Gharama halisi za kutoa gari bandarini, 2022

Mr Confidential

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,492
2,357
Habari wakuu,

Baada ya kupitia threads kadhaa zilizojaribu kuonyesha gharama halisi za kutoa gari bandarini, nimepata 'mawili-matatu' lakini bado kuna vitu vinanitatiza.
Screenshot_20220331-150526_Chrome.jpg

Mchangiaji wa kwanza ameorodhesha;
Shipping lines=150,000
Wharfage =115,000
Port charges =250,000
Plate number =30,000
Agency fee =300,000.
----*----****

Screenshot_20220331-150326_Chrome.jpg

Mchangiaji wa pili akaandika hivi:

Handling charges = $7 per cbm +VAT,
Corridor levy = $0.3 per cbm + VAT
Wharfage = 1.6% ya CIF

Screenshot_20220331-145919_Chrome.jpg

Mchangiaji wa tatu akaandika hivi;👆
*Hiyo namba moja sijaielewa.
*Namba 4 pia sijaelewa, kuna Port charges na Port handling charges?
 
*Nimejaribu kutafuta mchanganuo wa hizi gharama kwenye website ya TPA lakini nimekosa.
* gharama ninazohitaji kujua ni za magari madogo (ist, vitz,nk) maana ndo gari yangu ya kwanza nataka kuagiza.
*nimeshindwa kujua gharama halisi kwasababu kila mtu ameandika la kwake.
*pia ningependa kupata ushauri wow wowote kuhusu kumiliki gari kwa mara ya kwanza. Machaguo yangu ni vits au ist
 
Habari wakuu,

Baada ya kupitia threads kadhaa zilizojaribu kuonyesha gharama halisi za kutoa gari bandarini, nimepata 'mawili-matatu' lakini bado kuna vitu vinanitatiza.
View attachment 2170421

Mchangiaji wa kwanza ameorodhesha;
Shipping lines=150,000
Wharfage =115,000
Port charges =250,000
Plate number =30,000
Agency fee =300,000.
--------***

View attachment 2170438

Mchangiaji wa pili akaandika hivi:

Handling charges = $7 per cbm +VAT,
Corridor levy = $0.3 per cbm + VAT
Wharfage = 1.6% ya CIF

View attachment 2170445

Mchangiaji wa tatu akaandika hivi;
*Hiyo namba moja sijaielewa.
*Namba 4 pia sijaelewa, kuna Port charges na Port handling charges?
Kutoa gari bandarini kwanza inategemeana na aina ya gari yenyewe, kuna za kuanzia laki 6, laki 8 na kuendelea. Kwa huyo jamaa ambae kaandika hio laki 3 ya TBS ni kwamba gari yako ikifika hapa bongo ni lazima ikaguliwe, sasa katika ukaguzi ikatokea wameona faults ama shida ndani ya gari itatakiwa ukairekebishe kwanza then ndo iweze kupitishwa ko sielewi hio 300k kawapea TBS ya nini...ila akili yangu inanituma itakua ya kurekebisha fault iliokutwa au alijiongeza akawapea kitu kidogo ili gari yake ipite.
Malipo mengine kama number plate, storage na zingine zilizobakia ndo za lazima hizo. Maana gari yako haiwezi kaa bure pale and mostly baada ya kufikisha siku 7 kuanzia imefika bandarini
 
Ahaaa, Gari ni IST old model.
Sasa hii storage cost (7 days za mwanzo) inaingia kwenye hio Port charges?
Naona wachangiaji wengine hawajaiandika.
 
Bei Inategemeana na gari yako mkuu, ila service kama itahitajika kufanyika inakua sana sana ya kubadili oil, oil filter, brake pads nk. Katika mchanganuo wa oil hapo sasa ndo bei zinakua zinatofautiana...kuna oil za 45k na kuendelea huko mbele.
Kwa IST nikiweka budget ya 300,000 itafaa sio?
 
Kwa IST nikiweka budget ya 300,000 itafaa sio?

Kwa maana ya Service ya kumwaga oil, kama itaonekana haiko vizuri hydraulic oil(gear box), filter nk kwa maana hakuna parts zingine kama gari ilishafanyiwa Service Japan nafikiri hata 150,000 inaweza kufit. Kwa mfano
1. Oil ya Total au PUMA angalau Tsh50,000-60,000
2. Oil ya Gear Box Litre 3 au 4 angalau 50,000 Maximum side
3. Airfilter- 30,000
4. Oil Filter angalau 10,000

Hapo ni kama 140,000! Kazi hii mara nyingi huwa ni ya kawaida na hivyo ufundi wake ni Tsh 10,000 hadi 30,000 tu!
Bei hizo ni makadirio ya juu kidogo
Hivyo Bajeti ni kati ya TSh 130,000- 200,000 kutegemea na fundi na garage!
 
Nami nafutatilia kwa karibu sana; nami kimkwwche changu kiko njiani kinakuja..ila nasikia TBS wanasumbua sana; urasim mwingi sana; wanalimbikiza mambo tu bial sababu
 
Nimeelewa vizuri sana, Asante mkuu, Ishi sana
 
Nami nafutatilia kwa karibu sana; nami kimkwwche changu kiko njiani kinakuja..ila nasikia TBS wanasumbua sana; urasim mwingi sana; wanalimbikiza mambo tu bial sababu
Unatakiwa ucheze nao kwa akili nyingi, uwasome wanataka nini hasa, sana sana gari ikiwa haina dosari inapitishwa (japo ni ngumu sana)
 
Daaah! Kazi Ninayo

Tafuta agent mzoefu mwenye channel kule Tbs hata ikikutwa na tatizo ukirefusha mkono inapitishwa tu ila kuna rushwa kidogo andaa budget kama 150,000-200,000/= ya kuwapoza jamaa.
Mara nyingi matatizo yanayowakumba waaguzaji wa magari japani ni Tyres kama zime expire au crecks au leakege hizo ndizo common problems.

Assume unaambiwa ukabadilishe tyre zote ambazo zinagharimu hela kubwa (Kumbuka sometimes unakuwa na plan either ya kuliinua gari kama liko chini means ununue rims na tyre za size kubwa ) kitu ambacho ni gharama kidogo
Ila wale wajamaa ukiwaachia 150k wanaipitisha kisha unaendelea kurekebisha mdogo mdogo.

Angalizo: maagents wanaijua hii michezo.

Pia Tbs wanatoa siku 14 (au 21 kama sijakosea) kurekebisha kasoro zilizoonekana,
So gari unaendelwa kulitumia (bila kusajiliwa utatumia Chasisi no) huku ukijichanga kidogo kidogo kifanya marekebisho zikifika hizo siku unarudisha gari walihakiki kama umerekebisha so usumbufu hao wote unaweza kurefusha mkono ukamalizana nao.

Pia kuna issue kama ni tyre unaweza kuvua za gari la mtu ukaenda kukaguliwa then ukitoka unamrudishia unavaisha tena tyre kwenye gari lako.

Ni simple tu ukienda pale maeneo ya KEKO vijana wengi wanafanya hizi mambo na wana connection pia.
 
Hapa nimekuelewa. "Penye udhia penyeza rupia"
Asante
 
Back
Top Bottom