Godbless Lema afunga kula akiwa Polisi ili kuliombea Taifa

Godbless Lema afunga kula akiwa Polisi ili kuliombea Taifa

Anasaka huruma tu... Aache mdomo mchafu na nipo hapa central no one cares for Lema
 
The bible says mengine haya to kill ila kwa kuomba na kufunga. Maneno hayo ya litakapokukuta midomoni mwao Bwana Jesus mwenyewe. Keep it up boy we have joined you in your prayers and we believe this will strengthen you in your prophesies
 
Hatuombei lakini ikitokea Lema kafia mikoni mwapolisi hivi wanadhani nchi itakalika.... Wajifunze nchi zingine huwa vurugu zinatokana na wachache kushiba madaraka
 
So you are convinced he is the criminal? Be blessed
 
Magamba majinga sana, kama wangukuwa wanaelewa majina yananafasi gan ktk maisha yetu, wasinge thubutu kumgusu, Ila kwasababu wao na Idi amini wao, wamejawa na kiburi cha uzima ndiyo mana wanayatenda maovu yakuto kukubali ukweli, Nanina waambia malumumba Mungu siyo Mnafki kama mnavyofikiri na kumchezea, Hataweza Ikimbia Laana ya Mungt juu yenu
 
The issue is you guys have never been in the spiritual world
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
Mwenzenu anatafuta kuandikwa na magazeti,nyinyi mnachukulia kwa uzito mnaacha shughuli zenu na kukaa mnamfatilia huyo mtu.twaweza ifata siasa coz inaendelea hapa inchini na duniani kote,lakini kufuata kila la mwanasiasa wakati mwingine ni kujipotezea muda tu
 
Safi.Ni style tu ya maisha aliyoamua kuishi. Mshaurini ,ataishia jela na tutamsahau.
 
sharaapapopapo...yahwe..areepo popopo...tenet..ewe mola muondoshee dhuluma hii.
 
Ni kawaida yake huyo kujitafutia kiki kwa lazima.acha ashikishwe adabu asilete kujua hapa
 
Safari hii mbona ameanza kutafuta kick za 2015 mapema sana??!!!au Maji yameshazidi unga!!??
 
Hivi kweli yeye ndiye mpinzani kuliko wapinzani wengine? Hajui kwamba kumtakia mabaya Amir Jeshi Mkuu kunaamsha vyombo vya ulinzi na usalama na kusababisha watake kujua ana nia gani dhidi ya Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi yenye Silaha?

Lema hawezi kupata maono toka kwa Mungu. Hana utakaso wa kutosha kupata maono toka kwa Muumba. Kwa hiyo itabidi awaambie hao wanaomhoji alipewa maono hayo na nani kwa kuwa si toka kwa Mungu.
 
Lema afunga mahabusu kuliombea Taifa

Arusha. Kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefunga ili kuwa karibu na Mungu wakati akiendelea kushikiliwa na polisi mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata alipotafutwa kwa simu, hakupokea.

Suala la Lema kuacha kula ili awe karibu zaidi na Mungu limeelezwa na mwenyekiti wa Chadema wa mkoa, Amani Golugwa ambaye amesema ameelezwa na mke wa mbunge huyo.

Lema, ambaye alikamatwa Jumatano iliyopita mkoani Dodoma na kuletwa mjini hapa Alhamisi, bado hajafikishwa mahakamani.

Imeelezwa kuwa viongozi wa chama chake wameshindwa kumuona kutokana na kuzuiwa na polisi.

Golugwa amesema amepokea ujumbe kutoka kwa mke wa mbunge huyo, Neema Lema kuwa mumewe ameamua kufunga na kuomba kwa ajili ya Taifa kuhusu mambo yanayoendelea na kuwa ameona kipindi hiki ambacho yupo rumande ni cha kuwa karibu zaidi na Mungu.

“Kama tunavyomjua Lema ni mtu anayempenda sana Mungu, ameamua kujinyenyekeza mbele za Mungu. Anafunga na kuomba jioni mke wake anampelekea chakula na amesema yupo katika hali nzuri,” amesema Golugwa.

Amesema wamejitahidi kutaka kumuona Lema, lakini wamegonga mwamba na wameshindwa kumwekea dhamana mbunge huyo.

“Ni jambo la kushangaza kama mtuhumiwa anaweza kukaa rumande zaidi ya saa 48 kama sheria inavyotaka, nadhani hapa siyo sheria tena, labda ni kwa mujibu wa maelekezo ambayo hatujui yametoka wapi na kwa malengo yapi,” amehoji Golugwa.

Juzi, Kamanda Mkumbo alisema Lema hataachiwa hadi upelelezi ukamilike na mwanasheria wa Serikali atakapokuwa amemaliza kuandaa mashtaka kwa kuwa amekuwa akirudia makosa yaleyale ya uchochezi.
mp_lema.jpg
 
Lema Mungu yupo pamoja na wewe na binadamu atambue kuwa unaweza ukajilinda na bunduki,mabomu,vifaru,ndege za kivita na usalama wako ukajiamini asilimia 100,lakini hivyo vyote kwa mungu havina msaada wala faida linapokuja uwezo wa mungu,Lema acha binadamu aendelee kuchukua mamlaka ya mungu lkini vyote ni UBATILI MTUPU
 
Habari iliyonifikia Kutoke Huko Jijini Arusha inasema Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea
Huyo mungu anakua karibu nae akiwa rumande tu
Lema ni muoga wa selo
 
Kusema amefunga kula akiwa mikononi mwaka Police ili kuwa Karibu na Mungu nadhani hapo kuna Mashaka kidogo.

Lema kuna jambo analitafuta hapo ktk tamthilia hii
 
...Godbless J Lema Aliyokamatwa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge amefunga Kula ili kuwa Karibu Na Mwenyezi Mungu.

Tukumbuke tu Nchi hii inaitaji Maombi Sana kwa Mambo Mbalimbali yanayoendelea

Kama anataka kuwa karibu na Mungu wake sie wengine inatuhusu nini? halafu kwa nini anataka kuwa KARIBU naye badala ya KWENDA KABISA ili amuwahi MAGUFULI?
LOWASA kaiharibu kabisa CHADEMA. Hivi sasa limekuwa ni lichama la HOVYO kabisa, linapinga hata mambo ambayo CHADEMA original ilikuwa ikiyapigania huko nyuma.
WATANZANIA tumuombee Rais wetu Magufuli Mwenyezi Mungu amlinde dhidi ya hila za MAFISADI yote yaliyo CHADEMA, CCM na wapambe wao akina Lema, Mbowe nk.
 
Lema afungwe gerezani kifungo kirefu iwe fundisho kwa CHADEMA wengine wanaojitoa akili.....anasumbua sana huku mtaani hafai kukaa uraiani.
 
Back
Top Bottom