Nakumbuka siku moja niliingia matatani na jamaa wa suti nyeusi wale nakuaga kule nyuma ya ikulu beach kule wanao jifanyaga nao eti wanapanga upepo na hata mashati unaweza kuta wamevua.
Alikuja jamaa yangu kutoka mkoa hivyo nikaamua nimpeleke akaone bwana mkubwa wa wakati huo NKAPA anapoishi. Sasa kwa uzoefu wangu wa ule ukuta unaozunguka nyumba nyeupe kila baada ya mita tano au sita Kuna nguzo ya taa pamoja na vioo/camera ambavyo kazi yake wote twaijua.
Wakati tunapita kule upande wa beach nikawa namuelezea mgeni wangu juu ya hivyo vioo viliyo uzunguka ule ukuta wa nyumba nyeupe.katika hali isiyotarajiwa nilikuta mtu ananishika bega na kuanza nihoji vioo gani hivyo navyo zungumzia. Nilifikiria anatania tuu kumbe jamaa alikua kazini hasaaa.
Ashukuliwe mungu sikua na nia mbaya na Ile nyumba nyeupe, japo ilikua mbinde sana hadi kuwa huru.
Zama hizi za jiwe sio busara kabisa unapopita mitaa Ile kujaribu kukodolea macho eneo lile.
USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO