Girlfriend wangu kanitumia hela bila kumuomba

Girlfriend wangu kanitumia hela bila kumuomba

dem anakupenda anakuhonga unashangaa.....ok send it back na umwambie wewe sio marioooo...
 
Jiandae Kulipa Zaidi Ya Hzo Lak 4, Huo Mtego Tu. Istoshe Kila Upande Anashaur Mnunue Uwanja Nae. Look Very
 
Yaani we upewe papuchi usishangae, unapewa hela ndo unajifanya kushangaa... Hapana bana... Anatafuta ndoa huyo... Ila jua kwamba ukimuowa huyo mwanamke huyo jamaa mwingine ndo mchepuko wa kudumu..

Mkuu Amicus Curiae refer to the red colour huyu jamaa anaweza akawa anongea ukweli mtupu, kumbuka ukila kuku wa mwenzio miguu lazima itakurudia tu
 
kwahiyo unamaanisha huyu nae ni marioo?

Marioo ndo hupewagwa hela bila kuomba wala kuulizwa na wala kuombwa kupewa....... Enzi zetu tulikuwa tukiulizwa swali kama hili tunajibu... RULAAA HAPOOO
 
Nisiwachoshe, Ni hivi wakati nam approach mwaka 2011 tukiwa Chuo alikua na jamaa yake ambaye hatukua nae chuoni, ila kwasababu mimi ni king`ang`anizi sana ilifika mahali akanikubali, jamaa akipiga simu nikiwa nae nakaa kimya wanaongea, akikata tunaendelea kufanya yetu.

Nilivyomaliza undergraduate degree Mwaka 2012 yeye akaenda Chuo kingine (sitakitaja) kuendelea na degree couse chuo nilichokua nae yeye alikua anasoma diploma.

Ni mzuri sana kwa kweli, mzuri kila idara, nilikua nikisifiwa na watu hadi mabinti wenzie kila nilikopita nae hali iliyonifanya nimpende zaidi ukiachilia mbali na upole, ucha Mungu na ukarimu wake, kwa kifupi alikua na sifa za kuitwa mke, hata aliponishauri niliona tija kwenye ushauri wake.

Sasa wakati yupo hiko chuo alichoenda kujiendeleza tukiwa na mawasiliano mazuri tu, kuna siku yule jamaa yake alimtembelea akanishtukia kwamba natoka nae, akanipigia kwa no ya huyo msichana na kujitambulisha kisha kuniuliza ila nikakana katakata na kumwambia sisi ni marafiki na namfahamu yeye kama shem wangu, jamaa akafurahi sana!

Baada ya two days msichana akanipigia na kunishukuru huku akinishangaa kwa kumjibu jamaa vile. Siku mind couse jamaa alinitangulia kwamsichana alinieleza bayana.

Baada ya hapo tukawa na mawasiliano ya kawaida. Siku isiyo na jina msichana akanipigia analia, kumbe kagombana na jamaa vikali baada ya kumshauri jamaa wanunue kiwanja kwa hela ya mkopo aliyochukua huku jamaa akipinga na kutaka gari.

Nikamtuliza sana, akawa daily ananipigia. Huku na kule akaniomba msamaha akinisihi turudiane, kwasababu nilikua nampenda nikakubali wkt huo nikaweka spy chuoni kwao amchunguze, ikawa inasemekana ametulia ingawa anasumbuliwa sana.

Juzi kati wakati yuko field akaja kwangu, nikakaa nae for two weeks, akanitambulisha kwa mama yake ingawa ni kwa njia ya simu na mimi nikamtambulisha kwa wazee wangu live na wakampokea. Akanishauri tutafute kiwanja na yeye atachangia hela, tena tutafute mkoa nitakaopenda kuishi mimi.

Akarudi zake field, shirika alilokua anafanya field likampa afanye programme flani maalum kutokana na ufanisi wake kazini na wakamlipa laki kila siku for 10 consecutive days.

Cha kushangaza sasa, jana kanitumia laki nne bila kumuomba, nimepigwa na butwaa kwani hii sio kawaida kwa mabinti wa karne hii, eti jamani mkihusianisha na scenario niliyowapa, hapa kuna mapenzi.

Kids! Sioni cha ajabu hapo kwa kweli ila uhoji ni za nini. Ila kama analeta swala la kukuhonga, jaribu kulidiscourage.
 
Anakupenda huyo msichana jaman., halafu anataka mjenge maisha kwa sababu kakuona wewe ndo unafaa kua mshirika wake. Kafanya field kapata hela ya kutosha ndo maana kakupa nawe ufurahie jasho lake., hiv hujiuliz mbona mwanzo hakukupa? Halafu anaakili ya maisha sana na pia amekuamini sana., hivo hufikirii hamjaoana na bado anakwambia mnunue kiwanja kwan yy ameshindwa kununua peke ake? kakuamini,anakupenda na anakujali ndo maana anataka mjenge maisha. Mke mwema anatoka kwa mungu, na mungu kakuletea sasa unatetereka nn? mwanamke mwingne kaolewa na anafanya kaz lkn mume hajawai kushika pesa ya mkewe kwa sababu mwanamke ni nahili kwa hyo nawe unataka mwanamke bahili ili familia uilishe peke ako, ujenge mwenyewe na matatizo yote ya familia na ndugu yote utatue mwenyewe? Mungu kakuonyesha nyota njema mapemaaaaaaa ikumbatie basi usiiache iende utaikumbuka ikipotea. Ndukiiiiiiiiiii
 
Huyo hio pesa kahongwa na boss wake wa hapo anapofanyia field..stuka rafiki wa mahakama na chukua hatua.
 
hapana kwakweli, buku tu naumwa mwezi mzima!

Kuhonga kunategemea na kipato chako...ukiwa unamiliki elfu 10 kutoa buku inakuwa umetoa 1/10...na kama una 8 figure, kutoa milioni inakuwa umetoa asilimia 1..

Hivyo kimahesabu aliotoa buku kahonga zaidi ya alietoa milioni. Upo hapo???
 
Mwanamke ni kichwa sio sura wala umbile huyo kama anakushauri hadi masuala ya msingi ni wa ukweli sio jambazi kama yaliyojazana kitaa hapo cha msingi tuma mshenga kwao weka ndani mfanye maisha hiyo kilo nne nenda nakumati kafanye yako
 
Anakupenda huyo msichana jaman., halafu anataka mjenge maisha kwa sababu kakuona wewe ndo unafaa kua mshirika wake. Kafanya field kapata hela ya kutosha ndo maana kakupa nawe ufurahie jasho lake., hiv hujiuliz mbona mwanzo hakukupa? Halafu anaakili ya maisha sana na pia amekuamini sana., hivo hufikirii hamjaoana na bado anakwambia mnunue kiwanja kwan yy ameshindwa kununua peke ake? kakuamini,anakupenda na anakujali ndo maana anataka mjenge maisha. Mke mwema anatoka kwa mungu, na mungu kakuletea sasa unatetereka nn? mwanamke mwingne kaolewa na anafanya kaz lkn mume hajawai kushika pesa ya mkewe kwa sababu mwanamke ni nahili kwa hyo nawe unataka mwanamke bahili ili familia uilishe peke ako, ujenge mwenyewe na matatizo yote ya familia na ndugu yote utatue mwenyewe? Mungu kakuonyesha nyota njema mapemaaaaaaa ikumbatie basi usiiache iende utaikumbuka ikipotea. Ndukiiiiiiiiiii

Maneno mazuri mno haya yenye kutia moyo. Asante mkuu!
 
Mwanamke ni kichwa sio sura wala umbile huyo kama anakushauri hadi masuala ya msingi ni wa ukweli sio jambazi kama yaliyojazana kitaa hapo cha msingi tuma mshenga kwao weka ndani mfanye maisha hiyo kilo nne nenda nakumati kafanye yako

Maneno ya mbolea sana haya!
 
Back
Top Bottom