Hayo ni mawazo yako,tena mawazo finyu,nani amekuambia kazi ya mbunge ni kujenga barabara,vituo vya afya,kuleta maji n.k? huo upotoshaji mnaufanya baada ya kukosa mbinu mbadala za kupambana na wapinzani wenu,kama suala la maendeleo ndiyo tija ya mbunge kubaki basi wapinzani ulaya magharibi na marekani wasingepata viti vya uwakilishi kwenye mabunge yao kwa sababu nchi zao zimeendelea.Nawapongeza wabunge wa upinzani kwa kutimiza majukumu yao ya kuikosoa serikali na kuanika maovu,kwenu nyinyi watawala ndio mnaopaswa kuwaletea watanzania maendeleo kwa sababu ndie mnao kusanya kodi na daima mjue kuwa kuleta maendeleo ni wajibu wa serikali na si zawadi kama mnavyowadanganya watanzania.Naona kengele imelia anza kufungasha virago.......