God's time is a myth, The strategy of redundancy

Hatuwezi kujua kwamba hiki hakipo kwasababu ni kweli hakipo. Au kipo lakini umekosekana uthibitisho wa kuthibitisha kipo.

Ndio maana ukianza kudai kitu kipo, ina maana unajua kweli kipo, na unaweza ku prove kweli kipo. Unatakiwa kuthibitisha kweli kipo.

Sasa ukishindwa ku prove hicho unachodai kweli kipo, unabaki kusema kipo kwa vile hakuna uthibitisho wa kutokuwepo kwake. Hapo unakuwa umehamisha madai yako kwa mtu mwingine. Ume shift, The burden of proof.

Unataka yule anayekataa ndio athibitishe, wakati uliyeanza kudai uwepo wa kitu hicho ni wewe. Na umeshindwa kuthibitisha.

Anything asserted without evidence can be dismissed without evidence.

Chochote kinachodaiwa bila ushahidi kinaweza kutupiliwa mbali bila ushahidi.

Kwa sababu hatuwezi kujua kitu hakipo kwa sababu ni kweli hakipo, Au kipo lakini umekosekana tu uthibitisho wa ku prove kipo.

Kwa hiyo wewe unayeanza kusema kitu kipo ndio utoe uthibitisho wa kitu hicho.

Ukishindwa kutoa uthibitisho wa kitu hicho unachodai kwamba kipo, ina maana unachokidai kipo, hakipo.

Ndio maana umeshindwa kuthibitisha kipo.
Kipi kinakupa uhakika 100% kwamba mtu akishindwa kuthibitisha uwepo wa kitu alichodai kipo basi hicho kitu hakipo kweli na si vinginevyo?
 
Sawa mkuu,
mimi katika kitu naunga mkono bila kupepesa macho ni kwamba vile vitabu vya imani 2 za kutoka middle east vina matatizo
Kuona hivyo vitabu vina shida ni jambo moja na kuwa atheist kisa kuna shida kwenye hivyo vitabu ni jambo jengine kwa sababu wapo watu wanakosoa baadhi ya mambo kwenye hivyo vitabu ila bado ni wanaamini klhivyo vitabu pamoja na Mungu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Kipi kinakupa uhakika 100% kwamba mtu akishindwa kuthibitisha uwepo wa kitu alichodai kipo basi hicho kitu hakipo kweli na si vinginevyo?
Utasemaje kitu kipo halafu ushindwe kuthibitisha?
 
Kuona hivyo vitabu vina shida ni jambo moja na kuwa atheist kisa kuna shida kwenye hivyo vitabu ni jambo jengine kwa sababu wapo watu wanakosoa baadhi ya mambo kwenye hivyo vitabu ila bado ni wanaamini klhivyo vitabu pamoja na Mungu.
unaamini vitabu vile vimetoka kwa mungu ?
 
Sayansi si mbadala wa Mungu.
Inaeleza jinsi vitu vinavyotokea, si kwa nini vipo. Big Bang inaonyesha ulimwengu una mwanzo — kila kilicho na mwanzo kina sababu.
Qur’an 52:35: “Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji??”

Maadili bila Mungu ni maoni tu.
Kama hakuna Muumba, “haki za binadamu” ni makubaliano ya kijamii yanayoweza kubadilika kesho.
Leo unasema ndoa ya utotoni ni mbaya kwa msingi gani wa lazima kama hakuna sheria juu ya mwanadamu?

Uovu si kosa la Mungu, ni hiari ya mwanadamu.

Qur’an 67:2 . Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.
Dini si matumizi mabaya ya dini.
Qur’an 2:256: “Hakuna kulazimisha katika dini.”

Sayansi ni chombo. Maadili yanahitaji msingi. Bila Muumba, kunakuwa na maoni tu na si wajibu wa lazima kwa wote.
Ndio ni kweli Sayansi sio mbadala wa Mungu ambaye hayupo, labda kama angekuwepo.

Thibitisha kwamba Allah alikuwepo wakati wa Bing Bang.

Ni kweli pia kwamba Maadili ya Kihumanisti hubadilika. Ila unachopaswa kujua ni kwamba maadili ya Kihumanisti ni kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya Amani, Furaha, na Upendo kwa ajili ya Viumbe hai kuishi, na pale mabadiliko yanapotokea huwa ni kwa ajili kufanya maboresho kwenye sheria na misingi ili kuongeza furaha, amani, na upendo kati ya viumbe hai.

Humanistic morality changes for the better not for the worst.

Look at what Is in the Quran of the so called the Holy God (Allah)
  1. Surah Al-Baqarah (2:191) states, “Kill them wherever you overtake them and expel them from wherever they expelled you,” referring to confrontation with opposing forces during conflict.
  2. Surah Al-Baqarah (2:193) states, “Fight them until there is no persecution and religion is for Allah,” emphasizing continuation of fighting until persecution ceases.
  3. Surah An-Nisa (4:74) encourages believers to fight in the cause of Allah, promising spiritual reward for those who participate in such fighting.
  4. Surah An-Nisa (4:89) states, “If they turn away, then seize them and kill them wherever you find them,” referring to hostile defectors in a conflict setting.
  5. Surah Al-Ma’idah (5:33) prescribes execution or crucifixion for those who wage war against Allah and spread violent disorder in the land.
  6. Surah Al-Anfal (8:12) contains the phrase, “Strike above the necks and strike from them every fingertip,” which appears in the context of battle.
  7. Surah Al-Anfal (8:39) instructs believers to “Fight them until there is no more persecution and religion is entirely for Allah.”
  8. Surah At-Tawbah (9:5) states, “Kill the polytheists wherever you find them,” referring to certain groups during a specific conflict period.
  9. Surah At-Tawbah (9:29) commands fighting against certain non-believing groups until they submit to political authority and pay tribute.
  10. Surah Muhammad (47:4) states, “When you meet those who disbelieve in battle, strike their necks,” explicitly referring to combat situations.

It is lucky that i wasn't born in an Islam country, because the penalty for apostate is death. And you calling it a religion of peace and morality.

Islam is a threat to humanity, and should be condemned publicly.
 
Unajifanya ni Humanist na kisogoni umejaa ugalatia huku ukiwashutumu wenzako na utumiaji wa AI kumbe wewe ndiye professor wa AI 😛 😛 😛

Tuje kwenye hoja zako

Thibitisha kwamba Allah alikuwepo wakati wa Big Bang”​

Kwanza, kosa lako ni la kimantiki: Big Bang ni mwanzo wa nafasi, muda na maada. Kitu kinachoanza hakiwezi kujiumba chenyewe.
Qur'an inasema:“Je! Hawakuona wale waliokufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa kitu kimoja kisha Tukazipasua…” (21:30)
Hichi si kitabu cha fizikia, lakini kinaelekeza kuwa ulimwengu ulikuwa hali moja kisha ukatenganishwa , dhana inayofanana na nadharia ya Big Bang.
Lakini hoja kuu ya Kiislamu si aya hiyo. Hoja kuu ni ya kiakili:
Kila kinachoanza kuwa na kuwepo kina sababu., Ulimwengu ulianza kuwepo.na Kwa hiyo una sababu.
Sababu hiyo haiwezi kuwa:
ya kimaada (kwa sababu maada ilianza wakati huo), au ya muda (kwa sababu muda ulianza wakati huo).
Hivyo lazima iwe nje ya muda, nje ya maada, yenye uwezo na hiari , hicho ndicho tunachokiita Allah.
Ukisema “Thibitisha Allah alikuwepo wakati wa Big Bang,” tayari unafanya kosa: Allah katika Uislamu hayuko ndani ya muda mpaka aseme “wakati wa”. Yeye ndiye Muumba wa muda.

Kuhusu “Humanistic morality changes for the better”Unasema maadili ya kibinadamu hubadilika kwa ubora tu. Historia inakupinga.​

Utumwa ulihalalishwa kwa misingi ya “maendeleo ya kiuchumi.”, Ukoloni ulihalalishwa kwa jina la “ustaarabu.”, Mauaji ya halaiki yalifanywa kwa jina la “ustawi wa taifa.”, Wote walidhani wanaboresha dunia.
Maadili yakitegemea hisia na makubaliano ya watu: Leo kitu ni sawa na Kesho si sawa. na Kesho kutwa kinarudi kuwa sawa.
Uislamu unasema maadili yanatoka kwa Muumba, si kura ya watu.

Aya za vita ulizotaja — umezikata nje ya muktadha
Karibu aya zote ulizoorodhesha zinahusu hali ya vita halisi, si amri ya kuua kila asiye Muislamu.

Mfano: 2:191
Aya hiyo iko katikati ya maelezo ya vita dhidi ya wale waliowafukuza Waislamu Makkah. Na hapo hapo Qur’an inasema: “Lakini wakiacha, basi hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe.” (2:192)

5:33 Aya hii inahusu wahalifu wanaofanya ugaidi na mauaji ya kijamii (hirabah) — si watu wa dini tofauti.​

9:5 Hii inahusu makundi maalum ya washirikina waliovunja mikataba na kuanzisha vita. Si amri ya jumla kwa dunia yote. Ndiyo maana aya 9:6 inasema: “Na akikuomba hifadhi mmoja wa washirikina, mpe hifadhi…”​

Huwezi kunukuu amri ya vita bila kusoma kabla na baada yake.

“Adhabu ya kuacha Uislamu ni kifo”​

Hili ni mjadala wa kifiqhi (kisheria) unaohusiana na uhaini wa kisiasa katika dola ya zamani, si suala la mtu kubadili imani kimya kimya.
Na Qur’an yenyewe inasema wazi:
“Hakuna kulazimishwa katika dini.” (2:256) .Kama Uislamu ungekuwa unalazimisha kwa upanga, aya hii isingekuwepo.

“Islam is a threat to humanity”​

Hii si hoja. Hii ni kauli ya hasira. Uislamu umeishi kwa karne 1400+ Una wafuasi zaidi ya bilioni 1.8 .Umejenga ustaarabu wa elimu, tiba, hesabu, na falsafa.
Kama ungekuwa “tishio kwa ubinadamu,” dunia isingekuwa na karne za ustaarabu wa Kiislamu katika Baghdad, Cordoba na kwingineko.

Hoja yako ina tatizo moja kubwa​

Unachukua: Maovu ya baadhi ya Waislamu , unauhukumu Uislamu.
Aya za vita , unazitoa nje ya historia.
Mfumo wa maadili ya kibinadamu , unadhani ni kipimo cha mwisho cha ukweli.
Lakini hujaonyesha kosa la kimantiki ndani ya dhana ya Mungu mwenyewe.
Kukataa Mungu si ushahidi wa kutokuwepo kwake. Ni msimamo tu.
Kijana uelewe , Ukosoaji wa kweli unahitaji: , Kusoma muktadha mzima, si kunukuu vipande. , Kutofautisha kati ya maandiko na matendo ya watu.
Hoja za mantiki, si hasira.
Kama unataka mjadala wa kielimu, hoja kwa hoja, Uislamu uko tayari. Lakini kama ni kelele za chuki, hiyo si falsafa hiyo ni hisia. Na hisia si kipimo cha ukweli.
 
Utasemaje kitu kipo halafu ushindwe kuthibitisha?
Kwanza unapaswa ufahamu kwamba kuna aina tofauti za uthibitisho na zote zina misingi yake na ukomo wake. Mfano uthibitisho wa kisayansi, kihistoria, kisheria, kiimani n.k

Mfano watu wanaposema hakuna uthibitisho wa uchawi hasa hukusudia uthibitisho wa kisayansi, naweza nikawa nimeona mambo mengi tu ya uchawi ila nikashindwa kuthibitisha kisayansi uwepo wa uchawi kutokana kutokana na uthibitisho wa kisayansi una misingi yake.
 
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Uthibitisho sio suala la imani. Bali uthibitisho ni suala la uhakika.

Hakuna uthibitisho wa kiimani.

Kwa sababu hata uongo unaweza kuaminiwa kwa kutumia imani.

Hivyo imani sio uthibitisho.
 
Unajifanya ni Humanist na kisogoni umejaa ugalatia huku ukiwashutumu wenzako na utumiaji wa AI kumbe wewe ndiye professor wa AI 😛 😛 😛

Tuje kwenye hoja zako

Thibitisha kwamba Allah alikuwepo wakati wa Big Bang”​

Kwanza, kosa lako ni la kimantiki: Big Bang ni mwanzo wa nafasi, muda na maada. Kitu kinachoanza hakiwezi kujiumba chenyewe.
Qur'an inasema:“Je! Hawakuona wale waliokufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa kitu kimoja kisha Tukazipasua…” (21:30)
Hichi si kitabu cha fizikia, lakini kinaelekeza kuwa ulimwengu ulikuwa hali moja kisha ukatenganishwa , dhana inayofanana na nadharia ya Big Bang.
Lakini hoja kuu ya Kiislamu si aya hiyo. Hoja kuu ni ya kiakili:
Kila kinachoanza kuwa na kuwepo kina sababu., Ulimwengu ulianza kuwepo.na Kwa hiyo una sababu.
Sababu hiyo haiwezi kuwa:
ya kimaada (kwa sababu maada ilianza wakati huo), au ya muda (kwa sababu muda ulianza wakati huo).
Hivyo lazima iwe nje ya muda, nje ya maada, yenye uwezo na hiari , hicho ndicho tunachokiita Allah.
Ukisema “Thibitisha Allah alikuwepo wakati wa Big Bang,” tayari unafanya kosa: Allah katika Uislamu hayuko ndani ya muda mpaka aseme “wakati wa”. Yeye ndiye Muumba wa muda.

Kuhusu “Humanistic morality changes for the better”Unasema maadili ya kibinadamu hubadilika kwa ubora tu. Historia inakupinga.​

Utumwa ulihalalishwa kwa misingi ya “maendeleo ya kiuchumi.”, Ukoloni ulihalalishwa kwa jina la “ustaarabu.”, Mauaji ya halaiki yalifanywa kwa jina la “ustawi wa taifa.”, Wote walidhani wanaboresha dunia.
Maadili yakitegemea hisia na makubaliano ya watu: Leo kitu ni sawa na Kesho si sawa. na Kesho kutwa kinarudi kuwa sawa.
Uislamu unasema maadili yanatoka kwa Muumba, si kura ya watu.

Aya za vita ulizotaja — umezikata nje ya muktadha
Karibu aya zote ulizoorodhesha zinahusu hali ya vita halisi, si amri ya kuua kila asiye Muislamu.

Mfano: 2:191
Aya hiyo iko katikati ya maelezo ya vita dhidi ya wale waliowafukuza Waislamu Makkah. Na hapo hapo Qur’an inasema: “Lakini wakiacha, basi hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe.” (2:192)

5:33 Aya hii inahusu wahalifu wanaofanya ugaidi na mauaji ya kijamii (hirabah) — si watu wa dini tofauti.​

9:5 Hii inahusu makundi maalum ya washirikina waliovunja mikataba na kuanzisha vita. Si amri ya jumla kwa dunia yote. Ndiyo maana aya 9:6 inasema: “Na akikuomba hifadhi mmoja wa washirikina, mpe hifadhi…”​

Huwezi kunukuu amri ya vita bila kusoma kabla na baada yake.

“Adhabu ya kuacha Uislamu ni kifo”​

Hili ni mjadala wa kifiqhi (kisheria) unaohusiana na uhaini wa kisiasa katika dola ya zamani, si suala la mtu kubadili imani kimya kimya.
Na Qur’an yenyewe inasema wazi:
“Hakuna kulazimishwa katika dini.” (2:256) .Kama Uislamu ungekuwa unalazimisha kwa upanga, aya hii isingekuwepo.

“Islam is a threat to humanity”​

Hii si hoja. Hii ni kauli ya hasira. Uislamu umeishi kwa karne 1400+ Una wafuasi zaidi ya bilioni 1.8 .Umejenga ustaarabu wa elimu, tiba, hesabu, na falsafa.
Kama ungekuwa “tishio kwa ubinadamu,” dunia isingekuwa na karne za ustaarabu wa Kiislamu katika Baghdad, Cordoba na kwingineko.

Hoja yako ina tatizo moja kubwa​

Unachukua: Maovu ya baadhi ya Waislamu , unauhukumu Uislamu.
Aya za vita , unazitoa nje ya historia.
Mfumo wa maadili ya kibinadamu , unadhani ni kipimo cha mwisho cha ukweli.
Lakini hujaonyesha kosa la kimantiki ndani ya dhana ya Mungu mwenyewe.
Kukataa Mungu si ushahidi wa kutokuwepo kwake. Ni msimamo tu.
Kijana uelewe , Ukosoaji wa kweli unahitaji: , Kusoma muktadha mzima, si kunukuu vipande. , Kutofautisha kati ya maandiko na matendo ya watu.
Hoja za mantiki, si hasira.
Kama unataka mjadala wa kielimu, hoja kwa hoja, Uislamu uko tayari. Lakini kama ni kelele za chuki, hiyo si falsafa hiyo ni hisia. Na hisia si kipimo cha ukweli.
Jambo pekee mnaloweza kulizungumzia kwa Ufasha ni Stori za Kucheza PONO na Bikra 72 huko mnapopaita peponi.

Allah hayupo hizo ni stori za kusadikika Tu.

Uislamu hauna chochote çhenye uthibitisho juu ya Big Bang, Planetary Nebulae, Cosmic Microwave Radiation, hata hayo unayosema yameandikwa kwenye msaafu ni uthibitisho tosha juu ya namna gani: Islam is an Ignorant religion.

To say Heaven and Earth were óne is False, and Unscientific.

Kama Allah ndiye mwanzilishi wa muda, na maada, Je nani ndiye mwanzilishi wa Allah?

Historia inakupinga wewe: Utumwa, na Ukoloni havipo leo kwenye dunia ya Kisasa ni kwasababu ya Secular Humanism ambayo ndiye mwanzilishi wa Sheria za Haki za Binadamu.
 
unaamini vitabu vile vimetoka kwa mungu ?
Ukiniuliza kuhusu hivyo vitabu kuwa kama vimetoka kwa Mungu sina jibu la moja kwa moja kujibia vitabu vyote, ila naweza kujibu kwamba ninaamini kuna maneno ya Mungu katika hivyo vitabu.
 
100% au lah?
 
Tunawatwisha mzigo mkubwa sana kuthibitisha kuwa Mungu mnayemuamini ni halisi na anaishi. Kwanini?

Kwanza,
Imani yenu haikutokana na uthibitisho, bali ilitokana na urithi wa kijamii. Hamkuamini kwa sababu mlipewa ushahidi wa kimajaribio au uthibitisho wa moja kwa moja, bali kwa sababu mlirithishwa imani hiyo kutoka kwa wazazi au jamii yenu. Hata wale waliowarithisha nao hawakuamini kwa sababu ya uthibitisho, bali walirithishwa pia. Hii inaleta swali la msingi la kifalsafa: ni kwa msingi gani muumini wa kwanza aliamini kile alichoamini? Na zaidi ya hapo, unawezaje kujua kwamba kile alichoamini kilikuwa kweli na kinawakilisha uhalisia wa nje ya akili yake?

Pili, ni kweli kwamba Atheists hawawezi kuthibitisha kutokuwepo kwa aina yoyote ya Miungu. Hata hivyo, msimamo wa Atheism haujengwi juu ya kuthibitisha kutokuwepo, bali juu ya kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha uwepo. Badala ya kudai kwa uhakika kwamba hakuna Miungu, Atheists huuliza maswali ya uchunguzi kama: kwanini watu huamini katika Miungu? Ni aina gani ya ushahidi inaweza kuthibitisha uwepo wa Mungu? Je, madai haya yanalingana na uhalisia unaoweza kuchunguzwa? Katika mchakato wa kutafuta majibu, hutegemea falsafa, saikolojia, anthropolojia, na tafiti za kisayansi zinazochunguza asili na maendeleo ya imani za kidini.

Tatu, kwanini watu huamini katika Miungu? Tafiti za anthropolojia na historia ya dini zinaonyesha mifumo inayojirudia katika jamii nyingi. Kwanza, imani katika Miungu ilitumika kama njia ya kuelewa matukio ya asili ambayo hayakuwa na maelezo ya kisayansi, kama mvua, radi, magonjwa, na vifo. Pili, imani za kidini zilitumika kama nyenzo ya kuhalalisha mamlaka ya kisiasa na kudumisha utawala. Tatu, dini zilitumika kama mfumo wa kusimamia maadili ya kijamii na kudhibiti tabia za wanajamii. Hivyo, imani hizi zilikuwa na kazi za kijamii na kisaikolojia, bila kujali kama zilikuwa kweli au la.

Nne, unawezaje kuthibitisha kuwa Miungu ni halisi? Ili kujibu swali hili, ni lazima kwanza uchunguze chanzo cha imani yenyewe. Tafiti zinaonyesha kwamba waumini wa kwanza hawakuamini kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kimajaribio, bali kwa sababu walikuwa wanatafuta maelezo ya matukio ambayo hawakuyafahamu. Kwa mfano, jamii za kale ziliamini kwamba kutoa kafara kunasababisha mvua kunyesha. Hawakuamini hivyo kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kisayansi wa uhusiano wa kisababishi, bali kwa sababu hawakuwa na elimu ya meteorolojia kueleza rain-cycle. Vivyo hivyo, hadithi za kidini kama simulizi la Adamu na Eva zilitoa maelezo ya chanzo cha binadamu kabla ya uwepo wa ushahidi wa kisayansi kama microscope, radiometric dating, na DNA researching. Hivyo, imani hizi zilijaza pengo la maarifa, si matokeo ya uthibitisho wa kimajaribio.

Historia pia inaonyesha mgongano kati ya imani na uchunguzi wa kisayansi. Mfano maarufu ni wa Galileo Galilei, ambaye alipingwa vikali baada ya kuunga mkono ushahidi kwamba Dunia inazunguka Jua. Upinzani huu haukutokana na ushahidi wa kupinga, bali ulitokana na kulinda mfumo wa imani ya kikristo uliokuwepo. Hii inaonyesha kwamba imani nyingi za kidini zilijengwa juu ya mapokeo na mamlaka, si juu ya uchunguzi wa kimajaribio.

Tano, Ipi ni nafasi ya sayansi katika misingi ya Imani zetu? Kwanza Sayansi inaweza kutusaidia kuchunguza na kuthibitisha imani zetu. Pili, Sayansi inaweza kutusaidia kuelewa uhalisia wa mazingira tunayoishi. Baada ya Sayansi kufanya mambo hayo mawili, hapo ndipo tutaweza kuelewa zaidi dhana ya Uungu/Mungu.

Hivyo, sayansi haitoi uthibitisho wa moja kwa moja wa uwepo wa Mungu, bali hutoa mbinu ya kuchuja madai na kutenganisha yale yenye ushahidi na yale yasiyo na ushahidi. Kupitia mchakato huu, tunaweza kuelewa vyema zaidi ni madai gani yanaendana na uhalisia na ni madai gani yanategemea imani pekee.

Mwisho, Elimu ni bure kabisa, Jielimisheni juu ya Imani zenu, Stop Being Ignorant Believers.

Mifano ya watafiti mashuhuri kwenye Dini na vitabu vyao ni kama ifuatavyo. Israel Finkelstein - The Bible Unearthed: Archaeology’s New Vision of Ancient Israel and the Origin of Its Sacred Texts. Bart D. Ehrman - Misquoting Jesus: The Story Behind Who Changed the Bible and Why. Pia W. Montgomery Watt Muhammad at Mecca. Rodinson, Maxime. Muhammad. New York Review Books Classics, 2021.
 
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Uthibitisho sio suala la imani. Bali uthibitisho ni suala la uhakika.

Hakuna uthibitisho wa kiimani.

Kwa sababu hata uongo unaweza kuaminiwa kwa kutumia imani.

Hivyo imani sio uthibitisho.
SIo kila uhakika ndio ukweli.

Nimeeleza kwamba kuna aina tofauti za uthibitisho kwa nyanja mbalimbali na kwamba kuna misingi na ukomo wake kwenye kila aina ya uthibitisho. Masuala ya kiimani yana misingi yake ya uthibitisho na ukomo wake ni kwa wale wenye kuamini tu imani husika.

Kwenye historia pia kuna uthibitisho wake una misingi yake, tunasoma historia za watu na matukio ambayo hata hatukuwa tumezaliwa ila tunakubali/kuamini pasina shaka kutokana kuna uthibitisho wa kihistoria. Hauwezi kutaka kuthibitisha ukweli wa hayo matukio hayo kwa uthibitisho wenye misingi ya kisayansi.
 
100% au lah?
Hapana sio maneno yote kwa 100% ni ya kutoka kwa Mungu kwenye hivyo vitabu.

Unajua mkuu shida kubwa ni utofauti wa uelewa wetu kwenye kujaribu kutafsiri maana ya hayo maandiko kwenye hivyo vitabu. Hivi unajua kwamba kuna baadhi ya waumini wa hivyo vitabu hawaamini uwepo wa uchawi na majini?
 
Uhakika ni nini?

Ukweli ni nini?

Imani ni nini?
 
Tunawatwisha mzigo mkubwa sana kuthibitisha kuwa Mungu mnayemuamini ni halisi na anaishi. Kwanini?

Kwanza,
Imani yenu haikutokana na uthibitisho, bali ilitokana na urithi wa kijamii. Hamkuamini kwa sababu mlipewa ushahidi wa kimajaribio au uthibitisho wa moja kwa moja, bali kwa sababu mlirithishwa imani hiyo kutoka kwa wazazi au jamii yenu. Hata wale waliowarithisha nao hawakuamini kwa sababu ya uthibitisho, bali walirithishwa pia. Hii inaleta swali la msingi la kifalsafa: ni kwa msingi gani muumini wa kwanza aliamini kile alichoamini? Na zaidi ya hapo, unawezaje kujua kwamba kile alichoamini kilikuwa kweli na kinawakilisha uhalisia wa nje ya akili yake?

Pili, ni kweli kwamba Atheists hawawezi kuthibitisha kutokuwepo kwa aina yoyote ya Miungu. Hata hivyo, msimamo wa Atheism haujengwi juu ya kuthibitisha kutokuwepo, bali juu ya kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha uwepo. Badala ya kudai kwa uhakika kwamba hakuna Miungu, Atheists huuliza maswali ya uchunguzi kama: kwanini watu huamini katika Miungu? Ni aina gani ya ushahidi inaweza kuthibitisha uwepo wa Mungu? Je, madai haya yanalingana na uhalisia unaoweza kuchunguzwa? Katika mchakato wa kutafuta majibu, hutegemea falsafa, saikolojia, anthropolojia, na tafiti za kisayansi zinazochunguza asili na maendeleo ya imani za kidini.

Tatu, kwanini watu huamini katika Miungu? Tafiti za anthropolojia na historia ya dini zinaonyesha mifumo inayojirudia katika jamii nyingi. Kwanza, imani katika Miungu ilitumika kama njia ya kuelewa matukio ya asili ambayo hayakuwa na maelezo ya kisayansi, kama mvua, radi, magonjwa, na vifo. Pili, imani za kidini zilitumika kama nyenzo ya kuhalalisha mamlaka ya kisiasa na kudumisha utawala. Tatu, dini zilitumika kama mfumo wa kusimamia maadili ya kijamii na kudhibiti tabia za wanajamii. Hivyo, imani hizi zilikuwa na kazi za kijamii na kisaikolojia, bila kujali kama zilikuwa kweli au la.

Nne, unawezaje kuthibitisha kuwa Miungu ni halisi? Ili kujibu swali hili, ni lazima kwanza uchunguze chanzo cha imani yenyewe. Tafiti zinaonyesha kwamba waumini wa kwanza hawakuamini kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kimajaribio, bali kwa sababu walikuwa wanatafuta maelezo ya matukio ambayo hawakuyafahamu. Kwa mfano, jamii za kale ziliamini kwamba kutoa kafara kunasababisha mvua kunyesha. Hawakuamini hivyo kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kisayansi wa uhusiano wa kisababishi, bali kwa sababu hawakuwa na elimu ya meteorolojia kueleza rain-cycle. Vivyo hivyo, hadithi za kidini kama simulizi la Adamu na Eva zilitoa maelezo ya chanzo cha binadamu kabla ya uwepo wa ushahidi wa kisayansi kama microscope, radiometric dating, na DNA researching. Hivyo, imani hizi zilijaza pengo la maarifa, si matokeo ya uthibitisho wa kimajaribio.

Historia pia inaonyesha mgongano kati ya imani na uchunguzi wa kisayansi. Mfano maarufu ni wa Galileo Galilei, ambaye alipingwa vikali baada ya kuunga mkono ushahidi kwamba Dunia inazunguka Jua. Upinzani huu haukutokana na ushahidi wa kupinga, bali ulitokana na kulinda mfumo wa imani ya kikristo uliokuwepo. Hii inaonyesha kwamba imani nyingi za kidini zilijengwa juu ya mapokeo na mamlaka, si juu ya uchunguzi wa kimajaribio.

Tano, Ipi ni nafasi ya sayansi katika misingi ya Imani zetu? Kwanza Sayansi inaweza kutusaidia kuchunguza na kuthibitisha imani zetu. Pili, Sayansi inaweza kutusaidia kuelewa uhalisia wa mazingira tunayoishi. Baada ya Sayansi kufanya mambo hayo mawili, hapo ndipo tutaweza kuelewa zaidi dhana ya Uungu/Mungu.

Hivyo, sayansi haitoi uthibitisho wa moja kwa moja wa uwepo wa Mungu, bali hutoa mbinu ya kuchuja madai na kutenganisha yale yenye ushahidi na yale yasiyo na ushahidi. Kupitia mchakato huu, tunaweza kuelewa vyema zaidi ni madai gani yanaendana na uhalisia na ni madai gani yanategemea imani pekee.

Mwisho, Elimu ni bure kabisa, Jielimisheni juu ya Imani zenu, Stop Being Ignorant Believers.

Mifano ya watafiti mashuhuri kwenye Dini na vitabu vyao ni kama ifuatavyo. Israel Finkelstein - The Bible Unearthed: Archaeology’s New Vision of Ancient Israel and the Origin of Its Sacred Texts. Bart D. Ehrman - Misquoting Jesus: The Story Behind Who Changed the Bible and Why. Pia W. Montgomery Watt Muhammad at Mecca. Rodinson, Maxime. Muhammad. New York Review Books Classics, 2021.

Je, Imani ni urithi tu wa kijamii?​

Ni kweli watu wengi huzaliwa ndani ya dini fulani. Lakini Uislamu hautegemei “urithi kipofu” kama msingi wa ukweli wake.
Qur'an yenyewe inakosoa kufuata dini kwa sababu tu ya mababu:
“Na wanapoambiwa: Fuateni aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, husema: Hapana! Tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.” (2:170)
Kwa hiyo hoja ya Kiislamu si: “Ni kweli kwa sababu wazazi wangu waliamini.”
Bali ni: “Ni kweli kwa sababu kuna dalili za kiakili na kimaumbile zinazoonyesha uwepo wa Muumba.”
Katika teolojia ya Kiislamu (Ilm al-Kalam), uwepo wa Mungu hujengwa juu ya hoja kama:
Hoja ya uwezekano na lazima (contingency argument) – kila kilicho na mwanzo au kinachowezekana kuwepo kinahitaji kisababishi kisicho tegemezi.
Hoja ya mpangilio (design argument) – mpangilio wa sheria za kimaumbile unaashiria chanzo chenye maarifa.
Hoja ya maadili – kuwepo kwa maadili ya wajibu (objective morality) kunaashiria chanzo cha juu ya mwanadamu.

Hizi si hoja za “urithi wa kijamii”, bali ni hoja za kifalsafa.

“Atheism haisemi hakuna Mungu, bali hakuna ushahidi.”​

Hapa kuna suala la burden of proof.
Ni kweli Mwislamu anawajibika kutoa hoja za uwepo wa Mungu. Lakini pia dai la kwamba “hakuna ushahidi wa kutosha” ni dai la kifalsafa linalohitaji kutetewa.
Kwa mfano: Je, ni aina gani ya ushahidi unahitajika kuthibitisha Mungu? Je, lazima awe chini ya maabara?
Je, kila kilicho halisi lazima kipimwe kwa kifaa cha kisayansi?

Sayansi hushughulika na vitu vya kimaumbile (physical phenomena). Mungu katika Uislamu si sehemu ya ulimwengu wa maada ili apimwe kwa darubini.
Hivyo kutaka uthibitisho wa maabara kwa kitu kisicho cha maada ni makosa ya kimantiki (category error).

“Dini ilitokea kueleza mvua, radi, magonjwa…”​

Ni kweli dini za kale zilijaribu kueleza asili kwa mitazamo yao. Lakini hoja hii haikanushi uwepo wa Mungu — inaeleza tu sababu za kijamii za kuenea kwa imani.
Hata kama Dini ilitumika kuhalalisha mamlaka Au kudhibiti maadili , Hiyo haimaanishi Mungu hayupo. Inaweza tu kumaanisha watu walitumia dini vibaya.
Mfano: Sayansi pia imetumika kuhalalisha ubaguzi wa rangi (scientific racism), lakini hilo halikanushi ukweli wa sayansi yenyewe.
Kwa hiyo kueleza chanzo cha kijamii cha imani si sawa na kuthibitisha imani ni ya uongo. Hii huitwa genetic fallacy katika falsafa.

“Waumini wa kwanza waliamini kwa kujaza pengo la maarifa.”​

Hii ni hoja maarufu ya “God of the gaps”. Lakini Uislamu haumwekei Mungu kama mbadala wa maelezo ya kisayansi. Katika mtazamo wa Kiislamu: Sayansi hueleza jinsi (how) na Dini hueleza kwa nini (why)
Mfano wa Galileo Galilei mara nyingi hutumiwa kuonyesha mgongano wa dini na sayansi. Lakini huo ulikuwa mgongano kati ya taasisi ya kanisa na tafsiri fulani ya maandiko si hoja dhidi ya uwepo wa Mungu.
Katika historia ya Uislamu, wanasayansi kama: Ibn al-Haytham , Al-Biruni, Ibn Sina , waliona utafiti wa kisayansi kama njia ya kumtambua Muumba, si kumkanusha.

Kuhusu tafiti za wanahistoria wa dini​

Ni kweli kuna watafiti kama: Israel Finkelstein – The Bible Unearthed , Bart D. Ehrman – Misquoting Jesus ,W Montgomery Watt – Muhammad at Mecca , Maxime Rodinson – Muhammad , Lakini tafiti zao zinahusu: historia ya maandiko , maendeleo ya jamii na uchambuzi wa kisosholojia.
Hazithibitishi wala kukanusha uwepo wa Mungu. Zinachunguza historia ya dini, si ontolojia ya Mungu.

Nafasi ya Sayansi katika Imani​

Uislamu hauogopi sayansi. Kinyume chake: Unahimiza kutafakari (tafakkur) , pia , Unahimiza kutazama maumbile kama dalili (ayat) . Lakini sayansi ina mipaka: Haiwezi kuthibitisha maana ya maisha , Haiwezi kuthibitisha thamani ya maadili , Haiwezi kuthibitisha kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kitu . Haya ni maswali ya kifalsafa, si ya maabara
 
Jambo pekee mnaloweza kulizungumzia kwa Ufasha ni Stori za Kucheza PONO na Bikra 72 huko mnapopaita peponi.

Allah hayupo hizo ni stori za kusadikika Tu.

Uislamu hauna chochote çhenye uthibitisho juu ya Big Bang, Planetary Nebulae, Cosmic Microwave Radiation, hata hayo unayosema yameandikwa kwenye msaafu ni uthibitisho tosha juu ya namna gani: Islam is an Ignorant religion.

To say Heaven and Earth were óne is False, and Unscientific.

Kama Allah ndiye mwanzilishi wa muda, na maada, Je nani ndiye mwanzilishi wa Allah?

Historia inakupinga wewe: Utumwa, na Ukoloni havipo leo kwenye dunia ya Kisasa ni kwasababu ya Secular Humanism ambayo ndiye mwanzilishi wa Sheria za Haki za Binadamu.

Kwanza, kudai kwamba Uislamu unazungumzia “pono na bikra 72 tu” ni hoja dhaifu sana (strawman argument). Qur'an ina aya zaidi ya 6,000 zinazozungumzia tawhidi, maadili, haki, uchumi, elimu, sayansi ya kutafakari maumbile, na uwajibikaji wa mwanadamu. Kupunguza dini nzima kwenye simulizi moja ni ama ujinga au upotoshaji wa makusudi.

Pili, kusema “Allah hayupo” si hoja ya kisayansi bali ni msimamo wa kifalsafa. Sayansi huchunguza jinsi vitu vinavyofanya kazi, si kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kitu. Hata nadharia ya Big Bang haijibu chanzo cha uwepo , inaeleza mwanzo wa upanuzi wa ulimwengu unaoonekana. Swali la chanzo cha sheria za fizikia na uwepo wa kitu badala ya utupu bado lipo.

Unaposema Qur’an haizungumzii Big Bang, hiyo si kweli kabisa. Aya inayosema mbingu na ardhi zilikuwa kitu kimoja kisha zikatenganishwa haidai kuwa ni kitabu cha fizikia, bali ni ishara ya asili ya ulimwengu kuwa na mwanzo mmoja. Hata wanasayansi wakubwa kama Georges Lemaître — aliyependekeza nadharia ya Big Bang alikuwa padre. Hivyo kuamini Mungu na kukubali cosmology ya kisasa si vitu vinavyopingana.

Swali lako “kama Allah ndiye mwanzilishi wa muda na maada, nani aliyemwanzisha Allah?” lina tatizo la kimantiki. Kama muda ulianza na uumbaji, basi kuuliza “kabla ya Mungu” ni sawa na kuuliza “kaskazini mwa North Pole ni wapi?” — ni swali lisilo na muktadha. Kwa ufafanuzi wa kitheolojia, Allah si kiumbe ndani ya muda; Yeye ndiye sababu isiyosababishwa (Necessary Being). Huwezi kumuweka Muumba ndani ya mfumo aliouumba.

Kuhusu utumwa na ukoloni, historia haiko upande wako kama unavyodhani. Nchi zilizofanya biashara ya utumwa kwa kiwango kikubwa zilikuwa za Ulaya za Kikristo kisha zikaja kuzalisha falsafa ya Secular humanism baada ya mapinduzi ya kielimu. Lakini kabla ya hapo, Uislamu uliweka mfumo wa kupunguza na kuondoa utumwa kwa njia ya hatua kwa hatua karne nyingi kabla ya Ulaya kuamka. Leo hakuna mfumo mkamilifu; hata mataifa yanayojitangaza kuwa ya “human rights” bado yana vita, ubaguzi na unyonyaji wa kiuchumi.

Hoja ya msingi hapa ni hii, kutokubaliana na dini hakufanyi dini iwe ya kijinga. Na kuamini sayansi hakumaanishi lazima ukatae uwepo wa Mungu. Sayansi inaeleza mechanism. Dini inaeleza meaning.

Ukosoaji wenye nguvu unahitaji uelewa sahihi wa unachokikosoa. Vinginevyo, kelele zinabaki kelele na si hoja.
 
Je, Imani ni urithi tu wa kijamii?​

Ni kweli watu wengi huzaliwa ndani ya dini fulani. Lakini Uislamu hautegemei “urithi kipofu” kama msingi wa ukweli wake.
Qur'an yenyewe inakosoa kufuata dini kwa sababu tu ya mababu:
“Na wanapoambiwa: Fuateni aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, husema: Hapana! Tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.” (2:170)
Kwa hiyo hoja ya Kiislamu si: “Ni kweli kwa sababu wazazi wangu waliamini.”
Bali ni: “Ni kweli kwa sababu kuna dalili za kiakili na kimaumbile zinazoonyesha uwepo wa Muumba.”
Katika teolojia ya Kiislamu (Ilm al-Kalam), uwepo wa Mungu hujengwa juu ya hoja kama:
Hoja ya uwezekano na lazima (contingency argument) – kila kilicho na mwanzo au kinachowezekana kuwepo kinahitaji kisababishi kisicho tegemezi.
Hoja ya mpangilio (design argument) – mpangilio wa sheria za kimaumbile unaashiria chanzo chenye maarifa.
Hoja ya maadili – kuwepo kwa maadili ya wajibu (objective morality) kunaashiria chanzo cha juu ya mwanadamu.

Hizi si hoja za “urithi wa kijamii”, bali ni hoja za kifalsafa.

“Atheism haisemi hakuna Mungu, bali hakuna ushahidi.”​

Hapa kuna suala la burden of proof.
Ni kweli Mwislamu anawajibika kutoa hoja za uwepo wa Mungu. Lakini pia dai la kwamba “hakuna ushahidi wa kutosha” ni dai la kifalsafa linalohitaji kutetewa.
Kwa mfano: Je, ni aina gani ya ushahidi unahitajika kuthibitisha Mungu? Je, lazima awe chini ya maabara?
Je, kila kilicho halisi lazima kipimwe kwa kifaa cha kisayansi?

Sayansi hushughulika na vitu vya kimaumbile (physical phenomena). Mungu katika Uislamu si sehemu ya ulimwengu wa maada ili apimwe kwa darubini.
Hivyo kutaka uthibitisho wa maabara kwa kitu kisicho cha maada ni makosa ya kimantiki (category error).

“Dini ilitokea kueleza mvua, radi, magonjwa…”​

Ni kweli dini za kale zilijaribu kueleza asili kwa mitazamo yao. Lakini hoja hii haikanushi uwepo wa Mungu — inaeleza tu sababu za kijamii za kuenea kwa imani.
Hata kama Dini ilitumika kuhalalisha mamlaka Au kudhibiti maadili , Hiyo haimaanishi Mungu hayupo. Inaweza tu kumaanisha watu walitumia dini vibaya.
Mfano: Sayansi pia imetumika kuhalalisha ubaguzi wa rangi (scientific racism), lakini hilo halikanushi ukweli wa sayansi yenyewe.
Kwa hiyo kueleza chanzo cha kijamii cha imani si sawa na kuthibitisha imani ni ya uongo. Hii huitwa genetic fallacy katika falsafa.

“Waumini wa kwanza waliamini kwa kujaza pengo la maarifa.”​

Hii ni hoja maarufu ya “God of the gaps”. Lakini Uislamu haumwekei Mungu kama mbadala wa maelezo ya kisayansi. Katika mtazamo wa Kiislamu: Sayansi hueleza jinsi (how) na Dini hueleza kwa nini (why)
Mfano wa Galileo Galilei mara nyingi hutumiwa kuonyesha mgongano wa dini na sayansi. Lakini huo ulikuwa mgongano kati ya taasisi ya kanisa na tafsiri fulani ya maandiko si hoja dhidi ya uwepo wa Mungu.
Katika historia ya Uislamu, wanasayansi kama: Ibn al-Haytham , Al-Biruni, Ibn Sina , waliona utafiti wa kisayansi kama njia ya kumtambua Muumba, si kumkanusha.

Kuhusu tafiti za wanahistoria wa dini​

Ni kweli kuna watafiti kama: Israel Finkelstein – The Bible Unearthed , Bart D. Ehrman – Misquoting Jesus ,W Montgomery Watt – Muhammad at Mecca , Maxime Rodinson – Muhammad , Lakini tafiti zao zinahusu: historia ya maandiko , maendeleo ya jamii na uchambuzi wa kisosholojia.
Hazithibitishi wala kukanusha uwepo wa Mungu. Zinachunguza historia ya dini, si ontolojia ya Mungu.

Nafasi ya Sayansi katika Imani​

Uislamu hauogopi sayansi. Kinyume chake: Unahimiza kutafakari (tafakkur) , pia , Unahimiza kutazama maumbile kama dalili (ayat) . Lakini sayansi ina mipaka: Haiwezi kuthibitisha maana ya maisha , Haiwezi kuthibitisha thamani ya maadili , Haiwezi kuthibitisha kwa nini kuna kitu badala ya kutokuwepo kitu . Haya ni maswali ya kifalsafa, si ya maabara

Unasema uislamu unasapoti sayansi, je unaweza kuniambia Sayansi ina maoni gani juu haya mambo yaliopo kwenye maandiko ya Imani ya Kiislamu?

  1. Muhammad kugawanyisha mbalamwezi kuwa vipande viwili. Quran 54:1
  2. Musa kuganwanyisha bahari. Quran 26:63
  3. Nabii Isa alipozungumza maneno akiwa kichanga. Quran 19:29-30
  4. Nabii Isa alipoumba na kumpa pumzi Ndege kwa kutumia udongo uliofinyangwa. Quran 3:49, 5:110
  5. Muhammad kupaishwa kwenda peponi kwa kupitia farasi mwenye mbawa mwenye uwezo wa kupaa (Buraq).
  6. Uwepo wa Mbingu 7.
  7. Uwepo wa Wanawake bikra 70 tayarishwa kwa ajili ya kucheza show ya Ponografia.
 
Hapana sio maneno yote kwa 100% ni ya kutoka kwa Mungu kwenye hivyo vitabu.

Unajua mkuu shida kubwa ni utofauti wa uelewa wetu kwenye kujaribu kutafsiri maana ya hayo maandiko kwenye hivyo vitabu. Hivi unajua kwamba kuna baadhi ya waumini wa hivyo vitabu hawaamini uwepo wa uchawi na majini?
SAsa kama sio 100% navyenyewe vinajinasibu 100% (hata wale wa inspired) si mgogoro huo tayari unaanza

Hao wasioamini mauchawi si watakua wanapingana na vitabu vyenyewe.

concept nzima inaweza kusound bila vitabu ofcourse kama miaka hiyo ya zamani , ila kwasasa kwa declaration ya vitabu inakua ngumu kuviweka mbali na ndo lawama zinapoanzia hapo.

Ndo maana kuna watu wanaswma hii framework yenyewe yote inashida huwezi wapa watu mgogoro wa fikra, alafu wakianguka upande wapili wanaenda kula kiberiti. --- jambo hili bila hata vitabu , ila wakija wenye quatations huwaambii kitu
 
Uhakika ni nini?

Ukweli ni nini?

Imani ni nini?
Uhakika kimsingi ni hali ya kutokuwa na shaka. Ni hisia inayotokea akilini mwako.
Si lazima uwe ukweli. Unaweza kuwa na uhakika wa uongo, na unaweza kuwa huna uhakika wa jambo ambalo kwa kweli ni la kweli.

Kwa ufupi kabisa: Ukweli ni hali ya kuwa sahihi au kupatana na uhalisi (reality).
 
Back
Top Bottom