Gharama za kutoa bandarini container la furniture za ndani

queenkami

JF-Expert Member
Feb 8, 2010
1,599
1,025
Habari zenu ndugu zangu.
Naomba mnisaidie nijue gharama na process nzima ya kutoa bandarini container lenye furniture ambazo sio za
biashara.

Najua kutoa gari bandarini ni mtihani ila je kwa container lenye vifaa vya ndani ambavyo sio vya biashara ni rahisi kulitoa au na lenyewe itakua mtihani?

Natanguliza shukrani zangu kwa wote mtakaonisaidia.
 
Container zima limejaa furniture? Iwe la ft 20 or 40 mtihani wa kwanza ni kuwaconvince kuwa sio furniture za biashara, kama kweli zimejaa container. Kwa makadirio cost itacheza kati ya dolla 5000 na 7500.
 
Kodi inatozwa bila kujali unachoingiza ni cha biashara au siyo cha biashara .... kodi hizi ni customs duty @25% and VAT @18% plus other taxes .... bidhaa zingine huwa na special HS codes kama zana za kilimo na pia kuna baadhi ya walipa kodi huwa na misamaha ya kodi (exemption) ... jitayarishe kulipa kodi bila kuangalia bithaa ni kwa ajili ya biashara au matumizi binafsi
 
Thanks mkuu.
Nimesema furniture kwa ujumla ila ni pamoja na vitu vingine vya nyumbani.

Ili uwashawishi sio vya biashara vinatumika vigezo gani?
 
Hizo percentage wanacharge kulinganisha na nini?
Kama je hivyo vitu nimepewa na sina risiti za kuonesha gharama zake,hizo kodi watakataje?
 
Watahitaji invoice ya mzigo. Hata kama kwako siyo biashara lakini wata charge kodi on the value of goods being imported into URT
Kama hivyo vitu ni used itakusumbua maana watahitaji mzigo wote uwe umefanyiwa inspection from country of origin. Muhimu tafuta clearing & forwarding agent mwaminifu afuatilie kwa karibu

NB. Avoid any advice about bending the law
 
Watahitaji invoice ya mzigo. Hata kama kwako siyo biashara lakini wata charge kodi on the value of goods being imported into URT
Kama hivyo vitu ni used itakusumbua maana watahitaji mzigo wote uwe umefanyiwa inspection from country of origin.
Mzigo uwe umefanyiwa inspection na nani?

Value of goods imported according to who? Who determines the value of used furniture?

Watahitaji invoice ya mzigo, furniture zina miaka 7, kwa mfano, utapata wapi invoice ilhali ishasemwa risiti hatuna?
 
Mzigo uwe umefanyiwa inspection na nani?

Value of goods imported according to who? Who determines the value of used furniture?

Watahitaji invoice ya mzigo, furniture zina 7, kwa mfano, utapata wapi invoice ilhali ishasemwa risiti hatuna?

Kama ni used items lazima hizo items ziwe zimefanyiwa inspection na SGS au Intertek au Cotecna tokea huko huko zinakotoka. Yule aliyekutumia alitakiwa awafahamishe inspector na kuwaita wafanye inspection. Kisha wanatoa ripoti direct kwa tawi la Tanzania na TBS. Bila hiyo ripoti utasumbuka sana.

Who determines the value of used furniture- wewe unatakiwa uwe na estimate ya value ya mzigo. Ni vigumu kuji invoice wewe mwenyewe but kumbuka watanzania tunakariri. Wasipo ona invoice waweza kuzungusha pia. Usipokuwa na your own invoice, TRA will estimate but mind you their estimate is going to milk you.
 
Habari zenu ndugu zangu.
Naomba mnisaidie nijue gharama na process nzima ya kutoa bandarini container lenye furniture ambazo sio za
biashara.

Najua kutoa gari bandarini ni mtihani ila je kwa container lenye vifaa vya ndani ambavyo sio vya biashara ni rahisi kulitoa au na lenyewe itakua mtihani?

Natanguliza shukrani zangu kwa wote mtakaonisaidia.

kama ulikuwa unasoma au kufanya kazi nje na hizo zilikuwa ni vifaa vyako na mybe ulikuwa na gari na umekaa huko nje kwa zaid ya mwaka mmoja vifaa ivyo vinaitwa ni personal effects huwa vinamsamaha wa kodi kwa maana huwa avilipiwi kodi zaidi ya charge za bandarini na kama vtalipiwa ni ela ndogo sana
 
Thanks mkuu.
Nimesema furniture kwa ujumla ila ni pamoja na vitu vingine vya nyumbani.

Ili uwashawishi sio vya biashara vinatumika vigezo gani?
Mpendwa, Tumia njia short-cut tafuta BROKER atayamaliza kwa haraka na urahisi !! ila ukianza wewe kuClear...naona utaviacha bandarini na dumarage ya Container utalipizwa!!
Nakutakia kheri na wepesi!!!
 
Kama ni used items lazima hizo items ziwe zimefanyiwa inspection na SGS au Intertek au Cotecna tokea huko huko zinakotoka. Yule aliyekutumia alitakiwa awafahamishe inspector na kuwaita wafanye inspection. Kisha wanatoa ripoti direct kwa tawi la Tanzania na TBS. Bila hiyo ripoti utasumbuka sana.

Who determines the value of used furniture- wewe unatakiwa uwe na estimate ya value ya mzigo. Ni vigumu kuji invoice wewe mwenyewe but kumbuka watanzania tunakariri. Wasipo ona invoice waweza kuzungusha pia. Usipokuwa na your own invoice, TRA will estimate but mind you their estimate is going to milk you.
Okay, sasa utajiandikiaje invoice wewe mwenyewe?

Siuzi furniture, sina kampuni, nitatengenezaje invoice za furniture zimetumika miaka kibao ???

Na hizo "SGS au Intertek au Cotecna" ndio kampuni za nchi gani hizo? Kuna nchi zingine furniture zikitumika kidogo wanatupa nje ya nyumba hapo kama garbage, sijasikia kuna kampuni kazi yake kuja ku inspect furniture nzee, I mean, I never heard of that. For what, to cater to immigrants wanaorudisha ma furniture mabovu Afrika? I mean, that's just a little surprising to me.
 
kama ulikuwa unasoma au kufanya kazi nje na hizo zilikuwa ni vifaa vyako na mybe ulikuwa na gari na umekaa huko nje kwa zaid ya mwaka mmoja vifaa ivyo vinaitwa ni personal effects huwa vinamsamaha wa kodi kwa maana huwa avilipiwi kodi zaidi ya charge za bandarini na kama vtalipiwa ni ela ndogo sana

Hii ni habari njema.
Asante kwa maelezo mkuu.
 
Hii ni habari njema.
Asante kwa maelezo mkuu.

owk mkuu kwan ilo container limefikia TICTS AU TPA ? ukikosa msaada ntafute naweza kukusaidia mkuu lakini ni kama vitu ivyo ulikuwa unavi2mia huko na umekaa huko kwa zaid ya mwaka mmoja na passport yako inaonyesha ivyo toka tarehe ya visa kwan TRA huwa wanatumia passport ili kujilidhisha kama kweli umekaa huko zaid ya mwaka
 
Container zima limejaa furniture? Iwe la ft 20 or 40 mtihani wa kwanza ni kuwaconvince kuwa sio furniture za biashara, kama kweli zimejaa container. Kwa makadirio cost itacheza kati ya dolla 5000 na 7500.
Shukrani mkuu,ila naomba kuulizia iyo makadirio ni kontena lolotee au ni vifaa vya furniture?.

Nilitaka kujua contena la cementi mkuu,pole kwa usumbufu na kazi njema
 
owk mkuu kwan ilo container limefikia TICTS AU TPA ? ukikosa msaada ntafute naweza kukusaidia mkuu lakini ni kama vitu ivyo ulikuwa unavi2mia huko na umekaa huko kwa zaid ya mwaka mmoja na passport yako inaonyesha ivyo toka tarehe ya visa kwan TRA huwa wanatumia passport ili kujilidhisha kama kweli umekaa huko zaid ya mwaka

Ntakutafuta mkuu.
Container bado halitumwa,naulizia kwanza nijue mchakato ndo niamue.
 
Kama umeishi nje zaidi ya mwaka vitu utakavyorudi navyo ni personal effect havina kodi. Ila ni kitu kimoja kimoja,mfano gari moja,friji moja,jiko moja etc. Kuna muda ambao na wewe unatakiwa uwe ushavileta hivyo vitu baada ya kufika tz,sio ukae miezi sita au mwaka ndio uvilete useme personal effect,mara nyingi inabidi uje navyo wakati unarudi[sina uhakika wa muda]
 
mi niliwai kuleta lakin TRA walilitolea macho gari tu na kulingashaa,nililipa kodi ya gari tu makororo na furniture sikulipa
 
Kama umeishi nje zaidi ya mwaka vitu utakavyorudi navyo ni personal effect havina kodi. Ila ni kitu kimoja kimoja,mfano gari moja,friji moja,jiko moja etc. Kuna muda ambao na wewe unatakiwa uwe ushavileta hivyo vitu baada ya kufika tz,sio ukae miezi sita au mwaka ndio uvilete useme personal effect,mara nyingi inabidi uje navyo wakati unarudi[sina uhakika wa muda]

Asante kwa maelezo.
 
Back
Top Bottom