Nimezisoma hizo nyarakafeki, sijaona ukashfa wala chembe ya kuiua chadema!
Mods: kumekuwa na taswira flani ya uachaji
wa mijadala ya kizushi inayotupotezea mda na kushusha hadhi ya jukwaa hili!
Uzushi kama huu haina haja ya kuuacha watu waendelee kuangalia!
Nimezisoma hata mimi pia..ni za kutengenezwa zenye lengo chafu...hazina ukweli wowote..chadema haiwezi kuambatana na wanafiki kama wewe MAMA POROJO _kama unaona CHADEMA Itaingia kaburini sababu ya hizo nyaraka iacha iingie wala hatutahitaji machozi yenu nyie wanafiq.
waulize wanachadema wa Arusha walioandika hiyo barua kwenye makao makuu ya chama. Mimi simo ni mjumbe tu.
Siasa ni mchezo wa mahesabu. Adui yako anachozingatia kuharibu ni image yako. Akishaiua anakuwa amimaliza trust ya watu kwako. Yaani ukiweza kumfanya mtu atiliwe mashaka, unakuwa umemmaliza kwa kiasi kikubwa. Unamfanya ajiteteee sana na unakuwa umempunguza kasi au nguvu. CDM muwe makini. Wanajua ukiwapiga wachungaji kondoo watapoteaa!
Mkuu vijana wengi wa chadema ni brainwashed hivyo ni vigumu sana kukuelewa unaongea niniNdugu yangu kama umeambiwa hii document ipo makao makuu na wewe unataka kuamini kuwa ipo na ikizingatiwa CDM ni transparent si uwaulize kama kweli ipo makao makuu? Na kama ipo basi Mnyika aje hapa aseme wanayo na wanaifanyia kazi ili tufunfe huu mjadala mpaka watakapotoka na majibu ya tuhuma hizi, wewe povu linakutoka kwanini?
Nimezisoma hizo nyarakafeki, sijaona ukashfa wala chembe ya kuiua chadema!
Mods: kumekuwa na taswira flani ya uachaji wa mijadala ya kizushi inayotupotezea mda na kushusha hadhi ya jukwaa hili!
Uzushi kama huu haina haja ya kuuacha watu waendelee kuangalia!
Manago, kwa ufafanuzi kidogo tu, hawa madiwani walitimuliwa na Chadema, lakini serikali ya CCM ikalazimisha waendelee na nyadhifa zao wakati wakisubiri hukumu ya kesi waliofungua mahakamani kupinga kufukuzwa kwao. Hata hivyo pamoja na kushindwa kesi bado CCM ikawashauri wakate rufaa ambayo nayo haikufanikiwa na wakaamriwa kulipa dharama za kesi. Hapo mshauri wao mkuu, CCM, kama kawaida akawakana na kuwakimbia.Hivi mbona mnapenda kubisha vitu ambavyo vipo wazi ndugu zangu? Mgogoro wa madiwani ulikuwa lini na hii barua imeandikwa lini?
Manago, CCM ni genge la wahuni...they are capable of doing just about anything to retain power. Poor Manago, it really pains me that there are my fellow Tanzanians, like you, who will always fall for this kind of hogwash! What's the matter with you people? Come on, wake up...this is 2013!CCM sycophant said:Our operation chaos is working kwani our never ending online attacks zimemfanya ajipime, ok now one more to go, next on line ni dr. slaa, naye ni lazima ajitoe kugombea ili our best interest zitto ndiye awe mgombea wao 2015!
Niliwaambieni hawa hawana mgombea urais 2015, so sasa wale wote tunaoshirikiana kuwadhoofisha kwa kutumia mitandao tuzidishe mashambulizi kama ilivyo sasa, ninalo bomu moja la kiongozi wao mmoja maarufu kutaka kumbaka demu mmoja majuu na kesi ipo mahakamani na documents zipo, ina maana huyu akipewa kugombea chadema akapata urais hataruhusiwa kwenda hiyo nchi, sasa tutakuwaje na rais ambaye ni limited kwenye internatinional community? saafi sana mheshimiwa mbowe kwa kujipima na kuachia ngazi sasa mshauri na mwenzako slaa ajipime! Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Yeriko unataka kibisha kuwa Lema alilitembeza Tractor Arusha nzima na akatangaza litakuwa linalima mashamba ya wajane na wao wataweka mafuta tu? Au ndugu yangu wewe ni mtu wa Arusha kwenye JF lakini unaishi Mtwara? Tatizo siyo Tractor hapa wala kiwanja tatizo kubwa ni kwamba yeye Lema mwenyewe alitamka kwenye mkutano wa hadhara na siyo kwenye press.
Crashwise katika uzi wa Octoba 2012 alijibu baadhi ya tuhuma hizi, majibu ambayo yanapatikana https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...azi-print.htm. Kwa kifupi alielaza kuwaIli kuweka mambo sawa, kiwanja cha hospital iliyoahidiwa na Lema kipo Burka kilomita tatu kutoka barabara kuu na kwa sasa michoro ya hosp. inaendelea, trekta lilikabidhiwa kwa wamama wasiojiweza lakini itakuwa chini Arusha Dev Fund (ArDF).
Naye Mkurugenzi wa Afya na Elimu (ArDF) alitoa taarifa hii:
Awali ya yote napenda sana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutujaalia uhai.
Nimeisoma na kuielewa vema mada yako ndugu Lengio, wenye kichwa cha habari "Lema katupapeli shamba alilo omba kujenga hospital ya Wazazi".
Napenda kueleza mambo machache ambayo yatakuwa na umuhimu kwetu na taifa kwa ujumla, na hasa kuondoa uvumi huu ambao hauna tija kwa taifa na ambao umekuwa ukienezwa na watu wenye fikra mgando. Awali ya yote naomba kueleza kwamba mimi ni mmoja wa Waasisi wa Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Arusha mjini,(Arusha Development Foundation -ArDF) Naitwa Kamanda Magoma Jr Magoma, kwa sasa ni Mkurugenzi wa Elimu na Afya katika taasisi ya ArDF (nikiwa na jukumu kubwa la kuhakikisha tunafanikiwa kutimiza malengo ya taasisi ya ArDF katika nyanja za Afya na Elimu) si kama ambavyo mleta mada ameeleza bila kuwa na haya wala soni hata tone kwa kufanya upotoshaji wa hali ya juu bila kupima madhara yake kwa jamii kwamba "Lema katutapeli shamba alio omba kujenga hospital ya Wazazi". Napenda nileezee historia ya awali ambayo ninahisi wanachi wengi hasa waishio nje ya Arusha hawaifahamu na wangependa kuifahamu. Mwaka 2010 katika kampeni za uchaguzi mkuu Kamanda Lema aliahidi kwamba atajenga hospitali ya mama na mtoto katika jimbo la Arusha mjini endapo atapewa dhamana ya kuliwakilisha jimbo la Arusha mjini katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kamanda Godbless Lema alisema "ili kuondoa adha ya huduma za afya kwa mama na mtoto, hasa ikizingatia kuwepo kwa msongamano na wagonjwa katika hostpitali ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) mkinichagua nitajenga hostiptali ya mama na mtoto". Baada ya kamanda Lema kushinda alikutana na wadau wengine wa maendeleo katika jimbo la Arusha na kuamua kuanzisha Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la arusha (ArDF). Aidha moja na malengo ya msingi ya ArDF ni kujenga hospitali ya mama na mtoto, hivyo ili kuweza kufanikisha malengo ya kujenga hospitali kiwanja ni semehu ya vitu muhimu katika utekelezaji wa ujenzi, hivyo wadau wa Maendeleo walitupatia eneo la ukubwa wa ekari tano katika eneo la Burka, na ili kuweka kumbukumbu sahihi kiwanja hicho kiko chini ya ArDF kikiwa kinasimaniwa na Mama na Mtoto Foundation (Taasisi tanzu ya ArDF) na kwamba si kweli kiwanja hicho kinamilikuwa na Kamanda Godbless Lema na wala hakijabadilishwa umiliki wake wa awali kama ambavyo ndugu Lengio atanaka kuupotosha umma. Hivyo napenda kuwajulisha kwamba alicho andika ndugu Lengio ni uongo na hali ya juu na ni uposhaji uliopiliza mipaka. Chadema ni chama chenye viongozi makini wenye lengo la dhati la kuijenga Tanzania. Aidha nichukue fursa hii kuwajulisha wanachi wa Arusha kwamba tumekuwa tukiwasiliana na wadau na wataalum wa Afya na baada ya muda tutaanza ujenzi wa Hospitali ya mama na watoto, ikisimamiwa na Mama na Mtoto Foundation. "Umoja Wetu ndio Silaha yetu"
Naomba kuwasilisha,
Asanteni Wana JF.
Kamanda Magoma Jr Magoma
(Mkurugenzi wa Elimu na Afya ArDF)
(M/Kiti Mstaafu CHADEMA Wilaya Arusha Mjini)
Hoja na viroja vya nyongeza?
Hawa wanaosimamia ArDF ndio beneficiaries wa huo ufisadi, unategemea waseme nini? Kama chadema iko serious imtume Kitila akafanye uchunguzi huru Arusha juu ya hizi tuhuma.
Kwanza tumia akili ndogo tu, Development foundation gani haina ripoti ya mwaka? Anachotakiwa kufanya ni kuleta ripoti ya mwaka ya mapato na matumizi pamoja na majina na anuani za walionufaika na ArDF.
Mwache Kitila ana yake yanayomtosha. Hukuona katika sakata la Masalia juu ya madiwani wa Arusha?
Hivi hii ndiyo development fund pekee Tanzania? Hata kama ikiwa na ripoti ya mwaka ni kwa ajili ya nani? Hata wewe usiyehusika inakuhusu? Uliona wapi mambo hayo? Ndiyo maana wakaunda Fund. Kama ingekuwa ni kitu cha kila mtu huundi Fund ya nini? Ukiona hivyo hicho ni chombo maalum kwa ajili ya watu maalum. Kama huhusiki na hiyo Development Fund ripoti yake ya mwaka waitakiani?