George Liundi ...

Tendwa ampiga `kijembe` Liundi
2009-01-03 12:00:40
Na Simon Mhina

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, amesema kama ni kweli mtangulizi wake, George Liundi anaishi maisha ya dhiki, basi anavuna alichokipanda.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Tendwa alisema Liundi ambaye ni Msajili wa kwanza wa vyama vya siasa nchini na ambaye pia aliwahi kushika nyadhifa kubwa serikalini, kama alishindwa kujijengea maisha bora wakati huo, hivi sasa `atajiju`.

Akifafanua, Msajili huyo alisema ukifuatilia historia ya Liundi tangu nchi ipate Uhuru, utakuta ameshika nyadhifa kubwa ambazo zilimfanya apokee mshahara mkubwa, ambao ungemfanya ajijenge kimaisha bila hata `kuchukua chake mapema`.

``Mfanyakazi yeyote unapokuwa kazini, sio tu unalipwa mshahara, lakini pia kuna pensheni, Liundi alikuwa afisa wa juu sana serikalini.

Anaposema ana shida ananishangaza mno. Anapotoa madai kama hayo, anataka na wale waliokuwa makarani kwenye ofisi alizofanyia kazi nao wasemeje?`` Alihoji.

Tendwa alisema hatma ya mfanyakazi yeyote, inategemea sana alivyokuwa anatumia mshahara wake na marupurupu wakati akiwa kazini na kujiwekea akiba ya uzeeni.

``Sasa kama mshahara wako ulikuwa unaumaliza, lazima utapata shida. Ukiwa madarakani, unatakiwa kipato chako ukitumie vema, unatakiwa kujipanga ukijua kuwa kuna leo na kesho ukishastaafu unaubeba msalaba wako mwenyewe, vinginevyo waswahili wanasema `utajiju` hakuna wa kukusaidia,`` alisema.

Aliongeza: ``hivi sasa hata akitokea malaika, siamini kama atakuwa na nafasi nzuri ya kumsaidia Liundi kimaisha kushinda fursa ambayo Mwenyezi Mungu alimpa miaka yote,`` alisema.

Alipoulizwa kama ofisi yake inaweza kumsaidia `chochote`Liundi kwa wakati huu, Tendwa aliangua kicheko huku akisema maisha ni sawa na msichana ambaye mvulana anatakiwa amtongoze mwenyewe.

Alisema mkongwe huyo hakuona mbali, kwa vile alitakiwa atafute kiwanja sehemu nzuri kama Kibamba, Mbezi maeneo ambayo huenda aliyakataa kwa vile yalionekana kuwa shamba.

Tendwa alisema kwa kutambua hilo, ndio maana yeye amejijengea maisha yake mazuri na kamwe hategemei kuwa na dhiki ndogo ndogo hata atakapostaafu.

``Mimi ninaishi Kibamba, nimejenga zinga la nyumba, nimeweka marumaru kwa vile nahusudu usafi, kila mtu ana mapenzi na mambo anayopenda kuyapa umuhimu, kwa hiyo huyo ambaye hana nyumba nzuri, huenda alikuwa hapendi mambo hayo,`` alijigamba.

Aliongeza: ``nina shamba kubwa lenye mifugo na mimea mingi. Nikiwa nyumbani, nakula machungwa niliyopanda mwenyewe, na mimi navuna nilichopanda,`` alisema.

Hata hivyo, alifafanua kuwa, mali alizonazo ni halali kabisa na kwamba hajadokoa chochote toka serikalini.

SOURCE: Nipashe
 
UJASIRIAMALI nayo ni issue jamani,wengi hawajui namna ya kufanya fedha walioyopokea kama mafao iwatumikie mpaka kufa kwao wanabaki kuitumikia mpaka wanakufa kabisa


..njia sahihi ya watumishi wa umma kujijengea maisha bora na kwa kuwekeza kwenye hisa....watumishi wengi wa umma wanakosea sana wanapokimbilia ujasiriamali uzeeni ...wengi wameishia kuwekeza pesa zao za mafao na zikapotea zote ...kwa hasara..

lazima wajuwe kuwa biashara au kilimo ni taaluma siku hizi ...au uzoefu ...kama huwezi bora uwaachie watu waeneshe na wewe ubakie mwanahisa...muhimu ni kuwa makiini kuchagua kampuni ya kuwekeza...

pia wastaafu wengi wanakosea kwa kutojuwa kuwa baada ya kustaafu maisha yanabadilika na inabidi ukubali hali...wengi hupenda ku keep standard ile ile..wakati haiwezekani ....kwani incentives nyingine walikuwa wanapewa bure..ie entertainment allowances...,influence,mialiko ya karamu etc....you can not maintain that status unless una pesa nyingi sana...au ukubali ku maintain status kwa miaka michache ...then ufilisike kabisa.....nadhani bora kuishi maisha simple na ya kiasi kwa maisha yako yote...kuliko raha ya muda mfupi......

unapostaafu lazima ujuwe its end of an era,,...unaachia wengine .......ukitaka kulazimisha utaanguka....
 
MH Tendwa usitukane Mamba kabla ya kuvuka mto.
Mamba anayemla Liundi anakusubiri wewe pia.
Pensheni wanayolipwa wastaafu Tanzania ni matusi matupu si pensheni.
Watu wengi na mamilioni yao wamestaafu kwa mbwembwe leo hii wako waya ile mbaya.
Kufanya biashara huku unaongezea mtaji kwa fedha za ufisadi au kuwekeza kwa kutumia cheo chako bado hiyo si biashara.
Kama ingekuwa ni kweli ninyi akina Tendwa na serikali ya sasa mna uchungu na maisha yenu siku ile ya kukalia benchi ikifika tungeona mkitunga sheria ili mashirika yaliyokuwa ya umma yanunuliwe na watanzania walio wengi na kuleta wataalamu toka nje ili wayaendeshe kibiashara.
siyo hii ya kwenda kujenga vijumba hapa na pale huku mmezoea kufuja fedha za umma bila kujali tarakimu yake.

Timu yenu inauza mashirika yote kwa maghaibu na kuvuta kitu kidogo kwa sababu kesho kwenu haina jina wala tafsiri.

MH Tendwa usiseme sana.
 
..........smh.....Huyu Liundi si anaye watoto, mara ya mwisho nimecheki Taji alikuwa meneja wa kituo cha redio...wampige jeki kama vipi......au kivyake.

Taji liundi hapa mtamuonea tu kwani nae maisha yake ya ujanjaujanja tu!jina kubwa kuliko kipato!
 
Kwa roho mbaya aliypnayo Taji, hawezi msaidoa huyo mzee George Liundi
 
Back
Top Bottom