Gharib Bilal ateuliwa mgombea mwenza wa Kikwete 2010

bwana wee-hakuna msafi na kila mtu ana uzuri na mabaya yake-kuliko hamuweke meghji haki yanai mimi ningekufa kwa pressure-bora huyo bilal mara mia. Maana bora yule ujuaye mambaya yake kuliko yule amabayo hatuyajui.Ongera zake-mzee walimuhaodi saana na ankubalika.Kazi anaweza kufanya.Ujue kila mtu ana nafasi ya kujifunza na kujirekebisha kupitia mabaya yake. Lkn uteuzi huu ni suprise!!
 
mZEE Shein akabidhi ule mKASI wake kwa Gharibu wazeenj wakati mwingine huniacha hoi!
 
Kumbe kutishia nyau kunalipa Lowassa naye yuko wapi ajaribu kutikisa kiberiti tuone maana naona JK ni kama pazia vile upepo ukija linafunuka, anapelekwa asikotaka.

Kama changes zinafanyika mwishoni mwishoni kutokana na upepo unavyovuma naona uongozi wa taifa hauna long term plan ni weupe kabisa tofauti na enzi za Mchonga ambaye katika uongozi alikuwa na msimamo lije jua ije mvua habadiliki.
 
Duh! Kikwete anaendelea kutu-disappoint huyu jamaa hafai kabisa. Alimteua Lowasa kwa urafiki, akamteua Shein kwa kulazimishwa na CC sasa kateua Bilal ili kumpoza. Jamaa yupo weak mno!

Mkuu wewe fanya tu shughuli zako kwa bidii na kwa uaminifu lakini kwa JK usitegemee chochote cha maana.
 
we ngoja aanze kula misambusa na misoseji ya ikulu atanona sasa hivi


....sidhani labda kuchoka ni umbile tu....maana pia hatujuwi mfumo wa mafao kwa rais mstaafu wa zanzibar au waziri kiongozi unakuwaje....kuna mawaziri kiongozi kama brig.faki..sidhani kama ana maisha mazuri sana...kama Salmini mwenyewe kuna wakati alikosa kulipiwa hata bill ya umeme ..ukakatwa ..na ikafikia hata akakosa gari ....ikabidi aazime gari la shirika la umma zanzibar.......
kama hatutakuwa na mfumo bora wa mafao itawalazimu mawaziri viongozi zanzibar waendelee kuutafuta urais kwa udi na uvumba kwa kuhofia mustakaba wao baada ya kutoka madarakani....na marais kama mfumo wa mafao sio straight forward watabaki wakitamani kuongezewa muda au kutaka kuweka wafuasi wao....
Serikali ya muungano naona mfumo wao wa mafao uko kikatiba na hauna upendeleo ndio maana mawaziri wastaafu wote .....wamestaafu na kutulizana wanakula pension..na hatujapata kusikia malalamiko awe salim,warioba,msuya,malecela,..sumaye na hata marehemu kawawa...

nadhani mtu kama Nahodha he is too young to retire and will soon find himself idle...unless nayeye achukuwe uamuzi wa kwenda kusoma kama Sumaye ...akijipanga kwa mwaka 2025..he will be 58 by then ......na akirudi na nguvu mpya anaweza kuambulia urais wa zanzibar au hata umakamu wa rais ....kama sera za rais atakayekuja zitaendelea kuwa za kupoozana!!!!
 
Hapa hatuna mtu, tulishakuwa watoto yatima. Wadau tujitokeze kugombea tubadilishe huu mfumo wa kubebana bila kuangalia maslahi ya taifa kwa ujumla
 
To be fair, Dr. Mohammed Billah, has been Permanent Secretrary for Ministry of Higher Learning... during when Mkapa was the minister, This guy has been Waziri Kiongozi... and prepared for several years to at least be president in Zanzibar.

I'm sure he is good leader as VC... and he is a guy who can lead the country in case....

Though I don't like the way running mate is being elected/appointed!!! There is policy problem within CCM and with Election Act.
 
To be fair, Dr. Mohammed Billah, has been Permanent Secretrary for Ministry of Higher Learning... during when Mkapa was the minister, This guy has been Waziri Kiongozi... and prepared for several years to at least be president in Zanzibar.

I'm sure he is good leader as VC... and he is a guy who can lead the country in case....

Though I don't like the way running mate is being elected/appointed!!! There is policy problem within CCM and with Election Act.


Mkuu you are saying Ghalib Bilal would make a god VP and in the unfortunate event would also make a good president. At the same time you don't like the system which chose him to be the running mate. Are you saying that a bad system........can produce a good leader sometimes?
 
Mbona majina yote mnayopendekeza ni waislamu tu?

Mkuu usiingize kile kisicho kuwepo. What's wrong with you? Raisi akitoka Bara lazima makamo atoke visiwani, visiwani ina julikana kabisa 99% ni Waislamu kwa hiyo hapo cha ajabu ni nini? Haya basi wewe pendekeza kiongozi Mzanzibari hata mmoja unaye mjua wewe ana weza kuwa makamo wa raisi na ni Mkristo. I'm a Christian but I hate when religion is put into politics.
 
A: Muhammed Seif Khatib
B: Shamsi Vuai Nahodha
C: Zakia Meghji
D: None of the above

And the answer is [ D ] substantiate your answer.

CONFIRMED:

Gharibu Bilal ameteuliwa rasmi kuwa mgombea mwenza wa Kikwete

Mkuu, mimi nilijua kuwa kinachofanyika hapo ni swap, kwani Bilal 2000 walimtosa, 2005 wakamwambia atoe jina kutokana na mchuano kuwa mkali kati yake na Shein ni dhahiri ili kuleta umoja ni JK alikuwa hana chaguo lingine zaidi ya Bilal.

https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-mkutano-mkuu-wa-ccm-dodoma-6.html#post984110
 
Heeh..bora tungemjaribu pweza atutabirie,ha ha!..Haya tumsubiri tu awe VP mana kelele nyingi lakini JK anapita 2nd term!
 
Back
Top Bottom