Sitosahau hii, siku moja natokea zangu jengo lile utumishi naenda zangu hospital ya Aga khan ilikuwa siku ya J2 mida ya saa kumi hivi.
Nikapita kule nyuma ya ikulu, sasa wakati napita nikawa napita upande wa katikat jamaa mmoja akanisimamisha na kuniambia nisipite pale nikamjibu mbona wale wanapita akaniacha nikaendelea kufika mbele nikaitwa na wale waliovaa za mabaka baka, nikaanza kupigishwa push up ila siku pekee yangu niliyekuwa nikipewa adhabu tulikuwa kama sita hivi.
Bahati nzuri akatokea mwana tunayefahamina naye katika wale walio mabaka baka ndo wakaniacha jioni yake baada ya kuonana na jamaa aliyenitetea kwa kwa ushauri alionipa sikutamani kupita njia ile tena na mpka leo sijarudia kupita njia ile japo nilikuwa napenda sana kuitumia..
Sent using
Jamii Forums mobile app