Jamanai jamani wakunga kazi yao ni nini? waacheni wakunga wafanye kazi zao.
Kweli uzazi wa siku hizi unachangamoto zake ila sio kwa kujitakia kisa flani na flani walipata shida ya kujifungua hivyo na mimi niwahi operation ili nisipate shida kama ya yule. Nani kawaambia yaliyomtokea mwajuma yatampata asha?? Natamani ningefanya semina kwa wadada na wakaka wazazi wa kipindi hiki niwaelimishe hatari za operation na faida za kujifungua kawaida.
Kwa utashi wangu mwanamke aliambiwa kwa uchungu atazaa sasa ikitokea kuna shida zaidi ya hapo ndipo wakunga watakupeleka ufanyiwe upasuaji au operation au siza kama wanavoita kwa lugha ya kitaalam na si kujiandikia kuwa ntafanyiwa operation kabla ya uchungu.
Hivi wazazi watarajiwa wa kipindi hiki mnajua madhara ya operation kweli? kama madaktari haohao na wakunga hao hao wanashindwa kuwa makini kwenye kuzalisha kawaida wataweza kuwa makini kwenye operation wamtoe mtoto salama bila mikwaruzo na mam je? watamshona bila kumuachia ulemavu au shida yoyote?
Mimi huwa siwaelewi kabisa wanaaomba operation, hebu acheni kujiombea matatizo KAMA HAMTAKI KUPATA UCHUNGU BASI MSISHIKE MIMBA KABISA NA KAMA MNATAKA WATOTO NENDENI MKAADAPT WATOTO YATIMA KIBAO.
Na wamama wasiotaka kupata uchungu na kujifungua kawaida bila kushauriwa na daktari wafanyiwe operation ndo hao hata watoto hawawanyonyeshi kazi kuwalisha makopo tuu. Yaani natamani wamama wote wajawazito na watarajiwa kuolewa wasome hapa waelewe kuwa kujifungua kawaida kama hutapata shida yoyote ni salama kuliko operation. N aikitokea shida ndo utafanyiwa operation ndiomaana wajawazito wanatakiwa kuattend clinic mara tu wajutambuapo ni wajawazito.
Jamani wakunga na madaktari najua mpo humu jamii forum ukiachilia mbali na biashara ya kuingizia hospitali hela kwa njia ya operation naombeni mnisaidie kuwashauri wamama watarajiwa wasichague operation kwa kisingizio cha kujifungua salama, tafadhali, yaani sijui nisemeje, sijui watu wanawaza mara mbili au wanaamua tuu..........
Muanzisha mada, kama mkeo hana shida yoyote hawezi kufanyiwa operation bila wewe kusign mkatalie kusign na umwambie ajifungue kawaida wacha operation ije kwa ushauri wa daktari na angalia asimuhonge daktari ili amuandikie operation au ajidai presha juu ili afanyiwe mshauri mkeo kuwa hii ni kwa afya yako, kama anajipenda yeye mwenyewe hawezi jitafutia makovu ya visu kwa kujitakia wakati angeweka kuzaa kawaida tuu.
Mwisho wa siku maamuzi ni yenu kuchagua jema na baya hata mungu aliwaachia wanadamu kuchagua moto au baridi mradi tuu usije kujuta baadae.
Na wanaojidanganya kwa kufanyiwa operation K inabaki kama ilivo poleee, ile ni maumbile wengine wamejifungu watoto 4 na bado inarudi japo si kama mwanzo ila kwa kipimo cha mumeo na bado wakafurahia tendo, sasa we wa operation utapata excuse ya kutofanya hadi kidonda kipone wakati wa kawaida siku 40 tuu mchezo kama kawa na baada ya kidonda kupona wengine wanatumia mshono kama kisingizio cha kutokuwapa waume zao mchezo akidai mshono unauma kumbe anagawa nje wewe unajikaza ulee mshono, poleni na kila la kheri ila shida iko kwa wamama wa kizazi hiki loooh