Gharama halisi za kutoa gari bandarini, 2022

Naomba uniorodhoshee gharama za bandarini. Hili ndo lilikua hitaji la kwanza la uzi

Mkuu, kwani bado hujaandaa clearing Agent wa kukufanyia process yote ya kutoa gari bandarini?

Agents wapo wengi mno. Wanakupa gharama zote na za bandari. Wanatofautiana (kidogo sana) kigharama. So unaconsult agents hata wawili watatu hivi na kulinganisha gharama, kisha unachagua mmoja.

Maswala yooote watakujibu, na wanakupa gharama yote complete kuanzia bandarini hadi ada yao. Gharama za bandari na ushuru wa TRA hutofautiana kutegemeana na aina ya gari.

Kuna baadhi ya gharama utalipia wewe mwenyewe directly via bank popote ulipo.. ushuru TRA, Port charges, na shipping line.

So tafuta clearing agent atakupa info zote zilizo up to date. Gharama zinabadilika badilika ama kupanda kila leo.

Waeza process wewe mwenyewe kutoa gari bandarini ili kukwepa agent fees. Lakini ni usumbufu mno mno ukifuatilia wewe mwenyewe. Watu wa bandari na hawa clearing agents ni kama wana kanetwork na 'konection' fulani. Wao kwa wao mchakato ni easy tu. Ukienda mtu binafsi kuclear gari lako unakutana na urasimu kibao!!

Cha muhimu chagua/tafuta a trusted agent.
 
Kutoa gari bandarini kwanza inategemeana na aina ya gari yenyewe, kuna za kuanzia laki 6, laki 8 na kuendelea. Kwa huyo jamaa ambae kaandika hio laki 3 ya TBS ni kwamba gari yako ikifika hapa bongo ni lazima ikaguliwe, sasa katika ukaguzi ikatokea wameona faults ama shida ndani ya gari itatakiwa ukairekebishe kwanza then ndo iweze kupitishwa ko sielewi hio 300k kawapea TBS ya nini...ila akili yangu inanituma itakua ya kurekebisha fault iliokutwa au alijiongeza akawapea kitu kidogo ili gari yake ipite.
Malipo mengine kama number plate, storage na zingine zilizobakia ndo za lazima hizo. Maana gari yako haiwezi kaa bure pale and mostly baada ya kufikisha siku 7 kuanzia imefika bandarini

TBS Tsh 350,000/= ni Lazima (gharama ya UKAGUZI) likikutwa na kasoro unaenda kurekebidha kisha utarudisha kwa gharama zako ila wao lazima 350,000 uilipe kwa Control number KABLA ya gari kukaguliwa.
 
TBS Tsh 350,000/= ni Lazima (gharama ya UKAGUZI) likikutwa na kasoro unaenda kurekebidha kisha utarudisha kwa gharama zako ila wao lazima 350,000 uilipe kwa Control number KABLA ya gari kukaguliwa.
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom