Gesi kushuka bei kesho

Gesi kushuka bei kesho

Daah,kweli ukiwa interia mambo ni magumu tuu huku tunanunua 22,000 kwa kilo 6
 
Mkuu hii LPG(Gesi ya kupikia) haivunwi hapa tanzania. Nayo ina ingizwa kama mafuta ya petrol na diesel!! Hii ya kwetu ni natural gas ambayo japo inaweza tumika kupikia ila sio kwa kuwekwa kwenye mitungi ina bidi wakuunganishie bomba hadi nyumbani kwako ndio uweze kutumia kuna baadhi ya nyumba masaki wanatumia gesi hiyo ya mtwara,
Asante kwa kutujuza mkuu
 
Vizuri, hata hivyo bado bei juu sana ikizingatiwa ges tunavuna wenyewe hapa hapa Tanzania, ilipaswa kwa kg 15 angalau iwe tsh 30,000 na kg 6 tsh 11500.

Nasikia ile gesi ya Mtwara haina uhusiano na hii tunayopikia majumbani, wataalam watufahamishe zaidi
 
Asante sana kwa taarifa, je mamlaka husika zimejipangaje kuhakikisha bidhaa inauzwa kwa bei elekezi katika maeneo yote?
 
Ule mtungi wa kg 15 inatakiwa ishuke hadi 25,000 ndo itakuwa fair, na itaonyesha kweli tunachimba gesi
narudia tena mkuu gesi ya kuchimba haiji leo wala kesho inahitaji mambomengi sana tunayotumia tunatoa nje na wanapakia pale bandarini unaweza pita ukaona matanki yao
 
Mkuu hii LPG(Gesi ya kupikia) haivunwi hapa tanzania. Nayo ina ingizwa kama mafuta ya petrol na diesel!! Hii ya kwetu ni natural gas ambayo japo inaweza tumika kupikia ila sio kwa kuwekwa kwenye mitungi ina bidi wakuunganishie bomba hadi nyumbani kwako ndio uweze kutumia kuna baadhi ya nyumba masaki wanatumia gesi hiyo ya mtwara,
Shukrani kwa ufafanuzi wa hili jambo. Watu wengi wanapoona mitungi ya gesi wanadhani inatokana na gesi ya Mtwara. Kenya imezuia gesi kuingia nchin kwao kutokea Tanzania na wakati huohuo Kenya nao wana bandari kwahiyo kuna kamchanganyiko hapa.
 
Back
Top Bottom