Gharama za uchaguzi wa kenya zatisha

Gharama za uchaguzi wa kenya zatisha

Morick

Senior Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
114
Reaction score
17
Gharama za uchaguzi mkuu wa kenya zafikia Tsh tilion 20 sawa na makusanyo ya kodi ya Tanzania ya miaka mitatu mfululizo. Hii inatufundisha nini kwa nchi zetu za Kiafrika? Nawasilisha
Source: Tbc1 uchaguzi mkuu kenya live
 
Na pia kutokana na katiba yao inavyosema ni kua endapo mgombea wa Uraisi kama hatapata ushindi wa kura wa asilimia 50+1 uchaguzi utarudiwa:A S 39:
 
Acha wewe, 20Trilion sio hela ndogo aisee, Mji wao wanaokusudia kuujenga haufikii hela hiyo.
 
20tril siyo mchezo labda kama sijasikia vizuri.

Hata mi nilijiuliza sana kuhusu ukubwa wa fedha hii lakin mtangazaji alipoendelea kuhoji aliambiwa wakenya wamefanya hivyo ili kuwekeza katk suala la amani kuliko kujirudia ya 2007
 
Well! Kwa source yako hiyo ya habari, asante na kwaheri!
 
TBC ni kama gazeti la Uhuru, huwezi kutumia kama chanzo cha habari. Watangazaji wake na wafanyakazi wake wengi walioko huko wapo kama hawapo.

Gharama za uchaguzi mkuu wa kenya zafikia Tsh tilion 20 sawa na makusanyo ya kodi ya Tanzania ya miaka mitatu mfululizo. Hii inatufundisha nini kwa nchi zetu za Kiafrika? Nawasilisha
Source: Tbc1 uchaguzi mkuu kenya live
 
Yule mtangazaji wa TBC Marin Hasan hajui alichokiongea, wakati namwangalia nilimshangaa sana. Gharama za kuandaa hivyo vifaa ni dola Mil 180 ambazo ni kama Bilion 20 na zaidi za kitanzania na sio trilion 20 kama alivyopotosha watu
Duh! Mgodi wa Buzwagi una thamani ya mill 300 dola, sasa si bora wangetafuta kilichobakia wakawekeza kwenye mgodi mkubwa kama Buzwagi huko kwao ungewatoa sana kiuchumi, kuliko kupoteza hela kwanye takataka!
 
It is billion not trilion. Remember democracy is expensive. Try the cost of no democracy.
 
It is billion not trilion. Remember democracy is expensive. Try the cost of no democracy.

Hakuna Demokrasia Afrika, na haitakuwepo hata kwa miaka 300 ijayo! Hivyo hizi chaguzi ni kupoteza pesa tu, wangeweza kutumia hizo pesa kuwekeza kwenye kuchimba Mafuta huko Turkana badala ya kuwapa makampuni ya Wazungu ambao wataiba mafuta yote!
 
Hata mi nilijiuliza sana kuhusu ukubwa wa fedha hii lakin mtangazaji alipoendelea kuhoji aliambiwa wakenya wamefanya hivyo ili kuwekeza katk suala la amani kuliko kujirudia ya 2007
wamewekeza kwenye amani gani sasa wakati usiku wa kuamkia leo karibu askari 17 wameuawa huko mombasa.
 
Gharama za uchaguzi mkuu wa kenya zafikia Tsh tilion 20 sawa na makusanyo ya kodi ya Tanzania ya miaka mitatu mfululizo. Hii inatufundisha nini kwa nchi zetu za Kiafrika? Nawasilisha
Source: Tbc1 uchaguzi mkuu kenya live

wewe na marine wako wote wanafiki wakubwa. Mmeongelea ya Tanzania mmeona hakuna anayewajali na sasa mmehamia Kenya. Mbona wakenya wenyewe hawalalamiki? Hata kama ni trioni 20, kubwa ukilinganisha na nini. Mbona hujaweka budget yao kwa mwaka huu ni sh. ngapi? mbona hujaweka pato lao la mwaka ni kiasi gani? Mbona hujaweka vipaumbele vyao vya taifa ni vipi?

Kwa taarifa yako Tume ya Uchaguzi ya Kenya imetengewa dola milioni 206 sawa na shilingi za kenya bilioni 17.5. Huyo Marine hata kama alitamka bilioni 20 kwa maana ya" approximate" amechemsha. Ku approximate bilioni 2.5 ni kubwa mno
 
The cost of the March 4 General Election will be Sh24.9 billion, three times that of the last poll, the Finance ministry has revealed in a document tabled in Parliament.

The bulk of this cost was for the procurement of the biometric voter registration kits (Sh6.6 billion), recruitment and remuneration of election officials (Sh4.8 billion) and procurement of election materials and equipment (Sh3.8 billion).

The defunct Electoral Commission of Kenya spent Sh8 billion to organise the last General Election in 2007.

MY TAKE:
Kweli waandishi wetu vilaza hawajuhi hata rate za exchange ?

24.9 Bil Kshs kwa rate ya 15 Tshs to 1 Ksh ni sawa na 373.5 Bil Tshs.

ndipo tulipofika katika demokrasia ya afrika wanasiasa wanatumia nguvu kubwa ya pesa kuingia madarakani wakifanikiwa kuingia ikulu wanarudisha pesa zao ni kama aina nyingine ya biashara.
 
Yule mtangazaji wa TBC Marin Hasan hajui alichokiongea, wakati namwangalia nilimshangaa sana. Gharama za kuandaa hivyo vifaa ni dola Mil 180 ambazo ni kama Bilion 20 na zaidi za kitanzania na sio trilion 20 kama alivyopotosha watu
Nadhani alichokuwa anamaanisha ni gharama ambazo wagombea, hasa wagombea urais wamezitumia katika kampeni zao... si gharama ambazo tume ya uchaguzi au serikali imeingia katika kuandaa uchaguzi
 
Ha ha haa TBC wanajua hata wakidanganya hakuna anaegundua! Kumbe kuna ma-GT wanawafuatilia kila wanachofanya.I Love JF
 
Haya makosa ya kuconvert toka hela za kigeni kuja kwenye Tshs ni makubwa sana hasa kwenye magazeti mara nyingine unajiuliza kama editors wanafanya kazi yao vizuri
 
Nadhani alichokuwa anamaanisha ni gharama ambazo wagombea, hasa wagombea urais wamezitumia katika kampeni zao... si gharama ambazo tume ya uchaguzi au serikali imeingia katika kuandaa uchaguzi

Hawezekani hata useme vipin yani kampeni ya miezi mitatu itumie hela zaidi ya Makusanyo ya Kodi ya nchi nzima.
 
Back
Top Bottom