Godbless Lema ni mwanasiasa anayejiamini mno

howard

Senior Member
Feb 21, 2011
188
28
Wanajamvini nilikuwa naangalia taarifa ya habari Channel 10 kuhusu sakata la dodoma nillkichokiona kwa Lema ni kuwa huyu ni mtu jasiri. Mkuu wa mkoa anasema "kuanzia sasa wanasiasa hawaruhusiwi kwenda vyuoni na kufanya shughuli za kiasiasa kwa kuwa wanasababisha vurugu na ndio maana wanafunzi wa UDOM wamejaa pale na kuletya vurugu". Lema akahojiwa akasema na "yeye hatasimama kwenda kwenye vyuo kwa kuwa si dhambi ataenda vyuo vingi tu hakuna sheria yoyote anayovunja kuongea na wanafunzi na mazingira anayoongea ni yale aliyokuwepo mkuu huyo wa mkoa ingawa watu wa TV hawakuonyesha mkuu huyo wa mkoa alikuwa wapi. anasema alikwenda UDOM kuwaambia wanafunzi waje kutoa mawazo yao kwa kuwa mswada umeandikwa kwa kiingereza na wale ni wasomi wanajua wanachangia nini. Nikasema hivi huyu jamaa akipewa uongozi wa aina yoyote sehemu anayoisimamia itakuwaje, Namkubali sana huyu jamaa ktk kuwakilisha hisia zake.Mungu amlinde
 
Mkuu wa mkoa mpuuzi kwani wanafunzi si raia?hawana haki ya kujadili mustakabali wa nchi yao?walizoea kuburuta wananchi muda huo sasa basi!
 
mpumbav mkuu wa mkoa, hajielewi, si amewekwa na ccm,,,, lema my mp,,, ulituahidi wakazi wa arusha wakati unaomba kura kuwa utakua mbele yetu siku zote na hauogopi chochote isipokua MUNGU,,,, nakushukuru sana mbunge wangu kwa kutimiza ahadi yako hiyo, na kamwe sintojutua kukupigia kura,,, God bless u GODBLESS LEMA,,, may the spirit which u have never ever fade, wana arusha tunakukubali mbaya,,,
 
Huyu jamaa sio tu anajiamini ila anajua anasimamia nini. Huyu jamaa ni very critical, analytical na bold. Nilifanikiwa kuwa kwenye mkutano wake pale iringa last week nilimvulia kosia. He is just GREAT.
 
Dah,naomba tu Mungu amlinde maana naamini watakua wana muwinda sana
 
Mbunge wetu huyo ni wa ukweli sana... Anajiamini sana.. Na hiyo ni jinsi inavyopaswa siasa kuwa..

Lema mwendo mdundo ila tu angalia wasikutoe kafara kama akina kolimba...
 
Nimekuwa nikimfatilia kwa umakini mkubwa sana Godbless Lema kila anapoongea...niligundua mambo yafuatayo kwake...

  1. Ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kujieleza...
  2. Ana ujasiri mkubwa sana ambao mtu wa kawaida hawezi kuwa nao..
  3. Ni patriotic leader...yupo tayari kwa lolote..
Bravo Godbless lema....vijana wa kitanzania tunachimba mengi mazuri toka kwako....
 
kaka, hawawezi kumtoa kafara,,, arachuggah hapatakalika... Hata wafanyeje, kwanza nangoja kwa hamu izo 21 dayz ziishe,, mi nakuhakikishia, machalii wataleta kwere mbaya.. Ccm wajiandae tu kumtoa meya,,,,
lema anakubalika sana nyumbani na hata nje, they cant dare touch him
 
Wanajamvini nilikuwa naangalia taarifa ya habari Channel 10 kuhusu sakata la dodoma nillkichokiona kwa Lema ni kuwa huyu ni mtu jasiri. Mkuu wa mkoa anasema "kuanzia sasa wanasiasa hawaruhusiwi kwenda vyuoni na kufanya shughuli za kiasiasa kwa kuwa wanasababisha vurugu na ndio maana wanafunzi wa UDOM wamejaa pale na kuletya vurugu". Lema akahojiwa akasema na "yeye hatasimama kwenda kwenye vyuo kwa kuwa si dhambi ataenda vyuo vingi tu hakuna sheria yoyote anayovunja kuongea na wanafunzi na mazingira anayoongea ni yale aliyokuwepo mkuu huyo wa mkoa ingawa watu wa TV hawakuonyesha mkuu huyo wa mkoa alikuwa wapi. anasema alikwenda UDOM kuwaambia wanafunzi waje kutoa mawazo yao kwa kuwa mswada umeandikwa kwa kiingereza na wale ni wasomi wanajua wanachangia nini. Nikasema hivi huyu jamaa akipewa uongozi wa aina yoyote sehemu anayoisimamia itakuwaje, Namkubali sana huyu jamaa ktk kuwakilisha hisia zake.Mungu amlinde

Huyo mkuu wa mkoa ni mpuuzi na jmamosi tunaenda kufungua tawi pale UDOM tunamkaribisha alete askari wa kutosha wakutukamata, kuhusu TBC1 tutazunguka nchi nzima kuwaambia wananchi waachane nayo kwani ni kituo cha kuficha uovu wa mafisadi
 
Nimekuwa nikimfatilia kwa umakini mkubwa sana Godbless Lema kila anapoongea...niligundua mambo yafuatayo kwake...

  1. Ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kujieleza...
  2. Ana ujasiri mkubwa sana ambao mtu wa kawaida hawezi kuwa nao..
  3. Ni patriotic leader...yupo tayari kwa lolote..

Bravo Godbless lema....vijana wa kitanzania tunachimba mengi mazuri toka kwako....
Huyu jamaa ananifundisha kitu kimoja usimuogope mtu mradi hauvunji sheria Arusha hongereni kwa kutuletea jasiri wa ukweli
 
Alivyokuwa akiongea na kujibu hoja za kipuuzi zilizotolewa na RC, Lema alionesha ni namna gani kiongozi wa Tanzania anatakiwa kuwa. mawazo yake ni shirikishi na hayana unafiki na kujikomba, nampongeza sana
Shame on you mkuu wa mkoa wa dodoma
 
Huyo mkuu wa mkoa ni mpuuzi na jmamosi tunaenda kufungua tawi pale UDOM tunamkaribisha alete askari wa kutosha wakutukamata, kuhusu TBC1 tutazunguka nchi nzima kuwaambia wananchi waachane nayo kwani ni kituo cha kuficha uovu wa mafisadi

hao TBC ni mafisadi mkuu kama unavyosema tokea aondoke Tido kituo kinamilikiwa na wizara kwa sasa na kuendeshwa na watui wa wizara nadhani ujinga mtupu
 
Alivyokuwa akiongea na kujibu hoja za kipuuzi zilizotolewa na RC, Lema alionesha ni namna gani kiongozi wa Tanzania anatakiwa kuwa. mawazo yake ni shirikishi na hayana unafiki na kujikomba, nampongeza sana
Shame on you mkuu wa mkoa wa dodoma

Nilitamani wangeonyesha mkuu wa mkoa wakati lema anaongea yale maneno nione sura ilivyomshuka kwa kijana kumpa ukweli wa kil;e anachokiwaza pale pale bila kumung`unya maneno bravo lema wewe ni role model wangu
 
Ndio maana nadiriki kuwaita baadhi ya viongoz wa aina ya huyu mzee wahuni wa uzeeni. Absolutely hopeless
 
Nchi ishauzwa hiii shenzi kabisa, turudishieni nchi yetu mafisadi tunataka katiba mpya kwa sasa
 
Tunahitaji viongozi kama hawa, achana nahawa vibaraka waliojaa katika ofisi za serikali hawana lolote la maana.
 
Mkuu wa mkoa mpuuzi kwani wanafunzi si raia?hawana haki ya kujadili mustakabali wa nchi yao?walizoea kuburuta wananchi muda huo sasa basi!

Siasa bana, huyu mkuu wa mkoa jamaa walikuwa wanamuhusudu sana na kumwita mtasha pale UDSM alipokuwa kitengo cha High Voltage pale kwa wahandisi, hivi sasa amukuwa na corrupted mind kiasi kwamba simple reasoning and flow of logic and Kirchhoff's application zote kasahau kwa kulinda ulaji wake.
 
Yaani wa kuu wa mikoa wote ni makada wa chama tawala so kwasasa wanataka watumie uboss wao kupingana na ukweli, ila ukweli haujawahi kushindwa hata siku moja, wanajaribu kuchelewesha haki za mtanzania ila mwisho umefika
 
The Rc is so inocent and green minded. Ana akili kama ya mtoto mchanga.
 
Back
Top Bottom