Girlfriend wangu kanitumia hela bila kumuomba

Girlfriend wangu kanitumia hela bila kumuomba

nisiwachoshe, ni hivi wakati nam approach mwaka 2011 tukiwa chuo alikua na jamaa yake ambaye hatukua nae chuoni, ila kwasababu mimi ni king`ang`anizi sana ilifika mahali akanikubali, jamaa akipiga simu nikiwa nae nakaa kimya wanaongea, akikata tunaendelea kufanya yetu.

Nilivyomaliza undergraduate degree mwaka 2012 yeye akaenda chuo kingine (sitakitaja) kuendelea na degree couse chuo nilichokua nae yeye alikua anasoma diploma.

Ni mzuri sana kwa kweli, mzuri kila idara, nilikua nikisifiwa na watu hadi mabinti wenzie kila nilikopita nae hali iliyonifanya nimpende zaidi ukiachilia mbali na upole, ucha mungu na ukarimu wake, kwa kifupi alikua na sifa za kuitwa mke, hata aliponishauri niliona tija kwenye ushauri wake.

Sasa wakati yupo hiko chuo alichoenda kujiendeleza tukiwa na mawasiliano mazuri tu, kuna siku yule jamaa yake alimtembelea akanishtukia kwamba natoka nae, akanipigia kwa no ya huyo msichana na kujitambulisha kisha kuniuliza ila nikakana katakata na kumwambia sisi ni marafiki na namfahamu yeye kama shem wangu, jamaa akafurahi sana!

Baada ya two days msichana akanipigia na kunishukuru huku akinishangaa kwa kumjibu jamaa vile. Siku mind couse jamaa alinitangulia kwamsichana alinieleza bayana.

Baada ya hapo tukawa na mawasiliano ya kawaida. Siku isiyo na jina msichana akanipigia analia, kumbe kagombana na jamaa vikali baada ya kumshauri jamaa wanunue kiwanja kwa hela ya mkopo aliyochukua huku jamaa akipinga na kutaka gari.

Nikamtuliza sana, akawa daily ananipigia. Huku na kule akaniomba msamaha akinisihi turudiane, kwasababu nilikua nampenda nikakubali wkt huo nikaweka spy chuoni kwao amchunguze, ikawa inasemekana ametulia ingawa anasumbuliwa sana.

Juzi kati wakati yuko field akaja kwangu, nikakaa nae for two weeks, akanitambulisha kwa mama yake ingawa ni kwa njia ya simu na mimi nikamtambulisha kwa wazee wangu live na wakampokea. Akanishauri tutafute kiwanja na yeye atachangia hela, tena tutafute mkoa nitakaopenda kuishi mimi.

Akarudi zake field, shirika alilokua anafanya field likampa afanye programme flani maalum kutokana na ufanisi wake kazini na wakamlipa laki kila siku for 10 consecutive days.

Cha kushangaza sasa, jana kanitumia laki nne bila kumuomba, nimepigwa na butwaa kwani hii sio kawaida kwa mabinti wa karne hii, eti jamani mkihusianisha na scenario niliyowapa, hapa kuna mapenzi.
nawempe. Ngoma
 
Amicus_Curiae mie ninakushauri hiyo pesa ichukue na uende nae mdogo mdogo tusiendeleze mahusiano yetu kwa kufuata reference za watu ilihali kila mtu ana tabia tofauti kutokana na maingira aliyokulia yeye. Hivyo kabla ya kutaka kumfikiria vibaya huyo msichana embu jaribu kumpa muda kidogo na mwisho wa siku lazima pumba zitajitenga zenyewe na mchele kubaki wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Vyuo vya siku hizi hazina tofauti na jumba la big brother maana ni ngono pekee iliyotamalaki......bora serikali hizo hela za mikopo wawape wajasiliamali..........
 
Cha kushangaza sasa, jana kanitumia laki nne bila kumuomba, nimepigwa na butwaa kwani hii sio kawaida kwa mabinti wa karne hii, eti jamani mkihusianisha na scenario niliyowapa, hapa kuna mapenzi.

Waisome akina Lady Ra, Da Asia, atoto, Da Pretty, Apologise lady, Baby is Mad

Nakala kwa MeinKempf, KikulachoChako, grafani11, Innocizy, immigrant, minuz kwa taarifa.

Cross reference: https://www.jamiiforums.com/mahusia...huu-ni-waraka-wangu-kwenu-marioo-wote-15.html
 
Ukitaka jibu la mtihani .. Bila woga na kama chizi mpigie simu yule shemeji yako wa uongo na umwambie huyo bint amelalamika kwako kuwa wamegombana na pia kwa sasa yuko free..hana boyfriend etc... Then angalia reaction ya bint... akifurahia hatua hiyo unaweza songa mbele.. akikasirika basi huna chako..rudisha hela..

Mmmmh huu kweli mtihani khaaaa!
 
Back
Top Bottom