George Liundi ... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

George Liundi ...

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Gembe, Dec 24, 2008.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Wakulu Heshima Mbele,

  Ni kawaida yangu kipindi cha sikukuu kuwasiliana na watu walioko nyumbani kujua khali ya maisha ikoje na kuwatumia japo pesa kidogo kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu.

  Kabala hata sijaanza kuuliza maisha yakoje,Mjomba akaniambia alikuwa akisoma gazeti moja la kiswahili la leo na wameandika makala moja ya kuelezea maisha ya Mwanasheria wa zamani wa wizara ambayo mjomba alikuwa akifanya kazi, ambaye baadaye alikuwa Msajili wa Vyama vya siasa ndugu George liundi.

  Mjomba likuwa na huzuni hasa anakumbuka jinsi Liundi alivyokuwa muadilifu.Makala hiyo imeelezea jinsi anavyoishi maisha duni ya kupanda daladala na kuishi uswahili tofauti na jinsi alivyotumika kwa uadilifu katika sehemu mbali mbali za wizara na taasisi za serikali.

  Maneno ya mjomba yameniangia sana kichwani mwangu,Mtu kama George ambaye alishawahi kuwa katibu wa wizara hana mali ambazo zinafikia bilioni 2(alizonazo katibu mstaafu Mgonja).Haishi mikocheni katika jumba la kifahari kama analomiliki Mgonja.Mgonja kaniambai anaishi mabibo tena mbali kusiko kuwa na Barabara .

  Hivi yule mzee mmoja ambaye alikuwa aktibu mkuu wa baraza la mawaziri na alitelekezwa yuko wapi?

  Nimesikitika sana na kama kuna mtu ana namba ya Mzee Huyu naomba anipe nahitaji kuzungumza naye ili aende kwa mjomba wakaongee.KLH News naomba mfanye jithada za kuzungumza naye kwa kuwa ana siri nzito ambazo hata mjomba mwenyewe kashtuka.Anawajua mamluki wote waliopandikizwa katika vyama vyetu

  Nimemwambia Mjomba atafute sehemu ascan gazeti na anitumie habari hiyo niiweke hapa.Aliniambia ni gazeti la Nipashe ila sijaona makala hiyo kwenye tovuti ya IPP
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Gembe,
  inatia huruma. Lakini hao wako wengi kuliko wanaoishi maisha ya raha, wengi waliolitumikia Taifa kwa upendo, moyo wa unyenyekevu ndio maisha yao yalivyo, wanaishi kwa kutegemea mafao ya uzeeni ambayo hayatoshi. Nayakumbuka maisha ya Prof. Machunda, ambaye aliwahi kuwa Waziri, kweli alikuwa anatia huruma sana. Katibu umzungumziaye ni Apiyo?
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  George Liundi ni mstaafu kama walivyo wengine waliotumikia umma kwa muda mrefu. Tulitegemea kwa nafasi zao wangetengeneza mfumo mzuri wa social security lakini hawakufanya hivyo na sasa wamekuwa wahanga wa uzembe wao wenyewe walipokuwa kazini.

  Tena bado hawajifunza kwani tunaona wale walio madarakani sasa hivi badala ya kurekebisha mfumo, wanatafuta njia za mkato kama tulivyoona kwa wale wachache walofikishwa mahakamani kisutu hivi karibuni.

  Wastaafu wengi waliokuwa waaminifu kazini sasa hivi wako taabani na hawana uhakika wa maisha. Tuliwahi kuambiwa mifano ya akina Timoth Apio aliyekuwa katibu mkuu ofisi ya Rais, n.k.
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mfumo,

  Tuko ukurasa mmoja ,Nilikuwa namzungumzia apiyo..Mzee huyu bado yuko hai?anafanya nini?

  Hivi walifanya dhambi gani mpaka wakatelekezwa?Kwanini hawaitwi katika vikao hata vya chama...?

  Mie huwa najiuliza hivi kwanini watu kama Kingunge bado wanadunda tu,Je wao sio wahanga wa hili au hakuwa Muadilifu?

  HAwa watu ni muhimu sana kwa mabadiliko ya nchii hii.Naomba tufanye jitihada za kuwakutanisha na watuambie kwanini wao wanaishi maisha tofauti na ya kina vicent Mrisho,Rutabanzibwa na wengine wengi.
   
 5. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2008
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ..........smh.....Huyu Liundi si anaye watoto, mara ya mwisho nimecheki Taji alikuwa meneja wa kituo cha redio...wampige jeki kama vipi......au kivyake.
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mfumo???, Mkuu Gembe, kuna wakati niliwahi soma sehemu huyu Apiyo anaishi maisha si mazuri, japo ndio watu walikuwa waaminifu katika Serikali ya Mwalimu. Kwa sasa sijui yuko wapi?. Lakini unapozungumzia kuitwa katika vikao vya chama, mi sio CCM ama mwanachama wa chama chochote nitazungumzia kwa uono wangu. Hawa jamaa walikuwa wasafi, na wameishi yale maisha ya kijamaa kwelikweli aliyotaka Mwalimu tuishi, sasa ukiwata katika vikao sijui kama watakubaliana na MADUDU yafanyikayo sasa. Lazima watapinga, wazee hawa wa zamani walikuwa na misimamo.

  Kingunge ni mtu wa Nyakati, wakati wa Mwalimu aliishi kama mjamaa, sasa anaishi kama waliokuwepo. Anaendana na upepo, hivyo naye ni miongoni mwao ndio maana wana muenzi vibaya mno.
   
 7. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kinguinge amekuwa Kimya bsana kwa miezi miwili ,toka watu wanaze kuzungumzi ishu za kagoda..

  Hivi taji ni mtoto wa Mzee Liundi?Basi ni laana
   
 8. E

  Edo JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Naungana na Kakalende kuwa hawa wazee walikuwa wagumu kubadili mfumo wa hifadhi ya jamii. Nakumbuka mtumishi mmoja wa umma mwandamizi alisema walimpelekea proposal ya kureform pension scheme ya serikali Bw Apiyo-huyo anayetetewa hapa, akaitupilia mbali akisema -' nyie vijana mnajua nini toa hii kitu hapa'. Hiyo ndo hali halisi, apiyo yupo anaishi Ukonga-nadhani serikali iliwahi kumsaidia kwa kumpa discovery ya kutemebelea-lakini baadaye mafuta ikawa ngoma!
   
 9. C

  Chechenya Member

  #9
  Dec 24, 2008
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu nimesoma kwenye gazeti moja kuwa msajili wa vyama vya siasa sasa anaishi uswazi. Alizoea kukodi ndege sasa anapanda daladala bila wasi wasi wowote kwa vile yeye sifisadi.
   
 10. O

  Onychomycosis Member

  #10
  Dec 24, 2008
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unamuongelea nani? Liundi?
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Vizuri tu... kwa mapana na marefu kuhusu George Liundi tembele kona hii
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwani kuishi uswahilini kuna tatizo gani?
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda mwanzisha mada alikwua anatoa compliments
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,553
  Likes Received: 18,239
  Trophy Points: 280
  George Liundi ni mtu very coservative. Huyu ni mtu bold typical Nyerere type. Jamaa enzi zake akiwa msajili, ni mtu wa kwanza kusema Mtikila ni Kichaa. Jamaa mmoja anaitwa Joshua Mwatuka alipanga interview na Msajili Liundi. Akaweka shurti isiulizwe lolote kuhusu DP. Mheshimiwa akaja Kilimanjaro Hotel enzi hinzo. Kabla interview haijaanza, Mchungaji Mtikila naye akaja Kilimanjaro hoteli kwa yake. mhe Liundi kumuona tuu, aliamka kwa hasira kuelekea kwenye gari yake and never- again alikubali kuendelea na ile interview. Hii ni misimamo mikali ya kutosikiliza excuse yoyote.

  By the way jamaa si ni mwanasheria?. Yasije yakawa yale yale ya waziri mstaafu kufuga kuku baada ya uwaziri. K
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna mengi yanasababisha wao kuwa kwenye hali kama hii. Mtu kama MZEE Apiyo anhitaji kulaaniwa kwa sababu yeye alikuwa engineer wa utaratibu wa mafao ya uzeeni ambao unawaumiza wengi. Kwa yeye kwa kuwa alikuwa kwenye utukufu, alijisahau kuwa huo utukufu siku moja utakwisha akawa anatumia mapesa kwa mambo ya kujiburudisha, sasa hivi anaona uchungu, bila kujua kuwa uchungu ameuleta yeye.
  Mzee Liundi naweza kusema ni mmoja kati ya wazee ninaowaonea huruma, kwa sababu naye inawezekana alikuwa muadilifu kwa maana hakuwa mwizi, lakini ukiangalia mambo aliyofanya hasa alipokuwa msajili wa vyama utaona kabisa ni mzee aliyekuwa hafai(sitaki kusema zaidi) kama maisha yana mgonga inawezekana ni adhabu.
  Kuna mzungu mmoja mtanzania anaitwa Rugumyamheto, na yeye naona anaelekea huko huko kwa akina Apiyo, nilishangaa sana kukaa nae kwenye baa moja ucharwa pale sinza, ilikuwa jabu kwa yeye kuja kwa sisi walala hoi.
  Lakini kuna wengi waliostahili kuthaminiwa lakini kwa sasa bahati mbaya wanateseka sio hao tu. Ndio maana baadhi ya watu wanailalamikia CCM.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Bongolander heshima mbele mkuu, nimesoma contribution yako na humo umemuandika bwana mmoja anaitwa Rugunyamheto kuwa nae anawezakuwa anaelekea walipofika wakina Apiyo!!! MKUU HIYO SI KWELI KWASABABU HUYU BWANA RUGUNYAMHETO NI FISADI ALIYEKUBUHU; ninastaajabu sana kuona kuwa yeye hajapandishwa Kisutu mpaka sasa. huyu bwana ndiye aliyejenga hoja kwa Mkapa mpaka nyumba za serikali wakauziwa kwa bei ya che,na yeye alikarabati nyumba yake kwakutumia mamilioni [pamoja na Lumbanga ] ya fedha za wadanganyika kabla ya kuuziwa. Sio hivyo tu huyu bwana amekula 10% yake ya commission kwenye ujenzi wa jumba la ofisi za UTUMISHI hapo karibu na feri!! Kwahiyo huyo mzungu wako anazo!!
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nazikumbuka ahadi za mwana TANU

  ...binadamu wote ni sawa...

  Sisi tunakaa huku uswazi siku zote na wao ni binadamu kama sisi, kwanini leo hii tunaona hawastahili kukaa huku? Au ndiyo sisi wenyewe tuna-bold uwepo wa matabaka, at the sametime tunalalamika wakijilimbikizia mali...mimi nadhani anastahili kuishi hivyo kwani haya ndiyo maisha ya wastaafu wengi wa serikali kama vile walimu, wauguzi, nk. kama ni huruma basi waonewe huruma maelfu ya wastaafu wanaoishi maisha kama yake.
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwa kuongezea wakuu,
  kuishi uswahilini siyo ishu kabisa.Kila mtu ana uchaguzi kuamua aishi wapi.Kama huo ndio uchaguzi wake sisi tuna haki gani kumshangaa au kuamuamulia ni wapi pangemfaa zaidi?
  Huyu ni mtu mzima, aliyepata fursa zote za kujiandaa kwa kustaafu hasa ukizingatia aliwahi kupewa kazi za mikataba hata baada ya kustaafu.Isitoshe amekuwemo kwenye ajira ndani ya serikali za awamu tatu ikimaanisha aliweza kuona wenzake waliostaafu bila kujiandaa walipatwa na adha gani.Ksma hakujiandaa na hivyo kujikuta maisha yakimuwia magumu hayo ni matokeo.
  Pia ana watoto kwa "ndoa zote mbili".. na "mkewe wa sasa" bado kijana na ana ajira.. hana sababu kwanini awe kwenye hali mbaya.Kama hawa nao hawamsaidii basi kuna jambo!
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Dec 25, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  wandugu,

  ..mke wa kwanza wa Mzee Liundi aliwanywesha sumu wanawe watatu. wawili walifariki, na mmoja ambaye anaitwa Taji Liundi alinusurika. inasemekana mke wa kwanza wa Mzee Liundi alichanganyikiwa kutokana na tabia ya ukware ya mumewe, na hivyo kupelekea kujaribu kujiua yeye na watoto wake.

  ..Mama Liundi alipelekwa mahakamani na sikumbuki kama alihukumiwa kifo au kifungo cha maisha.

  ..Mzee Liundi aliwahi kuwa-seconded nje ya nchi nadhani ilikuwa Zimbabwe ambako alifanya kazi kwa muda mrefu tu. Baadaye aliporejea nchini ndiyo akateuliwa msajili wa vyama vya siasa.

  ..sasa ukiangalia huyu Mzee wetu kwa kweli nafasi alipewa, ila labda hakupiga mahesabu yake vizuri na ndiyo maana leo hii maisha yake siyo mazuri sana.

  ..binafsi sikubaliani na mapendekezo ya baadhi yetu kwamba serikali sasa hivi umuonee huruma na kuamua kubeba jukumu la kumuinua kimaisha. nimechukua msimamo huo kwasababu watumishi wastaafu wenye hali mbaya kama ya Mzee Liundi wako wengi sana.

  ..kumuibua Mzee Liundi toka kundi kubwa la watumishi wenye hali kama yake kwa kweli itakuwa ni upendeleo wa namna fulani. itakuwa jambo jema kama kutakuwepo utaratibu wa kisheria wa kuboresha pensheni za watumishi wastaafu, na siyo kusaidia mmoja mmoja.

  ..majuzi alisaidia Mzee Apiyo. halafu tena Abel Mwanga, mwalimu wa kiingereza wa Sokoine, naye tukaambiwa ana hali ngumu. leo tena anaibuka Mzee Liundi. utafutwe utaratibu rasmi wa kuwasaidia watumishi wastaafu wote.
   
 20. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wajanja walipoona hilo wakaamua kujiuzia nyumba zoooote za awamu zote, Mungu akupe nini?
   
Loading...