Girlfriend wangu kanitumia hela bila kumuomba

Girlfriend wangu kanitumia hela bila kumuomba

nunua kiwanja ila ujue huyo si wako peke tako. napia wewe ulupora kwa mwenzako hivo ukae ukijua hilo
 
nilikua nasita kwel bofya huu uzi... Cjui why nimeufungua
 
Mrudishie hela hiyo haraka,maana mzinga utakao kuja ukizitumia itakuwa mara 5 ya hizo!

Jinsia hii kwenye kuona jinsi ya kuvuta mpunga huwa wanaona mbali kuliko jinsia yetu

kweli kabisa! nilishawahi kudate na kigogo flan hivi sasa siku y kwanza tulipoamka asubuhi akanipa hela akati ananirudisha home! Nikampiga nazo usoni kwamba akome mi si changudoa! Akati hapo nna njaa mbaya!
Alivoondoka nikaanza kujutia zile hela! Lols yule mbaba alianza kuchukua responsibilities kubwa kubwa mara elf ya ile hela na ndiyo aliyenitoa kimaisha...

Alinipenda akiamini ni mwanamke nisiyependa hela kuuumbe mweh!
 
Hujafunguka vizuri kuhusu yule uliyemwita shem au yule aliyekutangulia bado wako pamoja?
 
Hapa JF ni mwanamke gani yuko bikira au ni mwanaume gani ana mpenzi na kamkuta ni bikira au nyie wanaume mnaokandia huyo binti kuwa na waume wawili nani hachepuki. Mimi kutokana na maelezo ya kijana huyu ni kwamba yule binti kweli alikuwa na mpenzi wake wa awali ila alikuwa hajielewi na mpenzi wake huyo, ila kaja kwa huyu mtoa uzi kakuta kweli kuna mapenzi ya kweli.
Kwa hiyo kutokana na maelezo ni kwamba kweli kagundua alifanya makosa na hataki kurudia tena. Ameamua awe na mmoja na si mwingine bali huyu mtoa mada. Na ndiyo maana amejitoa amejitoa muhanga na kumtambulisha kwa mama yake na kijana kafanya vizuri kamtambulisha kwa wazazi. Cha muhimu kwa kuwa huyo dada anapenda maendeleo na ambacho wanaume wengi tunaombea tupate wanawake kama hao, hizo pesa azipokee ila amawambie mbona amemtumia badala ya kiwanja? Labda dada ana pesa nyingine na wewe basi mwanaume jikamue utoe nyingine mnunue kiwanja mjenge hata kama si kukaa mpangishe. Huyo ndiye mke material ukizubaa utakuja kukutana na mwingine mpenda maraha na utaishia kupigiwa kila siku
Akili za baadhi wanaume wakati mwingine sijui zikoje, yaani wewe unajisifu kabisa na kumuona huyo mwanamke ni mwaminifu mtu anayewachanga wanaume wawili, nyie wawili mnajuana je hao wenzenu msiowajua??????? Dah!! eti akatitambulisha kwa mama yake na mimi nikamtambulisha wazazi wangu, are you serious????????? Hata pesa alizokutumia ni hongo kutoka kwa boss wa hapo anapofanya field, mmnasikitisha sana. kutwa mnashinda kulalamika wanawake sio waaminifu wakati nyie wenyewe ndio mnatengeza kamtandao CHUKUA HATUA JITOE KWENYE MTANDAO!!!!!!
 
Nisiwachoshe, Ni hivi wakati nam approach mwaka 2011 tukiwa Chuo alikua na jamaa yake ambaye hatukua nae chuoni, ila kwasababu mimi ni king`ang`anizi sana ilifika mahali akanikubali, jamaa akipiga simu nikiwa nae nakaa kimya wanaongea, akikata tunaendelea kufanya yetu.

Nilivyomaliza undergraduate degree Mwaka 2012 yeye akaenda Chuo kingine (sitakitaja) kuendelea na degree couse chuo nilichokua nae yeye alikua anasoma diploma.

Ni mzuri sana kwa kweli, mzuri kila idara, nilikua nikisifiwa na watu hadi mabinti wenzie kila nilikopita nae hali iliyonifanya nimpende zaidi ukiachilia mbali na upole, ucha Mungu na ukarimu wake, kwa kifupi alikua na sifa za kuitwa mke, hata aliponishauri niliona tija kwenye ushauri wake.

Sasa wakati yupo hiko chuo alichoenda kujiendeleza tukiwa na mawasiliano mazuri tu, kuna siku yule jamaa yake alimtembelea akanishtukia kwamba natoka nae, akanipigia kwa no ya huyo msichana na kujitambulisha kisha kuniuliza ila nikakana katakata na kumwambia sisi ni marafiki na namfahamu yeye kama shem wangu, jamaa akafurahi sana!

Baada ya two days msichana akanipigia na kunishukuru huku akinishangaa kwa kumjibu jamaa vile. Siku mind couse jamaa alinitangulia kwamsichana alinieleza bayana.

Baada ya hapo tukawa na mawasiliano ya kawaida. Siku isiyo na jina msichana akanipigia analia, kumbe kagombana na jamaa vikali baada ya kumshauri jamaa wanunue kiwanja kwa hela ya mkopo aliyochukua huku jamaa akipinga na kutaka gari.

Nikamtuliza sana, akawa daily ananipigia. Huku na kule akaniomba msamaha akinisihi turudiane, kwasababu nilikua nampenda nikakubali wkt huo nikaweka spy chuoni kwao amchunguze, ikawa inasemekana ametulia ingawa anasumbuliwa sana.

Juzi kati wakati yuko field akaja kwangu, nikakaa nae for two weeks, akanitambulisha kwa mama yake ingawa ni kwa njia ya simu na mimi nikamtambulisha kwa wazee wangu live na wakampokea. Akanishauri tutafute kiwanja na yeye atachangia hela, tena tutafute mkoa nitakaopenda kuishi mimi.

Akarudi zake field, shirika alilokua anafanya field likampa afanye programme flani maalum kutokana na ufanisi wake kazini na wakamlipa laki kila siku for 10 consecutive days.

Cha kushangaza sasa, jana kanitumia laki nne bila kumuomba, nimepigwa na butwaa kwani hii sio kawaida kwa mabinti wa karne hii, eti jamani mkihusianisha na scenario niliyowapa, hapa kuna mapenzi.

Mbona alishakwambia atachangia kiwanja? huo ndo mchango wake wewe tafuta kiwanja kisha mjulishe kiwanja umepata mkoa ipi, period.
 
sifa ya mwanamke akishajua kuwa mwanaume mbeleni atakuwa ana future nzuri ya maisha basi atakufanyia kila jambo zuri ikiwemo pesa nk lakini hivyo vitu vyote alivyokugharamia vitarudi mkiingia ndoani,KUNA MSEMO UNASEMA HELA YA MWANAMKE HAILIWI HIVI HIVI JUAKUWA ITARUDI

Kumbe mnajua eeeeeh
 
1.Sion kama kama ni.muaminifu kama unavyojaribu kumpigia debe,kwa sababu kama aliweza kutokuwa muaminifu kwa jamaa ake wa awali na akakukubalia wewe,maana ake ipo siku atakutana na zaidi yako nae atakusaliti hivyo hivyo,maana tabia ya usaliti ni kama ngozi kuivua haiwezekan na pia malipo ni hapa hapa kwa dunian..
2.Nilichokigundua huyo dem siyo mzuri kama unavyojaribu kujenga hoja za kwenye majarida,zaidi ninachokiona ni kuwa wewe ni mgeni katika mahusiano(mapenz) na bado una mengi yakujifunza.
3.kupewa hela na mwanamke ni jambo la kawaida na yeye kafanya vyema tu,kaweka kama bank hivi maana kesho au kesho kutwa atakuomba mara mbili yake na kwa sababu umeshapokea zake,huwez kataa kutoa...hizo ni mbinu zakivita,ambazo mwanamke mwerevu wa fedha ndo anaweza fanya hivyo
 
Mwananchi, tulichomwambia mtoa mada ni taadahari tu, kwasababu hadi hapo yeye mwenyewe hajui kama huyo mwanamke ameachana tule mwanaume au la, suala la kumtambulisha sio shida, kwani kamtambalisha madhabahuni???? mim hata sababu anayoisema kuwa ndio imemkera kwa huyo bwana mimi hainiingii akilini, yeye nataka kiwanja, mwanaume anataka waanze kununua gari hivi mtu mwenye akili timamu hii peke yake inaweza kuwafanya watu waliokaa kwenye mahusiano zaidi ya miaka 2 waachane kwel???? hapo nitakuwa wa mwisho kuamini, mimi naamin bidada aliwaweka kwenye mizani alichoangalia yeye nani ataonyesha dalili ya kutangaza ndio akampa kipaumbele, anabaki linakuwa fumbo la imani.
 
Vijana wa kiume siku hizi wambea sana na akili ndogo mno. Yaani jambo dogo tu wamekimbilia JF!

You boys, mnatudhalilisha sana wanaume, muwe na akili.
 
kweli kabisa! nilishawahi kudate na kigogo flan hivi sasa siku y kwanza tulipoamka asubuhi akanipa hela akati ananirudisha home! Nikampiga nazo usoni kwamba akome mi si changudoa! Akati hapo nna njaa mbaya!
Alivoondoka nikaanza kujutia zile hela! Lols yule mbaba alianza kuchukua responsibilities kubwa kubwa mara elf ya ile hela na ndiyo aliyenitoa kimaisha...

Alinipenda akiamini ni mwanamke nisiyependa hela kuuumbe mweh!

!
!
Shkamo.
Asanti Sana.
Ulakoze.
 
Back
Top Bottom