Eti sikukuuu ya wanawake! Ina manufaa gani kwa wanawake walio vijijini?

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,846
ACHANENI NA HIZI SIKUKUU. NI MIRADI YA WATU

Mimi mamaangu sikuwahi kumuona akisherehekea siku hii. Wala Sijaona jinsi sikukuu hii ilivyomsaidia mwanamke au msichana kijijini. Kila mwaka ni wajanja wa mjini tu.

Anyway, hii sikukuu haiko peke yake. Mara sikukuu ya vitaulo, viziwi, albino, n.k. Upuuzi mtupu. Sikukuu ikipita wasio na vitaulo wanaongezeka! Viziwi wanaendelea kutosikia! Albino wanaendelea na ualbino wao! Kuna sikukuu ya watoto lakini waandaji na wanufaikaji ni watu wazima!

Asili ya hizi sikukuu ni sikukuu ya wafanyakazi aka Mei Dei. Mei Dei ilikuwa na maana zamani. Sherehe hii iliendana na wafanyakazi kupewa nyongeza ya mshahara nchi mbalimbali duniani.

Lakini nayo siku hizi imepoteza haya manufaa. Nyongeza haitolewi tena siku ya Mei Mosi. Wafanyakazi wanaambulia t-shirt na hotuba wanarudi majumbani na ahadi ya "fungeni mkanda mambo mazuri yanakuja"

Msilolijua: kuna kikundi Cha wajanja kilichopo New York. Kikundi hiki ndio kina husika na hizi siku uchwara! Linapiga debe wee hadi sikukuu itambuliwe na UN na jamii ya kimataifa .

Chenyewe kinafaidi hela! Kila muda ukipita kinabuni sikukuu. Kinapewa hela kuadhimisha hizi sikukuu. Ujanja huo umeteremka hadi kwenye nchi zetu. Vipo vikundi vya wajanja vinapata fedha za serikali na wafadhili kuandaa hizi sikukuu.

Tanzania kuna mfano hai. Yupo mama tulikuwa naye OTTU alikuwa mkuu wa idara ya wanawake pale OTTU. Raisi Mkapa akaomba OTTU impe majina ya wanawake wawili ili wapewe vyeo serikalini. Mmoja alipewa Waziri Wizara ya Elimu. Mwenzie aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Singida (Mama HK).

Mama alipokuwa RC Singida aka lobby sherehe ya siku ya Wanawake Duniani zifanyike Singida kitaifa. Akafanikiwa. Baadae ikagundulika mbali na kupewa fedha na serikali pia aliomba fedha kutoka shirika moja la UN Dar Es Salaam . Akapewa. Lakini hizi fedha kutoka serikalini na UN akapiga panga. Yakazuka malumbano na wenzake kwenye kamati. Fisi akaibia Fisi Wenzie!

Mashitaka yakafika hadi ofisi hiyo ya shirika la UN mjini Dar Es Salaam na mpaka Wizara husika.

Haukupita muda RC akahamishiwa Iringa. Huko nako ikatoka lawama za kula hela za mbio za mwenge!

RC alkateenguliwa bila kupangiwa kazi nyingine!

Najua wanaojifanya gender activists nitawakera! Lakini bora niwakere!

Hizi sikukuu ni miradi tu ya watu. Hakika mama wa kijijini hapati chochote. Ni hawa wa mjini wenye NGOs na watumishi serikalini ndio wanufaika. Wanaendesha warsha uchwara na kuongea kwenye tv tu!

Poleni sana wamama wa vijijini.
 
Back
Top Bottom