuu; jibu liko wazi kwamba mgogoro huo umejikita sana katika mvutano wa kihistoria na kidini juu ya mji wa Jerusalem, ambao una uzito mkubwa katika imani za Uyahudi na Uislamu. Hapa tunaona namna imani za kidini zinavyochanganyika na siasa na kuendeleza migogoro isiyoisha.

Pili, ni kweli ndoa za utotoni zilikuwepo kabla ya ustaarabu wa kisasa, lakini ustaarabu tunaouzungumzia leo umejengwa juu ya misingi ya haki za binadamu, si juu ya maandiko ya kidini. Msingi wa “Human Rights Charter” unatokana na falsafa ya kisekula inayotanguliza utu na usawa wa binadamu bila kujali dini. Ukiangalia takwimu za nchi zinazoongoza kwa ndoa za utotoni kama Somalia, Sudan, Afghanistan, Iran na Iraq, nyingi ni jamii zenye wafuasi wengi wa Uislamu. Hoja yangu ni kwamba pale ambapo tafsiri za kidini zinapopewa uzito kuliko misingi ya haki za binadamu, ustaarabu wa kweli unacheleweshwa kwa sababu mila na mifumo ya kale huendelea kuhalalishwa kwa kigezo cha dini.

Tatu, tunaposema Sayansi ndiye mkombozi wa dunia hatusemi kwa hisia bali kwa ushahidi. Kupitia chanjo, Sayansi imepunguza au kuondoa magonjwa yaliyokuwa yanaua mamilioni ya watu ndani ya muda mfupi. Kupitia teknolojia ya mawasiliano, watu walioko mabara tofauti wanaweza kuwasiliana papo hapo; bila Sayansi hilo lisingewezekana. Katika usafiri, mababu zetu walitembea umbali mrefu kutafuta chakula au huduma, lakini leo unachagua namna ya kusafiri kulingana na uwezo na hitaji lako. Sayansi imeleta mapinduzi katika afya, mawasiliano, uchukuzi na sekta nyingi nyingine, na uzuri wake hauhitaji kuabudiwa; unaitumia, inanufaisha maisha yako, na matokeo yake yanaonekana kwa vitendo.

Nne, hoja kwamba atheists ni wabishi au hawana uelewa si ya kweli. Kwa kiwango kikubwa, atheists wengi wamejifunza dini, sayansi, falsafa, siasa na tamaduni kwa kina kabla ya kufikia msimamo wao. Tofauti kuu iko kwenye mzigo wa uthibitisho; anayedai ndiye anayepaswa kuthibitisha. Ukidai nyoka alizungumza, Yesu alitembea juu ya maji, au Muhammad alipaa kwenda mbinguni, unapaswa kuleta ushahidi. Kwa upande wetu, ushahidi ndio msingi wa kuamini; tunaamini dunia inazunguka jua kwa sababu kuna ushahidi wa kisayansi, tunaamini dunia ina umbo la duara kwa sababu kuna ushahidi, tunaelewa mvua inavyonyesha na tetemeko la ardhi linavyotokea kwa sababu Sayansi imeeleza na kuthibitisha mifumo hiyo kwa majaribio na uchunguzi.

Mwisho, jambo la msingi zaidi kama binadamu ni kuhakikisha tunakuwa chanzo cha furaha na si mateso kwa wengine bila sababu ya msingi. Imani ni haki ya mtu binafsi, lakini inapopelekwa hadharani na kuanza kudai mamlaka juu ya maisha ya wengine bila ushahidi, huzalisha migogoro na mvutano. Wakati huo, kuulizwa maswali si chuki bali ni sehemu ya uwajibikaji wa hoja; na kama madai hayawezi kuthibitishwa, jamii ina haki ya kuyapima kwa mizani ya mantiki na ushahidi.

Kama tatizo ni mwanadamu, nani alimuumba Mwanadamu, Je si yeye mnayedai yakuwa ni mjuzi wa yajayo yani mjuzi wa vyote?

Sayansi si mbadala wa Mungu.
Inaeleza jinsi vitu vinavyotokea, si kwa nini vipo. Big Bang inaonyesha ulimwengu una mwanzo — kila kilicho na mwanzo kina sababu.
Qur’an 52:35: “Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji??”

Maadili bila Mungu ni maoni tu.
Kama hakuna Muumba, “haki za binadamu” ni makubaliano ya kijamii yanayoweza kubadilika kesho.
Leo unasema ndoa ya utotoni ni mbaya kwa msingi gani wa lazima kama hakuna sheria juu ya mwanadamu?

Uovu si kosa la Mungu, ni hiari ya mwanadamu.

Qur’an 67:2 . Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.
Dini si matumizi mabaya ya dini.
Qur’an 2:256: “Hakuna kulazimisha katika dini.”

Sayansi ni chombo. Maadili yanahitaji msingi. Bila Muumba, kunakuwa na maoni tu na si wajibu wa lazima kwa wote.
 
Kwani mkuu unaposema, Mungu unamaanisha nini?
Mkuu maana ya neno Mungu ipo kwenye mitazamo tofauti na ndio maana mimi nasema atheists wanapinga dhana ya Uungu kwa maana hadi Pantheism, sababu japokuwa Patheism haiamini Mungu kama wanavyoamini dini za Uyahudi,ukristo na uislamu ila bado Patheism ni aina ya imani katika dhana ya Uungu.
 
Back
Top Bottom