Contradictions halisi hizi hapa, Nakuwekea kabisa.
Kwanza tuanze na
The four Omnis of God.
Omniscient(All knowing God)-Mungu mjuzi wa vyote tangu mwanzo na hata milele.
Omnipotence(All powerful God)-Mungu muweza wa yote.
Omnipresence (Being everywhere at once) - Mungu aliyepo kila mahali kwa wakati wote.
Omnibenevolence(An All loving God)- Mungu mwenye upendo na huruma.
Sasa hizi
Four Omnis of God ukizileta kwenye
The problem of Evil(Epicurean paradox) Zinatengeneza
Contradictions . View attachment 3547475
Mungu muweza wa vyote na mwenye upendo angeweza kuumba Dunia isiyo na uovu, Lakini Dunia yenye uovu ipo, Mungu mwenye upendo na muweza wa vyote hawezi kuwepo kwenye Dunia yenye uovu.
Kwa sababu kama Mungu ni upendo, mabaya yasingekuwepo. Mabaya yapo, Mungu mwenye upendo hawezi kuwepo.
Kama Mungu ni muweza wa vyote, angeweza kuumba Dunia isiyo na mabaya. Dunia yenye mabaya ipo, Kama huyo Mungu ni muweza wa vyote na hapendi mabaya, Sasa alishindwaje kudhibiti mabaya yasiwepo?
Ni either Mungu huyo hawezi yote, ndio maana alishindwa kuumba Dunia isiyo na mabaya au Mungu huyo hayupo ndio maana Dunia ina mabaya.
Kuwepo kwa Mungu mwenye upendo na muweza wa vyote kwenye Dunia yenye mabaya, kuna tengeneza
contradictions .
Mungu mjuzi wa vyote tangu mwanzo na hata milele HAHITAJI
freewill ili kujua binadamu atachagua kutenda matendo gani. Kwa sababu yeye anajua yote. No need to test.
Uwepo wa freewill kwa Mungu mwenye kujua yote, kuna tengeneza contradictions.
Kwa sababu huyo Mungu kama anajua yote, freewill ni ya nini wakati anajua matendo yote utakayo tenda?
Anaweka freewill kukupima ili agundue nini asichokijua?
Kama freewill ipo basi Mungu hajui yote, ndio maana aliweka freewill ili aweze kujua matendo tutakayo tenda.
Lakini kama Mungu anajua yote, freewill haipo. Kwa sababu Mungu tayari anajua matendo yote tutakayo tenda, right from the beginning.
Kuwepo kwa freewill na Mungu mjuzi wa vyote, kunaleta contradictions.
Sasa kama bado huoni contradictions. Basi imani zenu zimewapumbaza ku ignore logic and reasoning.
Hakuna ushahidi wala uthibitisho wa kuwepo Mungu.
Ni imani tu inayo aminiwa na watu wengi. Ndio inafanya Mungu afosiwe yupo kwa vile majority wanaamini hivyo.
Uthibitisho wa kuwepo Mungu haupo. Watu wanafuata tu mkumbo kuamini Mungu yupo kwa vile majority ya watu wana amini yupo.
Hii ni
popularity fallacy.
Kama Mungu yupo kwa nini unahitaji kuamini?
Kama Mungu yupo kwa nini haujui kwa uhakika na uthibitisho kabisa?
Kwa nini unahitaji imani kuamini na si uhakika wa kujua?
Wanasayansi na wanafalsafa wengi kuamini Mungu yupo, HAKUFANYI Mungu huyo awepo kweli. Bado ni imani tu isiyo na uthibitisho.
Kutumia wanasayansi na wanafalsafa walioamini Mungu yupo, kuhitimisha moja kwa moja kwamba kuna Mungu, Ni kufanya logical fallacy inaitwa
Celebrity fallacy.
The celebrity fallacy (or appeal to celebrity) is a logical error occurring when a claim is accepted as true simply because a famous and popular person belives and supports it, rather than based on evidence. It is a form of faulty appeal to authority where the celebrity lacks relevant expertise in the subject.
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika, kuhisika na kupimika.
Vitu vingi havipo physically ila vinaweza kupimika na kufahamika vipo. Vitu kama upepo, joto, baridi n.k
Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.
Mungu ni fictional character wa kwenye hekaya za Biblia na Quran na maandiko mengine ya kiimani.