Godbless Lema afunga kula akiwa Polisi ili kuliombea Taifa

Godbless Lema afunga kula akiwa Polisi ili kuliombea Taifa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
-------------------

Arusha. Kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefunga ili kuwa karibu na Mungu wakati akiendelea kushikiliwa na polisi mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata alipotafutwa kwa simu, hakupokea.

Suala la Lema kuacha kula ili awe karibu zaidi na Mungu limeelezwa na mwenyekiti wa Chadema wa mkoa, Amani Golugwa ambaye amesema ameelezwa na mke wa mbunge huyo.

Lema, ambaye alikamatwa Jumatano iliyopita mkoani Dodoma na kuletwa mjini hapa Alhamisi, bado hajafikishwa mahakamani.

Imeelezwa kuwa viongozi wa chama chake wameshindwa kumuona kutokana na kuzuiwa na polisi.

Golugwa amesema amepokea ujumbe kutoka kwa mke wa mbunge huyo, Neema Lema kuwa mumewe ameamua kufunga na kuomba kwa ajili ya Taifa kuhusu mambo yanayoendelea na kuwa ameona kipindi hiki ambacho yupo rumande ni cha kuwa karibu zaidi na Mungu.

“Kama tunavyomjua Lema ni mtu anayempenda sana Mungu, ameamua kujinyenyekeza mbele za Mungu. Anafunga na kuomba jioni mke wake anampelekea chakula na amesema yupo katika hali nzuri,” amesema Golugwa.

Amesema wamejitahidi kutaka kumuona Lema, lakini wamegonga mwamba na wameshindwa kumwekea dhamana mbunge huyo.

“Ni jambo la kushangaza kama mtuhumiwa anaweza kukaa rumande zaidi ya saa 48 kama sheria inavyotaka, nadhani hapa siyo sheria tena, labda ni kwa mujibu wa maelekezo ambayo hatujui yametoka wapi na kwa malengo yapi,” amehoji Golugwa.

Juzi, Kamanda Mkumbo alisema Lema hataachiwa hadi upelelezi ukamilike na mwanasheria wa Serikali atakapokuwa amemaliza kuandaa mashtaka kwa kuwa amekuwa akirudia makosa yaleyale ya uchochezi.
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
Hana effect yoyote huyo, ale asile mara hii lazima afikishwe mahakamani. Kwani ni mara ya kwanza kufanya maigizo hayo!
 
Raisi wenu ndo nani si atakufa tuuu
Nyie chama mfu chadema kupitia kauli zenu mnasisitiza kumuua rais kabla ya 2020, na ndiyo maana lichama lenu lazima lipotee kwenye ramani. Dkt Magufuli hafi! Ni mpaka Mungu atakapoamua, ila siyo kwa mkono wenu chama mfu chadema au mtu yeyote kwani Mungu anamlinda Dkt Magufuli 24hrs/7days/12month, na vyombo vya usala vitawashughulikia ilivyo vema
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
Anafunga au anashinda njaa?
 
Mnafiki sana Lema, hivi unavyopanga mbinu za kumuua rais wetu kwa kutumia kauli za dharau kujionesha unakuwa na akili timamu???
Sasa mbona hammshitaki!..mnaenda kukagua kwake hamuoni kitu.hapo ndipo watoa mashtaka mnapochanganyikiwa,hamjui mmshitaki kwa lipi.ha haa
 
Polisi Arusha badala ya kuhangaika na mambo ya kitchen party waletwe Dar kwenye majambazi yanayoua poilsi
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea

tuache ushabiki wa kisiasa, kwa kauli zile za Lema za kutabiri hatari na kumtishia kifo mkuu wa kaya ilikuwa lazima alamatwe ahojiwe. Hata ingelikuwa ni ww ndo una jukumu la kumlinda mkuu wa kaya alafu ukasikia mtu anaongea tena kwa kujiamini kwamba unaemlinda yuko ktk hatari ni lazima huyo mtu umuhoji. Ndio mana hata CIA ili kupata info za mipango ya siri ya osama walikuwa wanamuhoji kila wanaemuhisi tena walikuwa wanawahoji kwa kutumia mbinu mbalimbali za mateso mpaka wanasema.
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
Safi mkuu, hivi si alisema amepewa maono na mungu kuhusu cjui nani akifanyaje cjui atakuaje
 
Naomba kujua kama wazazi wake wapo hai, nishauri kitu kwa tamaduni zetu za kichaga.
 
Back
Top Bottom