George Bush, Rais wa 41 wa Marekani afariki Dunia

George Bush, Rais wa 41 wa Marekani afariki Dunia

Yeye ndo alianzisha vita mwaka 1993?

Mbona mwaka 1993 rais wa Marekani alikuwa ni Bill Clinton....

Operation Desert Storm ilianza Januari 1991 na kumalizika Februari 1991.

Novemba 1992 uchaguzi mkuu ukafanyika na Bill Clinton akamshinda George Bush Sr.

Bill Clinton akaapishwa kuwa rais wa Marekani Januari 20 1993.

FACTS.
Typing errors smartphonechallenges.
 
Former president, CIA leader, vice president. Kuna Watu wamefaidi madaraka.

Mtoto wake naye akawa Rais, mwingine Gavana
Kweli mkuu ila Mungu alimaliza yote yani haijalishi we nani una nini ila mwisho unakufa yani hapo hapo nikifikiria ndipo nasema kweli kifo hakina huruma.
 
Mke wa aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush aaga dunia
  • 18 Aprili 2018
_100920959_c3ec6dab-706b-4769-898b-14fddd040be8.jpg
Image captionBarbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92.
Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92.
Ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo akiwemo mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush.


George HW Bush : Rais wa zamani wa Marekani afariki dunia akiwa na miaka 94, je alikuwa mtu wa aina gani?
  • Dakika 58 zilizopita
_104575283_mediaitem104575282.jpg
Haki miliki ya pichaREUTERS
Rais wa zamani wa Marekani George H W Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94, mwanawe rais wa zamani pia George W Bush ametangaza.
George Bush Senior, kama alivyofahamika sana, alifariki dunia mwendo wa saa nne na dakika kumi usiku (saa kumi na dakika kumi GMT), msemaji wa familia hiyo ametangaza.
Alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1993 baada ya kuongoza kwa mihula miwili kama makamu wa rais chini ya Rais Ronald Reagan.
Aprili, alilazwa hospitalini akiwa na maambukizi kwenye damu lakiniakatibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
George Herbert Walker Bush amefariki miezi saba tu baada ya kifuo cha mke wake Barbara.
Viongozi wamekuwa wakituma salamu za rambirambi na kumkumbuka mwanasiasa huyo, wakiongozwa na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump aliyemsifu kwa "uhalisiwa wake, ucheshi na kujitolea kwake kudumisha imani, kwa familia na kwa taifa.
Bendera katika ikulu ya White House zitapepea nusu mlingoti huku mipango ya mazishi ikiendelea.
_101300278_454326384.jpg
Haki miliki ya pichaAFPGeorge H W Bush alikuwa mtu wa aina gani?
Kuapishwa kwa George H W Bush kuwa Rais wa Marekani mnamo Januari 1989 kilikuwa kilele cha ufanisi wake katika siasa. Alikuwa ameandiliwa kwa muda mrefu kupitia mafunzo ya kiwango cha juu, na kupandishwa madaraka mara kwa mara kabla ya kuishia Ikulu ya White House.
Rais huyu wa 41 wa Marekani alifanya kazi kama makamu wa Rais wa Ronald Reagan kwa miaka minane.
Alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza aliyekuwa afisini kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais katika kipindi cha zaidi ya miaka 150.
Utawala wake unahusishwa sana na siasa za wakati ule ambapo Ukomunisti ulikuwa ukiporomoka Ulaya Mashariki na kusambaratika kwa Muungano wa Usovieti (USSR) ambapo Marekani iliachwa ikiwa taifa kubwa zaidi kiuchumi na kiviwanda duniani.
Uongozi wake ulisaidia kurejesha hadhi ya Marekani kwa dunia nzima na kurejesha heshima yake kufuatia uvamizi wa Marekani nchini Vietnam, ulioiletea Marekani aibu.
Hata hivyo alilaumiwa kwa kupuuza maswala ya ndani ya Marekani na kwa kupuuzilia mbali ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni ambapo aliahidi kuwa hataongeza kodi.
Kupuuzilia mbali kwa ahadi hiyo kulimfanya ashindwe katika uchaguzi uliofuata na Bill Clinton wa chama cha Democratic mwaka 1992.
 
Waarabu wapi watashangilia? Kuwait ilipovamiwa na Iraq unajua kwamba Syria, Saud Arabia walikuwa upande gani? .Vitu vingine muwe manafikir kabla ya kuongea. Shujaa ameondoka, RIp na dunia itamuenzi
Hao hawajiu historia wanachota story za kwenye ghahawa na kuleta hapa,wanaongozwa na chuki. Na hata hawajui kuwa USC ndio iliyoamuru hiyo Vita na Saudi Arabia na Syria nao walishiriki kumuondoa Saddam Kuwait na ndio maana Israel iliambiwa na Marekani asijibu shambulio lolote la scud kuutoka kwa Saddam ili isilete shida kwa Nchi za kiarabu na Kiislamu zinazoshiriki hiyo Vita.
 
Wa Iraq siyo huyo aliyefariki nibaba yake ndiye Wa vita vya squad mtoto yupo ndiye alipiga Iraq

Dingi aliipiga Iraq pia, kama unakumbuka Vita ya Uajemi.

Mwanae alikuja kummaliza Saddam.
 
Naona pangu pakavu mnapeana za uso humu, hahaaa wale Wenzangu na mimi achilia mbali u monitor wa la saba D, hata unyampara au mfunga/mfungua milango hujawah pata. Yaan ukigombea uchaguzi wowote hata upo peke yako hushindi, mpiga kura anawekewa wewe na kivuli chako, anachagua kivuli chako, Asalaaale kweli dunia haina huruma
 
Back
Top Bottom