The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Wikiendi iliyopita, Jumamosi na Jumapili nilipata wasaa wa kutembea Goba kwa sehemu kubwa kwa sababu nilikua na ndugu yangu ambae katoka huko mkoani anataka kiwanja na kujenga Dar.
Ndugu yangu kafika hapa tayari alishachagua eneo analolitaka kua ni Goba, basi tukatafta madalali na kuanza kuzungukia viwanja, kuanzia makongo, Goba Senta, Goba Kulagwa, Goba Kilalata kwa awadhi, ostabei na sehemu nyingine nyingi.
Baada ya mizunguko ya siku 2 ndio nikagundua kwamba Goba ni Uswahilini kwenye nyumba za kisasa.
Kwa maana kwamba Goba haijapangiliwa kabisa. Goba kuna nyumba kali na za kisasa sana ila hakujapangwa, nyumba nzuri ila zimejegwa zigzaga, hakuna mitaa iliyonyooka.
Miaka 30 ijayo Goba itakua kama Manzese ya sasa ama Tandale, itakua uswazi.
Ni wakati sasa Serikali inapaswa kuingilia hii biashara ya upimaji na uuzaji ardhi. Hua najiuliza hivi viongozi wetu wakienda huko ulaya hawaoni wenzetu miji yao ilivyopangwa? Mbona huku kwetu wanaacha mambo yanakua hovyo hivi?
Ni hayo tu wakuu.