Godbless Lema afunga kula akiwa Polisi ili kuliombea Taifa

Kulikuwa na mfalme aliota meno yake yote yameng'oka isipokuwa amebaki na jino moja basi akawaita watafsiri wa ndoto, kuna mmoja akamwambia ndugu zako wote watakufa isipokuwa wewe ndie utakaebaki, mfalme akakasirika akamuua yule mtafsiri,akaja wa pili akamwambia kuwa katika familia yako wewe ndio mwenye umri mrefu kuliko wote,mfalme akafurah sana na kumpa zawadi yule mtafsiri,hii maana yake ni nini,hata wakimwambia rais huta kufa milele haina maana kama uhalisia atakufa,ni ujinga kuwaambia watu umekula pilau wakati umekula mihogo
 
Alipokufa Nyerere wimbo wa "kifo hakina huruma" ulichezwa redioni mara moja tu!!! Kwa maana ulikuwa unazishushua akili zinazolandana na za kwako.

Nyie chama mfu chadema kupitia kauli zenu mnasisitiza kumuua rais kabla ya 2020, na ndiyo maana lichama lenu lazima lipotee kwenye ramani. Dkt Magufuli hafi! Ni mpaka Mungu atakapoamua, ila siyo kwa mkono wenu chama mfu chadema au mtu yeyote kwani Mungu anamlinda Dkt Magufuli 24hrs/7days/12month, na vyombo vya usala vitawashughulikia ilivyo vema
 
tuache ushabiki wa kisiasa, kwa kauli zile za Lema za kutabiri hatari na kumtishia kifo mkuu wa kaya ilikuwa lazima alamatwe ahojiwe. ... Ndio mana hata CIA ili kupata info za mipango ya siri ya osama walikuwa wanamuhoji kila wanaemuhisi tena walikuwa wanawahoji kwa kutumia mbinu mbalimbali za mateso mpaka wanasema.

Matumizi ya Bi Clinton barua pepe yake binafsi kwa masuala ya kotaifa imemwingiza matatani.

Lema, ni utoto na uchanga wa kisiasa unamsumbua. Lakini siyo ajabu kwani sifa ya kuwa kiongozi CHADEMA ni ulopokokaji.
 
Afunge ili aende kwa Mungu tuwaonyeshe hawa jamaa hasira za umma
 
Kutoka ndani ya uvungu wa Moyo wangu nasema Hakuna kiongoz aliye karbu zaid na Mungu kama Godbless!! Analitendetea Haki Jina Lake na anaish kama Jina Lake, mara nying sana Jina huwakilisha tabia ya mtu, na ndomana Mungu alikuwa anawabilisha watumishi wake majina, kwa lema kuwekwa Mahabusu na yeye kuamua kufunga na kuomba kama vile Paulo na sila, kwa wacha Mungu husikia wivu, bali wapumbavu na wajinga na wenye laana hufurahia kwasababu wamepigwa upofu wa akili zao na shetan
 
Lema afungwe gerezani kifungo kirefu iwe fundisho kwa CHADEMA wengine wanaojitoa akili.....anasumbua sana huku mtaani hafai kukaa uraiani.
Peleka unafiki huko lumumba njaa mbaya sana buku saba zinakufanya unaandika pumba.
 
Nyie chama mfu chadema kupitia kauli zenu mnasisitiza kumuua rais kabla ya 2020, na ndiyo maana lichama lenu lazima lipotee kwenye ramani. Dkt Magufuli hafi! Ni mpaka Mungu atakapoamua, ila siyo kwa mkono wenu chama mfu chadema au mtu yeyote kwani Mungu anamlinda Dkt Magufuli 24hrs/7days/12month, na vyombo vya usala vitawashughulikia ilivyo vema
Tatizo letu wabongo ni watu wa kuzusha kisha mahakamani mnashindwa,alichosema lema rais atakufa sio atauawa,mbona alikwenda Loliondo si alikua na hofu ya kufa na ugonjwa
 
Hatuombei lakini ikitokea Lema kafia mikoni mwapolisi hivi wanadhani nchi itakalika.... Wajifunze nchi zingine huwa vurugu zinatokana na wachache kushiba madaraka
Abwabwaje Mh Lema (mbunge - dhamana ya kujua madhara ya matamshi yake), agome kula (ili iweje - akimjaribu Mungu), wewe uhamasishe vurugu ati nchi isitawalike!

Maneno yako ni ya uchochezi wa hali ya juu!
 
Anatafuta vidonda vya tumbo huyo. Akishavipata ataacha hako kamchezo.

Tutegemee ufunuo/maono mapya atakayofunuliwa toka kwa Mungu.
 
Afungwe tu .wamtie adabu.ikiwezekana wawe wanamchapa na viboko
Kutoka ndani ya uvungu wa Moyo wangu nasema Hakuna kiongoz aliye karbu zaid na Mungu kama Godbless!! Analitendetea Haki Jina Lake na anaish kama Jina Lake, mara nying sana Jina huwakilisha tabia ya mtu, na ndomana Mungu alikuwa anawabilisha watumishi wake majina, kwa lema kuwekwa Mahabusu na yeye kuamua kufunga na kuomba kama vile Paulo na sila, kwa wacha Mungu husikia wivu, bali wapumbavu na wajinga na wenye laana hufurahia kwasababu wamepigwa upofu wa akili zao na shetan
d
 
Inakuwaje kuwa karibu na Mungu wake kila anapotiwa nguvuni
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
sasa anataka kua tapeli wa mambo ya kiroho kama kina gwajima. safari hii hawamwachi ng'o hadi jela. ni mjinga anajitakia balaa mwenyewe.
 
Lema afunga mahabusu kuliombea Taifa

Arusha. Kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefunga ili kuwa karibu na Mungu wakati akiendelea kushikiliwa na polisi mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata alipotafutwa kwa simu, hakupokea.

Suala la Lema kuacha kula ili awe karibu zaidi na Mungu limeelezwa na mwenyekiti wa Chadema wa mkoa, Amani Golugwa ambaye amesema ameelezwa na mke wa mbunge huyo.

Lema, ambaye alikamatwa Jumatano iliyopita mkoani Dodoma na kuletwa mjini hapa Alhamisi, bado hajafikishwa mahakamani.

Imeelezwa kuwa viongozi wa chama chake wameshindwa kumuona kutokana na kuzuiwa na polisi.

Golugwa amesema amepokea ujumbe kutoka kwa mke wa mbunge huyo, Neema Lema kuwa mumewe ameamua kufunga na kuomba kwa ajili ya Taifa kuhusu mambo yanayoendelea na kuwa ameona kipindi hiki ambacho yupo rumande ni cha kuwa karibu zaidi na Mungu.

“Kama tunavyomjua Lema ni mtu anayempenda sana Mungu, ameamua kujinyenyekeza mbele za Mungu. Anafunga na kuomba jioni mke wake anampelekea chakula na amesema yupo katika hali nzuri,” amesema Golugwa.

Amesema wamejitahidi kutaka kumuona Lema, lakini wamegonga mwamba na wameshindwa kumwekea dhamana mbunge huyo.

“Ni jambo la kushangaza kama mtuhumiwa anaweza kukaa rumande zaidi ya saa 48 kama sheria inavyotaka, nadhani hapa siyo sheria tena, labda ni kwa mujibu wa maelekezo ambayo hatujui yametoka wapi na kwa malengo yapi,” amehoji Golugwa.

Juzi, Kamanda Mkumbo alisema Lema hataachiwa hadi upelelezi ukamilike na mwanasheria wa Serikali atakapokuwa amemaliza kuandaa mashtaka kwa kuwa amekuwa akirudia makosa yaleyale ya uchochezi.
View attachment 429872
Kama watu hawaruhusiwi kumwona wee habari hizi umezitoa wapi ?
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
-------------------

Arusha. Kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefunga ili kuwa karibu na Mungu wakati akiendelea kushikiliwa na polisi mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata alipotafutwa kwa simu, hakupokea.

Suala la Lema kuacha kula ili awe karibu zaidi na Mungu limeelezwa na mwenyekiti wa Chadema wa mkoa, Amani Golugwa ambaye amesema ameelezwa na mke wa mbunge huyo.

Lema, ambaye alikamatwa Jumatano iliyopita mkoani Dodoma na kuletwa mjini hapa Alhamisi, bado hajafikishwa mahakamani.

Imeelezwa kuwa viongozi wa chama chake wameshindwa kumuona kutokana na kuzuiwa na polisi.

Golugwa amesema amepokea ujumbe kutoka kwa mke wa mbunge huyo, Neema Lema kuwa mumewe ameamua kufunga na kuomba kwa ajili ya Taifa kuhusu mambo yanayoendelea na kuwa ameona kipindi hiki ambacho yupo rumande ni cha kuwa karibu zaidi na Mungu.

“Kama tunavyomjua Lema ni mtu anayempenda sana Mungu, ameamua kujinyenyekeza mbele za Mungu. Anafunga na kuomba jioni mke wake anampelekea chakula na amesema yupo katika hali nzuri,” amesema Golugwa.

Amesema wamejitahidi kutaka kumuona Lema, lakini wamegonga mwamba na wameshindwa kumwekea dhamana mbunge huyo.

“Ni jambo la kushangaza kama mtuhumiwa anaweza kukaa rumande zaidi ya saa 48 kama sheria inavyotaka, nadhani hapa siyo sheria tena, labda ni kwa mujibu wa maelekezo ambayo hatujui yametoka wapi na kwa malengo yapi,” amehoji Golugwa.

Juzi, Kamanda Mkumbo alisema Lema hataachiwa hadi upelelezi ukamilike na mwanasheria wa Serikali atakapokuwa amemaliza kuandaa mashtaka kwa kuwa amekuwa akirudia makosa yaleyale ya uchochezi.

Wewe Ndugu yangu unayejiita Mwanahabari huru nimekuwa nikisoma posts zako nyingi...na inaonekana huwa hufanyi editing posts zako...jitahidi uwe unazifanyia editing ili wewe mwenyewe kujiongezea credibility..ni ushauri tu, you can as well ignore ushauri wangu...
 
Back
Top Bottom