GHARAMA ZA UENDESHAJI WA GARI - APRIL 2012.
Watu wengi wemekuwa na mtazamo kwamba gharama ya uendeshaji wa gari linapotembea ni mafuta yanayotumika tu.
Gharama za uendeshaji wa gari zimegawanyika katika makundi 2:
Gharama za uendeshaji wa gari zimegawanyika katika makundi 2:
1. GHARAMA ZA LAZIMA (Fixed Cost):
- Gharama hizi hufanyika kwa mwaka:
- Leseni ya barabarani (Road License) = Tsh. 100,000/=
- Bima (third part insurance) = Tsh. 50,000/=
- Ukaguzi wa gari = Tsh. 5,000/=
- Zimamoto (Fire Sticker) = Tsh. 5,000/=
JUMLA = Tsh. 160,000/= (kwa mwaka)
KWA SIKU = Tsh. 444.44 ~ Tsh. 500/=
2. GHARAMA ZITOKANAZO NA GARI KUTEMBEA (Running Cost):
Gharama hizi zinatokana na gari kutembea, ambapo tunaweza kuangalia kwa kila kilomita (1), inagharimu kiasi gani:
- Mafuta - Magari mengi utumiaji wa mafuta ni lita 1 kwa mwendo wa kilomita 10 - 14, inategemea na aina ya gari. Hivyo basi makadirio nitafanya kwa gari linalotumia lita 1 kwa kilomita 10. Bei ya Petrol kwa sasa ni Tsh. 2290/= kwa lita, Hivyo basi kwa kila kilomita 1 = Tsh. 229/= ~ Tsh. 230/=
- Matengenezo (Service) - Hii hufanyika gari baada ya kutembea takribani kilomita 4000. Gari inahitaji kubadilishwa engine oil n.k. Gharama za matengenezo haya hufikia takribani Tsh.100,000/=. Hivyo basi kwa kila kilomita 1 = Tsh 25/=
- Uchakavu (ware-out) - Gari linapotembea vipuri mbalimbali huanza kusagika/kuharibika yakiwemo matairi. Gharama hizi zinaweza kukadiriwa Tsh. 500/= kwa kilomita.
JUMLA KWA KILOMITA = Tsh. 755/=
Hivyo basi gari likitembea kilomita 10 = Tsh 7,550/= (Gharama za kutembea gari tu) + Gharama ya lazima ya siku = 500/=, itakuwa Jumla ni Tsh. 8,550/=
NB: Kwa gari ya biashara (TAXI)
>> Utahitaji malipo ya dereva kwa siku = Tsh. 10,000/=
>> Kodi
Kumbuka biashara yeyote inapaswa kupata faida isiyopungua asilimia 15% kutokana na malipo ya huduma/bidhaa.
TUNAWEZA KUPATA UWIANO WA GHARAMA ZA UENDESHAJI NA MALIPO YANAYOFANYIKA KWA HUDUMA YA TAXI NA KUANGALIA KAMA NI BIASHARA INAYOLIPA?
KWA MTAZAMO MWINGINE:
- Kuna umuhimu wa kila Mtanzania kumiliki gari (baba na mama kila mmoja gari lake, watoto n.k), hivi tunajiuliza gharama kabla...!!!
- Kwa nini tusiboreshe huduma za usafiri wa jamii (public transport) kuokoa fedha tunazotumia kila siku kuendesha magari.
MCHANGO ZAIDI UNAWEZA KUTOLEWA KATIKA GHARAMA ZA UENDESHAJI GARI..........!!!!!