Navyojua atheist ni mtu asiye amini Mungu/miungu, mtu huyo ndio anaitwa atheist sasa mimi naamini Mungu hivyo sidhani kama utakuwa sahihi kwa maana ya hilo neno lenyewe.
Iko hivi ikiwa wewe una amini katika Mungu mmoja huyo wakwako yaani maanake hapo umechagua kuwa
Monotheist, na kwakua umewakataa miungu mingine yote kama
Zeus, Jupiter, Thor, El, Baàl, nk. Mpaka hapo wewe tayari ni
Atheist wa Asilimia letsay
95.
Nini kinakutofautisha wewe na
Atheists wenye asilimia
100?
Atheists wa Asilimia
100 wao wamekataa Miungu yote uliyoikataa wewe, pamoja na huyo mmoja wako unayemuanini.
Dhana pekee ambazo zinazoweza kuwashawishi
Atheists juu ya Uungu/UMungu ni kama zile za
Deists, Pantheists, Agnostics.
Kuna wakati watu wanadhani
Agnostics wapo ule upande wa Dini kama Ukristo, Uislamu, Uyahudi, nk.
Agnostics wote kwa Asilimia kubwa huwa ni maEX wa Dini fuata mkumbo i.e Ukristo, Uislamu, Uyahudi, nk. Wanashawishika zaidi na dhana ya Uungu/Mungu kutoka kwa
Deists, na Pantheists.
Hitimisho
Wakristo hukataa madai ya Uislamu.
Waislamu hukataa madai ya Ukristo.
Wayahudi hukataa yote mawili.
Na kila kundi hukataa miungu ya kale au ya tamaduni nyingine.
Atheists wanakubaliana na kila dini katika kukataa miungu mingine — isipokuwa wanaenda hatua moja zaidi kwa kukataa hata huyo Mungu wa mwisho aliyebaki.
Kwa hiyo, tofauti kati ya muumini na atheist si katika kitendo cha kukataa miungu, bali katika idadi ya miungu iliyokataliwa.