JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amejibu maswali kadhaa wakati wa mahojiano aliyofanya na Kituo cha UTV, leo Jumatatu Oktoba 13, 2025;
Mnadhani kwa nini Maandamano yanapangwa Siku ya Uchaguzi?
Siamini kama Wananchi wanapanga maandamano hayo, ni vikundi vya watu wachache, tunajua ni michezo ya watu, mtu mmoja anaweza kuwa na akaunti hata 200 anatumia hizo ili ionekane ni watu wengi.
Watanzania wanajitokeza kwa wingi kwenye kampeni, wangekuwa hawataki kushiriki uchaguzi wasingeenda kwenye kampeni.
Kila kitu kinachukuliwa kwa uzito wake, niwahakikishie tarehe 29 Oktoba amani ipo ya kutosha, hakuna atakayekimbizwa na hakuna atakayefanywa chochote.
Kwa Tanzania kuna mipaka katika uhuru wa kutoa maoni?
Mipaka ipo, Watanzania wana uhuru wa kutoa maoni lakini kila uhuru una wajibu, huwezi kutoa maoni yenye madhara kwenye jamii kisha Serikali ikakaa kimya.
Serikali ipo hapa kuhakikisha unatekeleza haki zako lakini wakati huohuo unalinda haki za watu wengine.
Nchi yetu haijazuia Vyombo vya Habari, Serikali kama chombo tuna wajibu wa kulinda nchi, tukiona una hoja za kuleta madhara kwenye Jamii tunachukua hatua, tumefanya hivyo kwa wachache, ndio maana hata mitandao ya kijamii ipo na inaendelea kufanya kazi.