Gerson Msigwa: Tuko mbioni kuanzisha Televisheni ya Serikali itakayorusha Habari za Maendeleo tu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,015
142,055
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema wizara ya habari iko mbioni kuanzisha Television ya serikali itayorusha mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali.

Television hiyo itakuwa tofauti kabisa na TBC kwani itarusha mambo ya msingi ya serikali amesema Msigwa.

Chanzo: Clouds tv
 
Hii nchi ni ngumu sana kuielewa!!yaani Tv ya taifa ipo na ndio mpiga debe mkuu wa serikali, kuna chaneli ten, mpiga debe wa chama, zote hizo hazitoshi?!!sasa kama ni hivyo kwanini wasiifanye TBC 2, ndio iwe na majukumu hayo?!!
 
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema wizara ya habari iko mbioni kuanzisha Television ya serikali itayorusha mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali.

Television hiyo itakuwa tofauti kabisa na TBC kwani itarusha mambo ya msingi ya serikali amesema Msigwa.

Source: Clouds tv
Huu ni mradi mpya,je kwenye bajeti ya 2021/22 ulitengewa fedha? Au ndoto ya mchana?
 
Mzigo wote huo wa Gharama anabebeshwa Mwananchi wa Kawaida, TBC yenyewe imekuwa Mzigo ndiyo Sembuse hiyo TV channel mpya?

Bora hiyo gharama mngejikita kwenye kutoa Bima ya afya kwa kila Mwananchi
 
Ukiona Hivyo Kuna Deal Wameshalipamba, Hii hata Haiwezi Kuingia akilini Kwa Maana kuna TBC1, TBC2 na Chanel Ten then eti anapanga Kuanzisha Utopolo Mwingine. Kwanza Watanzania Wachache Wanaziangalia Hizi TVs za CCM Kwa Jina la TV za Taifa
 
Back
Top Bottom