George Liundi ...

Cha muhimu ni mtu kuishi maisha kulingana na jasho lake, whether u end up in buguruni or one of those posh suburbs ndio effort zako zimekufikisha hapo. What's important at the end of the day is one should have a clear conscience and not have to look over their shoulder. What good are Mramba etc's ill acquired mansions and other perishables now? The shame, the confinement in Dar, "the looks", laana(i'm told hizi zinaaffect waliomo na wasiokuwemo ie even generations to come in the clan)
 
Bongolander heshima mbele mkuu, nimesoma contribution yako na humo umemuandika bwana mmoja anaitwa Rugunyamheto kuwa nae anawezakuwa anaelekea walipofika wakina Apiyo!!! MKUU HIYO SI KWELI KWASABABU HUYU BWANA RUGUNYAMHETO NI FISADI ALIYEKUBUHU; ninastaajabu sana kuona kuwa yeye hajapandishwa Kisutu mpaka sasa. huyu bwana ndiye aliyejenga hoja kwa Mkapa mpaka nyumba za serikali wakauziwa kwa bei ya che,na yeye alikarabati nyumba yake kwakutumia mamilioni [pamoja na Lumbanga ] ya fedha za wadanganyika kabla ya kuuziwa. Sio hivyo tu huyu bwana amekula 10% yake ya commission kwenye ujenzi wa jumba la ofisi za UTUMISHI hapo karibu na feri!! Kwahiyo huyo mzungu wako anazo!!

Du thanks mzee kwa kuniweka sawa, naona list inazidi kuongezeka na kuongezeka. Let us hope sheria itamfikia pia!
 
..hawa wazee msiwaonee huruma hata kidogo..washamba kabisa..!!!..wanatutia aibu....,mtu huwezi kuwa kwenye rank ya presidential appointment..yet unashindwa kutumia mapato yako vema ..then uje kulaalama...wajinga hawa...sio lazima uwe fisadi ili uwe na maisha bora..ukweli ni kuwa posho,mishahara,safari na allowances nyingi wanazopata hawa wakuu hawatakiwi kuwa masikini hata kama mfumo wa mafao ya uzeeni ni mbovu.....waliendekeza starehe na kujengea mabibi majumba hawa!!!!!!!!

..just lets be serious..huwezi kuniambia mtu kama chedial mgonja...a long time foreign minister...mtu kama..jaji mwesiumo...mtu kama marehemu..profesa machunda [one time agriculture minister ...na wengine wengi leo hii wanakuwa malofa au wanakufa malofa...wakinga hawa na wafujaji.....na ndio wamesababisha wanasiasa wa sasa wakiwaona wanaamua kuiba...wakifikiri watatajirika...wanasiasa wa bongo hata wakiwa na 100 billion...leo mpe miaka mitano anafilisika....

juzi nimekutana na waziri mstaafu wa muda mrefu ..arcado ...naona naye kachoka hadi unamuonea huruma....serikali lazima i adree hili tatizo....nashauri wanasiasa wa tanzania wakifunze kuwekeza mafao yao kwenye HISA,mashamba makubwa[commercial farming .....etc...

juzi nilikuwa naangalia tv ..nikiwa kenya....nikaona wanaoonyesha maisha ya waziri mmoja mstaafu....wakawa wanamuuliza retirement benefit na savings zake amefanyia nini...aliwapeleka kwenye apartments anazojenga ....na pia akawaonesha shamba la chai na ngombe.....

kingine watanzania tunaabudu sana umaskini.....utakuta mtumishi wa umma hata kama atakuwa na shughuli halali au ana pesa za fortune...akifanya mradi mkubwa tayari maneno yanaaza..hii mwisho husababisha wanasiasa na watumishi wa umma kuamua kufanyia starehe pesa zao..wakiogopa kufanya mradi wa kuonekana ili wasipate kashfa...nashauri tuache wivu!!!!...hii inasababisha pesa zetu zinaibiwa kwenye ufisadi...na wala haziwekezwi ..zinaishia kutumika kwa hanaasa....

........nadhani tone fahari kuwa na watumishi ambao wanaweza kuwekeza vipato vyao kwenye njia halali......na tunapoona wanafanikiwa tusikimbilie kuwaita mafisadi...hadi tumechunguza na kubaini........
 
Huyo Liunda ana laana ya mkewe. Kumbukeni huyo mzee alimtelekeza mkee wake na watoto wakete (mama yake Taji) mpaka mama akachanganyikiwa akaamua kunywa sumu na kuwanywesha watoto wake. Ni bahati mbaya au nzuri mama na Taji walisalimika lakini wote waliaga dunia. Huyo mama alishitakiwa na kuhukumiwa ila nasikia alipata msamaha wa Rais wa awamu ya kwanza.

Na ninasikia Taji na baba yake hawana mahusiano mazuri kutokana na matattizo ya mzee.
 
..
..just lets be serious..huwezi kuniambia mtu kama chedial mgonja...a long time foreign minister...mtu kama..jaji mwesiumo...mtu kama marehemu..profesa machunda [one time agriculture minister ....
Thanks for the info'

RIP Profesa Machunda
 
..

kingine watanzania tunaabudu sana umaskini.....utakuta mtumishi wa umma hata kama atakuwa na shughuli halali au ana pesa za fortune...akifanya mradi mkubwa tayari maneno yanaaza..hii mwisho husababisha wanasiasa na watumishi wa umma kuamua kufanyia starehe pesa zao..wakiogopa kufanya mradi wa kuonekana ili wasipate kashfa...nashauri tuache wivu!!!!...hii inasababisha pesa zetu zinaibiwa kwenye ufisadi...na wala haziwekezwi ..zinaishia kutumika kwa hanaasa....

........nadhani tone fahari kuwa na watumishi ambao wanaweza kuwekeza vipato vyao kwenye njia halali......na tunapoona wanafanikiwa tusikimbilie kuwaita mafisadi...hadi tumechunguza na kubaini........

Kaka nakubaliana nawe juu ya hawa wastaafu ambao walikuwa Mafuska.....ila ningependa kuweka sawa hio qoute hapo juu, ...Hakuna anaependa Umaskini...
utakuta wengi ambao sasa wana suffer in one or another babu/baba zao walitumia vibaya ujana wao....Mtumishi wa Umma kama anawekeza ktk Halali atafahamika....Mfano mwalim akiwekeza atajulikana...ila wengi kwa hivi leo tunapenda njia za Mkato...Huwezi itwa Fisadi kama una njia Halali za kuendesha maisha yako....

Unajua njia za Haramu huwezi fanya peke yako, wale unaoshirikiano nao ndio watakaotoa siri kuwa Umeiba au umedhulumu...na hapo ndipo sie watu wa mtaani tutakapokwita Fisadi...Ukichuma vya Halali even neighbors watapata harufu ya sifa unazoletewa......

Huwezi fanya dhulma ukakaa kimya, Hata mzinifu akishazini lazima aje ajitambe...Ahha yule nimemla..etc ......kulikuwa na muuza duka la rejareja..akaja mtu kununua kadi ya simu...baadae akasahau simu yake pale dukani...aliporudi....muuza duka akakataa kabisa hakuchukua simu. Kumbe kachukua kaizima...then akampelekea simu mkewe...mkewe akamuuliza umeipata wapi simu...jamaa akampa real story, then akamwambia usiwaambia Jirani..ila wakikuuliza waambie kuwa nimeokota ktk daladala...Mkewe kweli alipohojiwa na Jiran simu umepata wapi kwani wanafahamika kipato chao!!!...Mkewe awali akasema mumewe ameokota...Ikatokea Jiran mmoja akamuazima hio simu ...akaenda nayo sokoni...alipofika Soko la Karume Ilala...akakutana na Missiona town..watu wa kanyaboya...Wakamuuzia Dhahabu Feki ...nae akapigwa bao la SIMU...Jiran aliporudi home kuulizwa simu ipo wapi...akasema ametapeliwa...Jiran mmoja ikabidi ambane yule mke wa muuza duka vema...ikabidi aseme ukweli simu ile namna ilivyopatikana.!!..mali ya Wizi/dhulma haitakuwa na mwisho mwema!!!
 
..hawa wazee msiwaonee huruma hata kidogo..washamba kabisa..!!!..wanatutia aibu....,mtu huwezi kuwa kwenye rank ya presidential appointment..yet unashindwa kutumia mapato yako vema ..then uje kulaalama...wajinga hawa...sio lazima uwe fisadi ili uwe na maisha bora..ukweli ni kuwa posho,mishahara,safari na allowances nyingi wanazopata hawa wakuu hawatakiwi kuwa masikini hata kama mfumo wa mafao ya uzeeni ni mbovu.....waliendekeza starehe na kujengea mabibi majumba hawa!!!!!!!!

..just lets be serious..huwezi kuniambia mtu kama chedial mgonja...a long time foreign minister...mtu kama..jaji mwesiumo...mtu kama marehemu..profesa machunda [one time agriculture minister ...na wengine wengi leo hii wanakuwa malofa au wanakufa malofa...wakinga hawa na wafujaji.....na ndio wamesababisha wanasiasa wa sasa wakiwaona wanaamua kuiba...wakifikiri watatajirika...wanasiasa wa bongo hata wakiwa na 100 billion...leo mpe miaka mitano anafilisika....

juzi nimekutana na waziri mstaafu wa muda mrefu ..arcado ...naona naye kachoka hadi unamuonea huruma....serikali lazima i adree hili tatizo....nashauri wanasiasa wa tanzania wakifunze kuwekeza mafao yao kwenye HISA,mashamba makubwa[commercial farming .....etc...

juzi nilikuwa naangalia tv ..nikiwa kenya....nikaona wanaoonyesha maisha ya waziri mmoja mstaafu....wakawa wanamuuliza retirement benefit na savings zake amefanyia nini...aliwapeleka kwenye apartments anazojenga ....na pia akawaonesha shamba la chai na ngombe.....

kingine watanzania tunaabudu sana umaskini.....utakuta mtumishi wa umma hata kama atakuwa na shughuli halali au ana pesa za fortune...akifanya mradi mkubwa tayari maneno yanaaza..hii mwisho husababisha wanasiasa na watumishi wa umma kuamua kufanyia starehe pesa zao..wakiogopa kufanya mradi wa kuonekana ili wasipate kashfa...nashauri tuache wivu!!!!...hii inasababisha pesa zetu zinaibiwa kwenye ufisadi...na wala haziwekezwi ..zinaishia kutumika kwa hanaasa....

........nadhani tone fahari kuwa na watumishi ambao wanaweza kuwekeza vipato vyao kwenye njia halali......na tunapoona wanafanikiwa tusikimbilie kuwaita mafisadi...hadi tumechunguza na kubaini........

Mkuu PM

Kweli mstaafu makini aliyechuma hela kwa jasho lake na makini kwenye kazi ake ataacha kuwekeza kwa faida yake ya baadae kwa sababu anaogopa kashfa?? Kama ni hivyo wacha wafe kwa umaskini wao....
 
Wana JF

Hili tatizo la wastaafu labda lingeangaliwa kwa upande mwingine kidogo...hebu tuangalai jinsi maisha ya mtanzania wa mwenye kipato cha kawaida yako vipi. Mimi naona kizazi kipya 45 Years kushuka chini wameweka viwango vya maisha vya hali ya juu na ndio maana tunaona wengi ya hawa wastaafu wana shida. Tutakuwa tufanya makosa iwapo tulitegemea wastaafu wetu wawe wanaendesha magari mazuri, wanatibiwa hospitali nzuri na kuvaa viwalo va gharama. Sio kwamba hawastahili hayo na mengine yote mazuri bali ni kwa sababu wao ndio waliweka misingi ya mibovu iliyotufikisha hapa tulipo.

Wahenga walisema utavuna ulichopanda na hawa wazee ndio sasa wanavuna. Kana kwamba shida wanazopata hazitoshi, utaona wastaafu wengi wala hawana la kusema kuhusu hali ya sasa ya maisha. Wengi wao wala hawaungi mkono mabadiliko ya kweli kwa maendeleo ya nchi yetu; wao bado wanaona "mfumo wa sasa" chini ya CCM ndio jibu la matatizo yote waliyonayo...ni hawa hawa wastaafu walisoma elimu ya mkoloni na ile ya kijadi iliwafundisha umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu lakini wao wala hatuoni wakitumia uzoefu wao kushauri ipasavyo katika sekta mbali mbali...angalau Warioba anajaribu.
 
Phillemon umenena sawia. haiwezekani mtu ashike nafasi kubwa katika uongozi, halafu ushindwe kujitngenezsea maisha yako ya baadaye kwa kutumia kipato chako halali. nsololi anaweka maneno mazuri kuthibitisha maneno ya Phillemon kuwa baadhi ya wazee wetu waliendekeza sana starehe hata kufikia hatua ya kuneglect familia zao, matokeo yake ndiyo kama hayo
 
..hawa wazee msiwaonee huruma hata kidogo..washamba kabisa..!!!..wanatutia aibu....,mtu huwezi kuwa kwenye rank ya presidential appointment..yet unashindwa kutumia mapato yako vema ..then uje kulaalama...wajinga hawa...sio lazima uwe fisadi ili uwe na maisha bora..ukweli ni kuwa posho,mishahara,safari na allowances nyingi wanazopata hawa wakuu hawatakiwi kuwa masikini hata kama mfumo wa mafao ya uzeeni ni mbovu.....waliendekeza starehe na kujengea mabibi majumba hawa!!!!!!!!

..just lets be serious..huwezi kuniambia mtu kama chedial mgonja...a long time foreign minister...mtu kama..jaji mwesiumo...mtu kama marehemu..profesa machunda [one time agriculture minister ...na wengine wengi leo hii wanakuwa malofa au wanakufa malofa...wakinga hawa na wafujaji.....na ndio wamesababisha wanasiasa wa sasa wakiwaona wanaamua kuiba...wakifikiri watatajirika...wanasiasa wa bongo hata wakiwa na 100 billion...leo mpe miaka mitano anafilisika....

juzi nimekutana na waziri mstaafu wa muda mrefu ..arcado ...naona naye kachoka hadi unamuonea huruma....serikali lazima i adree hili tatizo....nashauri wanasiasa wa tanzania wakifunze kuwekeza mafao yao kwenye HISA,mashamba makubwa[commercial farming .....etc...

juzi nilikuwa naangalia tv ..nikiwa kenya....nikaona wanaoonyesha maisha ya waziri mmoja mstaafu....wakawa wanamuuliza retirement benefit na savings zake amefanyia nini...aliwapeleka kwenye apartments anazojenga ....na pia akawaonesha shamba la chai na ngombe.....

kingine watanzania tunaabudu sana umaskini.....utakuta mtumishi wa umma hata kama atakuwa na shughuli halali au ana pesa za fortune...akifanya mradi mkubwa tayari maneno yanaaza..hii mwisho husababisha wanasiasa na watumishi wa umma kuamua kufanyia starehe pesa zao..wakiogopa kufanya mradi wa kuonekana ili wasipate kashfa...nashauri tuache wivu!!!!...hii inasababisha pesa zetu zinaibiwa kwenye ufisadi...na wala haziwekezwi ..zinaishia kutumika kwa hanaasa....

........nadhani tone fahari kuwa na watumishi ambao wanaweza kuwekeza vipato vyao kwenye njia halali......na tunapoona wanafanikiwa tusikimbilie kuwaita mafisadi...hadi tumechunguza na kubaini........

Full kujichanganya!!!
 
Liundi akosoa utaratibu wa utoaji ruzuku

2008-12-26 14:21:27
Na Simon Mhina

Msajili wa kwanza wa vyama vya siasa nchini, George Liundi amekosoa utaratibu wa ugawaji rukuzu kwa vyama vya siasa vyenye wabunge pekee na kusema utaratibu huo sasa haufai kwa vile unalenga kukitajirisha Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Liundi ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alienda mbali zaidi na kusema utaratibu huo, unaonekana zaidi kukineemesha CCM na kuvidumaza vyama vya upinzani, hasa vile vipya vinavyoanzishwa.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam Liundi alisema ni kweli yeye ndiye aliasisi utaratibu huo, lakini ulikuwa wa mpito katika kipindi cha kujifunza kwa vile utaratibu wa vyama vingi ulikuwa mgeni nchini.

Alisema fedha zinazochotwa na CCM zinatosha kabisa kukitajirisha, achilia mbali kuendesha shughuli zake huku vyama vingine `vikifa njaa`.

Akifafanua, Liundi alitoa kauli ambayo wakati fulani iliwahi kutolewa na Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema, kwamba hata kama chama kingekuwa na viongozi wajanja na maarufu kwa kiasi gani, hakiwezi kufanya shughuli zake bila kupata fedha.

Alisema kwa msingi huo, vyama vinahitaji ruzuku kwa vile michango ya shilingi mia mia toka kwa wanachama haiwezi kuendesha chama.

Alisema inabidi vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vipewe kiasi fulani cha fedha, bila kujali kina wabunge au la.

Pia alisema ruzuku inayozidi itolewa kwa mujibu wa idadi ya wanachama na ofisi za Chama husika nchi nzima.

Alisema kigezo kingine cha kutoa ruzuku ni jinsi chama kinavyowajibika kisiasa na kura wanazopata katika chaguzi mbalimbali.

Pia alisema ruzuku inatakiwa pia kutolewe kwa vyama kwa kuangalia namna vilivyofanikiwa kupata wabunge na madiwani.

``Kigezo cha ubunge na udiwani, kiwe kigezo cha mwisho cha kukipatia chama ruzuku,`` alisema na kuongeza: ``Vyama vipya vitapataje madiwani na wabunge bila kufanya shughuli za kisiasa kwanza na shughuli za kisiasa ndio hizi ambazo zinategemea fedha? Lazima utaratibu huu tuubadili,`` alisema.

Alipoulizwa kwa nini katika enzi zake hakuubadilisha, alisema ili kuboresha vyama, alishabadilisha mfumo wa utoaji ruzuku mara mbili.

Alisema mwanzoni mwaka 1995 kila mgombea alipewa ruzuku yake ya Sh 500,000 kabla ya uchaguzi, na kiasi hicho baadaye.

Akasema utaratibu huo ukaonekana kuwa na kasoro, hivyo ukabadilika kuwa wa kutoa ruzuku kwa chama chenye wabunge.

``Wakati wangu ulikuwa wa kujifunza, mfumo huu wa vyama vingi ulikuwa mgeni mno, hivyo inabidi kubadilika kila wakati ili kuuboresha ,`` alisema.

SOURCE: Nipashe
 
Philemon Mikael said:
..just lets be serious..huwezi kuniambia mtu kama chedial mgonja...a long time foreign minister...mtu kama..jaji mwesiumo...mtu kama marehemu..profesa machunda [one time agriculture minister ...na wengine wengi leo hii wanakuwa malofa au wanakufa malofa...wakinga hawa na wafujaji.....na ndio wamesababisha wanasiasa wa sasa wakiwaona wanaamua kuiba...wakifikiri watatajirika...wanasiasa wa bongo hata wakiwa na 100 billion...leo mpe miaka mitano anafilisika....

Philemon Mikael,

..Chediel Mgonja alifilisika kutokana na kesi yake ya uchaguzi iliyochukua muda mrefu sana. kesi hiyo ilikwenda mpaka mahakama ya rufaa.

..wakati wa utawala wa Mwalimu umasikini au ufukara ilikuwa kama ndiyo kigezo cha kiongozi bora na mjamaa wa kweli. nakumbuka wakati Mwalimu anamu-eulogize Sokoine alimsifia sana kwamba alifariki akiwa masikini!!

..wa-Tanzania pia wamejijengea imani kwamba hakuna njia yoyote ile mtumishi wa umma anaweza kuwa na maisha mazuri au utajiri wa namna yoyote ile.
 
UJASIRIAMALI nayo ni issue jamani,wengi hawajui namna ya kufanya fedha walioyopokea kama mafao iwatumikie mpaka kufa kwao wanabaki kuitumikia mpaka wanakufa kabisa
 
fafanua tafadhari kuna watu wanaguswa na statement yako.

Nayeguswa aseme!

Kandambili,Haiingii akilini mtu kama Taji kushindwa kuishi vizuri na mzee wake kama siyo mambo ya laana.Shetani aliingia nadani ya familia na hivyo wanaitaji upako.

Au kama vipi waende kwa kakobe
 
UJASIRIAMALI nayo ni issue jamani,wengi hawajui namna ya kufanya fedha walioyopokea kama mafao iwatumikie mpaka kufa kwao wanabaki kuitumikia mpaka wanakufa kabisa

Mkuu Ulusungu..
Kuna nchi nyingi tu ambazo wastaafu hawajiingizi kwenye ujasirimali na wanaishi maisha mazuri tu kwa kutumia malipo yao wanayopata baada ya kustaafu. Mimi nafikiri la muhimu ni kufanya kazi kwa bidii huku tukiepuka ufisadi ili na sie tuwe na system kama hizo. Sio kila mtu anaweza kuwa mjasirimali...
 
Mwache apande dala dala sisi tunaopanda na kukaa uswahilini mbona hamtuonei huruma
Gembe acha unafiki
 
Mimi nashangaa sana fikra za watu, kuna siku jamaa kaja ofisini kwangu mimi simjui, ila sura yake haikuwa ngeni machoni, baada ya kusalimiana akataka kuonesha kwamba ananijua vizuri kwa kuniuliza bado unakaa vingunguti???, (nikashangaa, kwani sijawahi kufikiria kuhama) nikamuuliza kwani aliskia ninajenga kwingine?? akasema no unajua nyie watu wakubwa sio wa kukaa huko!!!, tangia hapo sikuweza kumpa nafasi ya kuongea naye vizuri, nilimjibu mkatomkato hadi akatahayari na kuondoka. sasa nikajiuliza inamaana kipato kikiongezeka niondoke vingunguti?, niende wapi?, pia nimekua nikiongea na jamaa zangu mara nyingine nikiwa kwenye daladala nikimwambia mtu nipigie baadaye kidogo niko kwenye basi, hawakubali kwamba ninastahili kuwa kwenye basi. na kwa kweli sina kipato kikubwa cha kuniwezesha kuwa na mkoko wangu labda mwakani akipenda Allah nitakuwa nao, japo ikibidi kupanda daladala nitapanda. sasa vitu kama hivyo usipokuwa makini basi ujue utaharibikiwa kwani utaishi maisha kwa kuendeshwa na watu wengine badala ya kuishi jinsi maisha yako yalivyo, matokeo yake uibe na utumie kuzidi kipato ufilisike.
 
Back
Top Bottom