Girlfriend wangu kanitumia hela bila kumuomba

Nisiwachoshe, Ni hivi wakati nam approach mwaka 2011 tukiwa Chuo alikua na jamaa yake ambaye hatukua nae chuoni, ila kwasababu mimi ni king`ang`anizi sana ilifika mahali akanikubali, jamaa akipiga simu nikiwa nae nakaa kimya wanaongea, akikata tunaendelea kufanya yetu!

Nilivyomaliza undergraduate degree Mwaka 2012 yeye akaenda Chuo kingine (sitakitaja) kuendelea na degree couse chuo nilichokua nae yeye alikua anasoma diploma.

Ni mzuri sana kwa kweli, mzuri kila idara, nilikua nikisifiwa na watu hadi mabinti wenzie kila nilikopita nae hali iliyonifanya nimpende zaidi ukiachilia mbali na upole, ucha Mungu na ukarimu wake, kwa kifupi alikua na sifa za kuitwa mke, hata aliponishauri niliona tija kwenye ushauri wake.

Sasa wakati yupo hiko chuo alichoenda kujiendeleza tukiwa na mawasiliano mazuri tu, kuna siku yule jamaa yake alimtembelea akanishtukia kwamba natoka nae, akanipigia kwa no ya huyo msichana na kujitambulisha kisha kuniuliza ila nikakana katakata na kumwambia sisi ni marafiki na namfahamu yeye kama shem wangu, jamaa akafurahi sana!

Baada ya two days msichana akanipigia na kunishukuru huku akinishangaa kwa kumjibu jamaa vile. Siku mind couse jamaa alinitangulia kwamsichana alinieleza bayana.

Baada ya hapo tukawa na mawasiliano ya kawaida. Siku isiyo na jina msichana akanipigia analia, kumbe kagombana na jamaa vikali baada ya kumshauri jamaa wanunue kiwanja kwa hela ya mkopo aliyochukua huku jamaa akipinga na kutaka gari.

Nikamtuliza sana, akawa daily ananipigia. Huku na kule akaniomba msamaha akinisihi turudiane, kwasababu nilikua nampenda nikakubali wkt huo nikaweka spy chuoni kwao amchunguze, ikawa inasemekana ametulia ingawa anasumbuliwa sana.

Juzi kati wakati yuko field akaja kwangu, nikakaa nae for two weeks, akanitambulisha kwa mama yake ingawa ni kwa njia ya simu na mimi nikamtambulisha kwa wazee wangu live na wakampokea. Akanishauri tutafute kiwanja na yeye atachangia hela, tena tutafute mkoa nitakaopenda kuishi mimi.

Akarudi zake field, shirika alilokua anafanya field likampa afanye programme flani maalum kutokana na ufanisi wake kazini na wakamlipa laki kila siku for 10 consecutive days.

Cha kushangaza sasa, jana kanitumia laki nne bila kumuomba, nimepigwa na butwaa kwani hii sio kawaida kwa mabinti wa karne hii, eti jamani mkihusianisha na scenario niliyowapa, hapa kuna mapenzi.
Wadada wa leo hawakawii kukutangazia Umarioo....
 
mnh, hii nadhani ni hadithi hadithi, uongo njoo, ukweli njoo utamu kolea
 
dah nmecheka na kufurahi sanaa kwenye huu Uzi wakuu. Jf ndo kila kitu
 
Inaonekana wkt alipokwambia wamegombana wewe ulimshawishi ili uonekane wewe ndo bora sasa jua siku na wewe mkigombana yule anaye mfuatilia nae atuwa bora mwanamke wa hivyo hafai hana msimamo siku yakikukuta uje utuambie
 
Ushauri unaopewa changanya na zako:
bado karne hii kuna mabinti wema tu wanaoamini kuwa maisha ni kusaidiana na kama lengo lenu ni kuoana hapo anakutega kuwa hiyo hela unafanyia nini; Cha muhimu ni kuwekeza katika maendeleo na kumshirikisha kwa kila jambo. Una bahati binti kukukumbusha mnunue kiwanja? Angekuwa selfish angeweza kununua mwenyewe na wazazi wake akajenga taratibu, but she believes in togetherness. Kama waihofia sana hiyo hela muulize kwa upole kuwa amekutumia kwa madhumuni ya kiwanja au nini?
 
hapo sioni cha kushangaza.....au kutumiwa pesa za kuongezea kiwanja...?
 
Nisiwachoshe, Ni hivi wakati nam approach mwaka 2011 tukiwa Chuo alikua na jamaa yake ambaye hatukua nae chuoni, ila kwasababu mimi ni king`ang`anizi sana ilifika mahali akanikubali, jamaa akipiga simu nikiwa nae nakaa kimya wanaongea, akikata tunaendelea kufanya yetu.

Nilivyomaliza undergraduate degree Mwaka 2012 yeye akaenda Chuo kingine (sitakitaja) kuendelea na degree couse chuo nilichokua nae yeye alikua anasoma diploma.

Ni mzuri sana kwa kweli, mzuri kila idara, nilikua nikisifiwa na watu hadi mabinti wenzie kila nilikopita nae hali iliyonifanya nimpende zaidi ukiachilia mbali na upole, ucha Mungu na ukarimu wake, kwa kifupi alikua na sifa za kuitwa mke, hata aliponishauri niliona tija kwenye ushauri wake.

Sasa wakati yupo hiko chuo alichoenda kujiendeleza tukiwa na mawasiliano mazuri tu, kuna siku yule jamaa yake alimtembelea akanishtukia kwamba natoka nae, akanipigia kwa no ya huyo msichana na kujitambulisha kisha kuniuliza ila nikakana katakata na kumwambia sisi ni marafiki na namfahamu yeye kama shem wangu, jamaa akafurahi sana!

Baada ya two days msichana akanipigia na kunishukuru huku akinishangaa kwa kumjibu jamaa vile. Siku mind couse jamaa alinitangulia kwamsichana alinieleza bayana.

Baada ya hapo tukawa na mawasiliano ya kawaida. Siku isiyo na jina msichana akanipigia analia, kumbe kagombana na jamaa vikali baada ya kumshauri jamaa wanunue kiwanja kwa hela ya mkopo aliyochukua huku jamaa akipinga na kutaka gari.

Nikamtuliza sana, akawa daily ananipigia. Huku na kule akaniomba msamaha akinisihi turudiane, kwasababu nilikua nampenda nikakubali wkt huo nikaweka spy chuoni kwao amchunguze, ikawa inasemekana ametulia ingawa anasumbuliwa sana.

Juzi kati wakati yuko field akaja kwangu, nikakaa nae for two weeks, akanitambulisha kwa mama yake ingawa ni kwa njia ya simu na mimi nikamtambulisha kwa wazee wangu live na wakampokea. Akanishauri tutafute kiwanja na yeye atachangia hela, tena tutafute mkoa nitakaopenda kuishi mimi.

Akarudi zake field, shirika alilokua anafanya field likampa afanye programme flani maalum kutokana na ufanisi wake kazini na wakamlipa laki kila siku for 10 consecutive days.

Cha kushangaza sasa, jana kanitumia laki nne bila kumuomba, nimepigwa na butwaa kwani hii sio kawaida kwa mabinti wa karne hii, eti jamani mkihusianisha na scenario niliyowapa, hapa kuna mapenzi.

Usiwe na shaka ww kula tu haitapita ht mwez utaombwa zaid ya hz anasafisha njia
 
sifa ya mwanamke akishajua kuwa mwanaume mbeleni atakuwa ana future nzuri ya maisha basi atakufanyia kila jambo zuri ikiwemo pesa nk lakini hivyo vitu vyote alivyokugharamia vitarudi mkiingia ndoani,KUNA MSEMO UNASEMA HELA YA MWANAMKE HAILIWI HIVI HIVI JUAKUWA ITARUDI

Kweli kbs itarud hy
 
kama kwelie mnapendana kwanini hamuoani, mwaka wa nne mnapotezeana muda tu, mie mambo ya kupewa pesa sitachangia kwa kweli, kwanza utuambie kikwazo cha kutooana ni kipi. Kuna aliyedai eti ukimuoa huyo jamaa mwingine atakua mchepuko, sio kweli, akipewa ndoa atatulia, hawezi kumuacha yule maana hajui msimamo wako.
 
Blaza muda wa kazi huu,achana na hizo fantasies.Samahani lakini mkuu! Amicus Curiae
 
Last edited by a moderator:
Kuku hupewa mchele ili aliwe na wali. Akili zako changanya na mawaidha ya bure.Hamna free lunch karne hii.
 
kama kwelie mnapendana kwanini hamuoani, mwaka wa nne mnapotezeana muda tu, mie mambo ya kupewa pesa sitachangia kwa kweli, kwanza utuambie kikwazo cha kutooana ni kipi. Kuna aliyedai eti ukimuoa huyo jamaa mwingine atakua mchepuko, sio kweli, akipewa ndoa atatulia, hawezi kumuacha yule maana hajui msimamo wako.
chalii HAJIAMINI ,.. NA HAWEZI OA HUYU BIBIE
 
Back
Top Bottom