Godbless Lema katika kashfa ya kuiua CHADEMA Arusha

Godbless Lema katika kashfa ya kuiua CHADEMA Arusha

My Take: Chadema isipokuwa makini umaarufu wake utapungua kutokana na migogoro mingi inayokikumba chama hicho. Mwaka 2015 si mbali jahazi linaonekana kuyumba ukilinganisha na huko nyuma. Wengi wataumia ndani ya chama hicho kwani umaarufu wa mtu unakuwa juu ya chama. Hizi tuhuma dhidi ya Lema hazikijengi chama bali zinakibomoa. Arusha hali si shwari.

mODS SAIDIA KUWEKA WAZI DOCUMENT HII ILI WANAJf WAPATE KUSOMA KWA URAHISI.
yule bwana ninavyomfahamu na siasa zake za jazba na kukurupuka;siku si nyingi atafanya kituko cha mwaka.mtaniambia.(mimi sio wassira lakini)
 
mama porojo hiyo document unayoisema iko wapi? Na huo mgogoro unaousema ni upi? Wewe umesoma hebu elezea kwa kifupi tukutathmini wewe coz wewe ndiyo mleta mada kuhusu Lema na CDM tuone kama unaijua Arusha vizuri au unaisikia tu
 
Nimezisoma hizo nyarakafeki, sijaona ukashfa wala chembe ya kuiua chadema!

Mods: kumekuwa na taswira flani ya uachaji wa mijadala ya kizushi inayotupotezea mda na kushusha hadhi ya jukwaa hili!

Uzushi kama huu haina haja ya kuuacha watu waendelee kuangalia!

Uzushu!!!!!!

Umeona majina ya walioandika na kusaini document hiyo. Tuambie walipeleka malalamiko chadema makao makuu kwa sababu ipi?

Kumtetea Lema kwa sababu ananga'a na kufumbia madhambi yake ni kuipeleka chadema kaburini
 
hujasoma na kuelewa ndio maana hujaona uzito wa kashfa hizo.

Mama porojo wal ausijali shida ya pro cdm hawataki kabisa kusikia kinyume na yale wanyoyapenda, sasa kosa lako hapa nini? we si umeleta document tu watu wajisomee? iwe ya kweli iwe ya uongo ni wao wanajua! vingapi hapa vinaletwa? agrrr
 
mama porojo hiyo document unayoisema iko wapi? Na huo mgogoro unaousema ni upi? Wewe umesoma hebu elezea kwa kifupi tukutathmini wewe coz wewe ndiyo mleta mada kuhusu Lema na CDM tuone kama unaijua Arusha vizuri au unaisikia tu

waulize wanachadema wa Arusha walioandika hiyo barua kwenye makao makuu ya chama. Mimi simo ni mjumbe tu.
 
Mama porojo wal ausijali shida ya pro cdm hawataki kabisa kusikia kinyume na yale wanyoyapenda, sasa kosa lako hapa nini? we si umeleta document tu watu wajisomee? iwe ya kweli iwe ya uongo ni wao wanajua! vingapi hapa vinaletwa? agrrr

CCM ikishikwa pabaya ni halali

CHADEMA ikishikwa pabaya ni haramu

Kwa mwendo huu tutafika salama????????
 
Mmemuandama dr slaa sana tu atikisiki,Mmeanza kumchimba Lema.NIKIWA KAMA Katibu mwenezi wa chadema ktk mojawapo ya kata hapa arusha Mjini napingana nawe.HALI YA CHADEMA ARUSHA NI SHWARI na hapa tulivyo ni vigumu mno hata kuona bendera ya magamba kwa mabalozi ambao nadhani HAWAPO siku hizi ktk jimbo hili.hizi ni siasa za sewage za mama porojo na akina mama chatanda.
Asante sana mkuu,hayo ndio majibu yao,sisi wanachadema list yetu ya ushindi iko palepale, apa Arusha tunajua mbunge wetu ni Lema,wala awawezi kutubabaisha kwenye hilo.
 
Uzushu!!!!!!

Umeona majina ya walioandika na kusaini document hiyo. Tuambie walipeleka malalamiko chadema makao makuu kwa sababu ipi?

Kumtetea Lema kwa sababu ananga'a na kufumbia madhambi yake ni kuipeleka chadema kaburini
Na wewe utaumia sana Chadema ikienda kaburini?
 
Mkuu, document hiyo imetoka kwenu Arusha na kusainiwa majina hayo umeyaona na imetumwa hadi makao makuu ya chadema. Mimi sijaongeza neno kwa nini unanishambulia mimi binafsi? badala ya kujibu yatokanayo na hiyo Document?
tunachotaka,hasa wana Arusha ni kuondoa magamba madarakani,mambo mengine tutakusikiliza baada ya 2015
 
Mods, ziweke wazi hiyo document naona naandamwa mimi au mwanaJf yeyote aziweke wazi kwani zina ushahidi wa ninachosema dalili hizo ni mbaya kwa chadema Arusha.
Kama ni dalili mbaya yaani kati wanachama millioni kadhaa wewe ndiye umeguswa kuliko wengine? Hebu kaa mbele ya kioo ujiangalie sura yako kama inakusuta.
 
Tunahitaji upinzani wa kweli nitaumia chadema ikienda kaburini. Vyama vingi ni kwa mujibu wa katiba ya nchi na vinachochea maendeleo.
Wewe nimeshafuatilia threads zako, hata za Kawe kuhusu Mdee na Ubungo kuhusu Mnyika.

Wewe kazi yako si kuimarisha bali kuleta habari mbaya dhidi ya CDM.

Nionyeshe hata thread moja uliyoleta habari mbaya dhidi ya CCM? Nakumbuka kuna watu wa Kigamboni walikuwa wanamlalamikia mbunge wao wewe ndiwe ulikuwa mtetezi mkuu. Au kwao hakuna makosa na migogoro, au wao ni wakamilifu?

Mbona kuna dhana ya kujivua gamba, na pamoja na posts zaidi ya 1700 ulizoleta hapa hakuna hata moja inayokosoa CCM.

Usitudanganye na majitaka yako.

Pilipili usiyoila yakuwashiani?
 
Mivutano ya nini? Kinachotakiwa ni Slaa atuthibitishie kama alipokea barua ya namna hiyo au lah. Hilo tu linatosha.
Tusifanye kazi ya utabiri, wakati wahusika wapo humuhumu.
Hayo yaliyoandikwa yote yameshawahi kusemwa hapa kwa nyakati tofauti, sasa imeletwa barua yenyewe. Je, Slaa hii barua ilipita kwako kama ilivyoandikwa hapo juu?
 
Bila shaka mlezi wa vyama vya siasa Tendwa atawashauri CDM nini cha kufanya.
 
Back
Top Bottom