Gharib Bilal ateuliwa mgombea mwenza wa Kikwete 2010

....sidhani labda kuchoka ni umbile tu....maana pia hatujuwi mfumo wa mafao kwa rais mstaafu wa zanzibar au waziri kiongozi unakuwaje....kuna mawaziri kiongozi kama brig.faki..sidhani kama ana maisha mazuri sana...kama Salmini mwenyewe kuna wakati alikosa kulipiwa hata bill ya umeme ..ukakatwa ..na ikafikia hata akakosa gari ....ikabidi aazime gari la shirika la umma zanzibar.......
kama hatutakuwa na mfumo bora wa mafao itawalazimu mawaziri viongozi zanzibar waendelee kuutafuta urais kwa udi na uvumba kwa kuhofia mustakaba wao baada ya kutoka madarakani....na marais kama mfumo wa mafao sio straight forward watabaki wakitamani kuongezewa muda au kutaka kuweka wafuasi wao....
Serikali ya muungano naona mfumo wao wa mafao uko kikatiba na hauna upendeleo ndio maana mawaziri wastaafu wote .....wamestaafu na kutulizana wanakula pension..na hatujapata kusikia malalamiko awe salim,warioba,msuya,malecela,..sumaye na hata marehemu kawawa...

nadhani mtu kama Nahodha he is too young to retire and will soon find himself idle...unless nayeye achukuwe uamuzi wa kwenda kusoma kama Sumaye ...akijipanga kwa mwaka 2025..he will be 58 by then ......na akirudi na nguvu mpya anaweza kuambulia urais wa zanzibar au hata umakamu wa rais ....kama sera za rais atakayekuja zitaendelea kuwa za kupoozana!!!!

Nahodha ameshaambiwa kuna kazi nyingi za kufanya, nadhani anaweza akapewa Waziri wa mambo ya nje
 
Akileta mauzauza Mungu atampiga chini, kama unabisha muulize Sauli bwana, Mungu alivyomkataa ok aliendelea kuongoza nchi lakini kumbe alishakataliwa na Mungu siku nyingi, hao wengine washakataliwa wanashupaza shingo tu :twitch:
 
I don't think it can be Shamsi Vuai Nahodha. If he was being prepared to be VP he would have known it by now and not bothered to run in Zanzibar. I don't think he is that important to the CCM establishment or Kikwete's goals to be given the consolation prize of VP.

*From what I know Kikwete had a running mate prepared for 2005 but was forced to keep Shain in his ticket. I don;t know who his choice was but common sense tells me that he is probably going with that person this time around.


What makes you think he wasnt "forced" to keep Bilal on his ticket THIS TIME?

Bro, soma alama za nyakati. Hakuwa na jinsi... angemuacha angekiona cha mtema kuni!

Si-hasa si makida-makida au rede!

./Mwana wa Haki
 
What a disaster?! Siasa ya Tanzania kama mchezo wa mwanasesere. Sasa tunatoka ICU tunaelekea mochwari ndoto za maendeleo Tz. ni hadithi simulizi. Mimi nitaukataa Utanzania kuanzia sasa nilikuwa nafikiri kutakuwa na kaahueni kidogo lakini kwa mtindo huu we are finisheeeeed!
 
Tetesi kutoka huku ndani kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma ni kuwa wazee wa chama wamemshauri Kikwete amteuwe Dr Gharib Billal kuwa mgombea mwenza wake. Lengo ni kumpooza baada ya kutoswa kwenye Urais wa Zanzibar. Dr Shein is a weak candidate na bila support ya kundi la Billal hawezi kumshinda Seif Shariff Hamad wa CUF kwenye uchaguzi. Kuna hofu kuwa Billal, ambaye alikuwa anaungwa mkono na mafisadi Edward Lowassa na Rostam Aziz anaweza kuhamia chama cha Jahazi kugombea Urais Zanzibar na hivyo kuwa ni kiama kwa CCM. Kikwete anasemekana kupendelea kumteuwa mkwe wake Zakia Meghji awe VP ili aache legacy ya kuteuwa makamu wa rais wa kwanza mwanamke.
Nitawapa taarifa zaidi ili kujua ni nini kinaendelea punde habari zitakavyo vuja kwenye hiki kikaao.
Chaguo la kikwete la running mate mwaka 2005 alikuwa ni Mohamed Seif Khatib, naye anatajwa pamoja na Rais Karume.
Tatizo ni kuwa Karume anaonekana kuwa ni jeuri na hakumhusisha JK kwenye makubaliano yake ya siri na CUF.

naomba nisaidiwe kuelimishwa, hatuna sheria yoyote inayombana rahisi kuchagua VP maana hapa naona rais ana uwezo wa kumchagua hata shemeji yake lol..
 
Kwa taarifa yenu tu ,iwapo CUF itachukua madaraka ya Zanzibar ,basi haumalizi mwaka makamo wa Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar atakuwa ni alie Raisi wa Zanzibar na si vinginevyo ,pia iwapo Shein atashinda Uchaguzi wa Zanzibar bado posibility ya yeye kuwezeshwa kuwa ni Makamo wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ,itasogezwa na kuwa issue ya kero za muungano nambari moja.

Mambo ya kuokota watu na kuwafanya kuwa makamo wa Rais hayo hayakubaliki katika siasa za Zanzibar na popote pale ,penye muungano wa nchi mbili au zaidi.

Yaani kwa kuwa wewe ni mgombea basi unaokota mutu yeyote yule eti mwenza ! mke au mume ? na kumpa post ya umakamo wa Raisi .aloo ,wamesoma lakini siwakujua !!
 
Mwana JF,
Huyu Dr. M.G.Billal ni msomi na sio Docta wa mifugo kama hawa waliomtanguliwa au JK aliyerushiwa Taulo, CV yake kitaaluma imekaa sawa. Ila hee ni mbabe wa kupindukia, jeuri ya shule, mbaguzi, uzanzibari, udini, n.k.

Ngoja niwape kidogo. Akiwa katibu mkuu wizara ya Sayansi na Elimu ya juu na Ben. Mkapa akiwa waziri mambo yalikuwa hayaendi kwani anachosema waziri akija katibu anapinga mbele yake na maneno ya kejeli. Nikiwa mmojawapo wa deligate iliyokuwa inashughulikia madai mbali mbali ya wanafunzi wa UDSM tulikuwa tunaenda wizarani kukutana na hawa watu, nakumbuka 1994 May, wanafunzi wa OFF COMPUS walikuwa wanadai malimbikizo yao ya OFF COMPUS allowance na wliahidiwa na Waziri kuwa malipo yatafanyika mchana kitu ambacho hakikuwa na kesho yake wanafunzi wakarudi kufuatilia ambapo Waziri alisema hebu nikamuulize Katibu kwani haikuwa effected. Jibu mbele yangu "Nani kasema kuna pesa ya kulipa? Mtendaji ni mimi achana na huyu mwanasiasa, nasema pesa hakuna, serikali haina pesa. Nenda kawaeleze wenzeni" Waziri (Ben) alikasirika na kusema "Anayetaka kusoma asome asiyetaka aache siwezi kutukanwa as if pesa napeleka kwenye familia yangu na muelewe serikali ya sasa hivii ni ya WAZANZIBAR, nawaruhusu fanya mnachoona kinafaa" Mwisho wa siku hiyo eneo la Wizara lilikuwa halitamaniki kwa virungu vya FFU. Ushahidi muulize RUGEMEREZA NSHALA, (Wakili) na wengine walioishia kulazwa muhimbili kwa kipigo nje ya ofisi ya Billal. Sio hapo tu, Prof. Mahalu (Director working with Billal by then) alifukuzwa ofisini kwa Katibu akiwa anafuatilia majina ya scolarship yaliyobadilishwa kutoa wa Bara na kuweka wazanzibar. TUMEKUFA OIC, UDINI, UBAGUZI, n.k. VIPO MLANGONI.
Kenge (Eng)

Umesema ukweli huyu mtu kiburi kinamtesa sana, ni kweli wakati akiwa katibu wa elimu ya juu alikuwa akikata hata ushauri wa Mkapa wakati huo waziri. Nakumbuka siku moja tilienda pale wizarani Jamhuri street Bilal akakataa kuteremka kuongea na wanafunzi, akaita FFU wakatuzingira pande zote za barabara.

Wanafunzi wote tukaa chini barabarani kuonyesha hatukuridhika, katika kututuliza ikabidi FFU wamuombe Bilal kwa kumpigia magoti aje kuongea na sisi akateremshwa chini ya ulinzi wa polisi, alipofika chini akasema sentesi ambayo bado naikumbuka 'Nimesema serikali haina hela anayetaka kusoma arudi chuoni asiyetaka aende nyumbani' akapanda gari akaondoka nafikiri unaweza kubashiri kilichofuata chini ya FFU.

Tunapojaribu kuelezea utendaji wa Dr. Bilal uliopita si kwamba tunapinga uteuzi wake au tutabadilisha kitu la, ila tunajaribu kuonyesha jamii ya watanzania ni kiongozi gani na uongozi gani tuutegemee kutoka kwa huyu mtu. Ni kiburi, jeuri, na dharau.
 
Nasikia mzee ni m'binafsi sana... Lakini tusubiri maana binadamu haweshi kubadilika.
 
..miaka ile kila Mzanzibari alikuwa na kiburi na kejeli dhidi ya Watanganyika.
 
Wakuu...tunaomba CV ya huyu bwana aliyeteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Kikwete kwa kupitia tiketi ya CCM! Sijui ni wangapi humu wanamfahamu...maana mimi ndo kwanza namsikia!

natanguliza shukrani!
 
bora wangemchagua John mashaka walahiiii.....hicho kibabu bilal kishajikongorokea sijui cha kazi gani? :twitch:
 
Huyo ni mtu wa hasira na nongwa au chuki ,ukimtizama anaweza kuona kuwa unamchukia.
 
hali yake ya kifedha ilikuwa mbaya sana angalau afya itarudi kidogo sasa.
 
Huyu babu kachoka kwa kweli....Sikuwahi muona hapo awali ndiio namuona this time alipochaguliwa...ata meno labda yatakuwa yameshapungua mdomoni...la nimeangalia kwenye google na wikipendia sio CV yake...kama wasomi wenzie.

So sijui kasomea wapi huyu.
 
Back
Top Bottom