Kabla ya kuwaleta DP World turekebishe kwanza sheria za kodi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,303
Toka hili sakata la Bandari liibuke nilikaa kimya kwanza nitafute facts za kutosha ndo nitoe maoni yangu. Wengi wenu mmekuwa mkinisumbua kutaka kujua msimamo wangu kuhusu hili lakini sikujibu chochote hadi leo nilipoona ni muda sahihi. Niwakumbushe tu kuwa baadhi ya maoni yangu huwa yanakuwa yanaendana na ya serikali. Some huu uzi Hatimaye ushauri niliowahi kuutoa hapa JF leo umetamkwa hadharani na Rais Rais

Kwa upande wangu ninakubaliana kabisa kwa 100% hawa DP World kupewa uendeshaji wa bandari. Sababu zangu kuu ni kuboresha ufanisi na kuongeza mapato ya serikali. Ufanisi ukiongezeka itakuwa ni faida kubwa kwa watumiaji wote wa bandari hivyo kuhamasisha sana biashara na shughuli zingine za maendeleo. Kwa uendeshaji wa TICTS tuliona hadi vifaa vya miradi vikikwama bandarini bila sababu za kueleweka. Kuna wakati hayati JPM aliokota magari na vichwa vya treni. Yaani ulikuwa ni uozo. Meli inaweza toka China na ikafika Dar ndani ya siku 21 ila hadi upate mzigo unahesabu siku 21 zingine. Hali ni mbaya. DP world ni suluhisho.

UPIGAJI. Kwa miaka mingi hadi leo bandarini kumekuaa sehemu ya watu kujipatia utajiri kwa njia ovu. Ukienda bandarini utaona umati wa watu uko bize lakini karibu wote wanawaza upigaji. Hayati JPM alipambana sana na watumishi wa bandari pamoja na washirika wao kwenye upigaji ila hakuweza kufua dafu. Vijana wengi walipelekwa mbele ya vyombo vya sheria na wengine wengi hadi sasa wana kesi mahakamani kwasababu ya tuhuma za wizi wa fedha za umma. Kimsingi nchi inahujumiwa mno kupitia bandari. DP World itasaidia kufutilia mbali huu upigaji kwa kupunguza mianya ya upigaji kupitia mifumo imara ya kiteknolojia.

Kimsingi wanaopinga ujio wa DP World wapo kwenye makundi matatu yenye agenda tofauti; kundi la kwanza ni la WAFANYABIASHARA NA WATUMISHI wasio waaminifu waliokuwa wananufaika kupitia ukwepaji kodi na mambo mengine ya uhujumu bandarini. Vigogo wa hili kundi ni ngumu kujitokeza hadharani ila wameajiri wapambe kupinga. Kwa mfano aliyekuwa mfanyabiashara mkubwa aliyekuwa akiendesha shughuli za bandari yuko kimya lakini bibi mmoja mzee profesa wa huko kijijini kwao yuko bize kupinga hili jambo la faida kwa taifa.

Kundi la pili ni la WANASIASA NA WANAHARAKATI UCHWARA. Hili kundi ni la wasomi walioamua kwa makusudi kabisa kupinga kila jambo la serikali ya CCM ili kupata political mileage. Mtu kama Profesa Shivji ambaye wanafunzi wake wa sheria wamekuwa mabingwa wa kufeli mitihani ya Law School anajua kabisa umuhimu wa DP World ila kwa kiburi kaamua kupinga. Kina Lissu, Mbowe na wanasiasa wengine ni wa kupuuzwa tu kwasababu wao wanajulikana kwa miaka mingi kwenye kupinga kila kitu. Wasipopinga watapoteza sifa ya kuitwa wapinzani.

Kundi la tatu ni la WANANCHI WAFUATA MIKUMBO. Hili kundi lina watu wengi ambao hawajui chochote ila kwasababu Mbowe kasema na wao wanaunga tela. Ni kundi lililojaa vijana wa hovyo waliokosa uzalendo kwa nchi yao. Wao wapo kwenye kila jambo linalotamkwa na viongozi wao bila kujali maslahi mapana ya taifa.

Ninashauri serikali irekebishe sheria zake za kodi ili wananchi wawe na hiari ya kulipa kodi bila kulazimishwa. Kiukweli karibu wafanyabiashara wote hukwepa kodi pale bandarini. Kwa mfano ukiagiza vifaa vya hospitali kutoka China itabidi uwe na kibali cha TMDA & TBS lakini ukisafirisha na Silent Ocean hupeleki kibali chochote zaidi ya kwenda kuchukua mzigo wako Godown. Huwa najiuliza wanawezaje kutoa mzigo kama huu ambao sio wa kwao? Ukisafirisha mwenyewe inabidi umpatie agent hivyo vibali.

Kimsingi kwa huo utaratibu wa Silent Ocean, GNM na makampuni mengine ya usafirishaji ni kuwa kuna tatizo bandarini na kwenye mifumo. Lakini wafanyabiashara wengi tunawatumia hao kwasababu gharama zinakuwa chini. Ukisema ufuate utaratibu wote ulivyo hakika hutatoboa kibiashara. Kodi ni ya maumivu. Serikali kabla ya kumalizana na DP tunaomba sheria za kodi zifanyiwe kazi ili watu wengi wasiwe wanakwepa kodi.
 
Back
Top Bottom