Genge la wahuni ni lipi kati yetu na wao?

Genge la wahuni ni lipi kati yetu na wao?

Joined
Apr 29, 2025
Posts
51
Reaction score
135
Wanaiba mali za umma, wanauza hovyo rasilimali za taifa. Hawataki tuwaambie ukweli kwamba hii nchi ndiyo kwetu. Mukiitapanya leo tutaishi wapi kesho? Watoto wetu, wajukuu na vitukuu na vizazi vijavyo, wataishije kesho kama hamzingatii leo yetu?

Tukiwaambia hawatusikilizi. Wanatuteka, wanatutesa, wanatuua kikatili. Wanatubambikia kesi tunasota magerezani.

Tukipaza sauti, wanashika mitutu wanatuua kwa maelfu. Kisha wanatuzika kusikojulikana. Yote ni ili wasalie madarakani walinde maovu yao.

Wakitoka hadharani, sisi tunaoibua maovu yao na kuwaambia waache kwaajili ya kesho yetu sote, sisi tunaopaza sauti na kuuawa kwa ajili ya kesho bora yetu sote, wanatuita magenge ya wahuni.

Hivi kiuhalisia, genge la wahuni ni lipi? sisi au wao?!
 
Back
Top Bottom