N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,988
- 12,019
Muda unaonekana mrefu ukiwa na miaka 18, 20 au 25. Lakini ukweli ni kwamba miaka inapita kwa kasi ajabu. Jana ulikuwa mwanafunzi, ghafla una miaka 30 unajiuliza muda ulienda wapi.
Ndiyo maana:
• Jifunze mapema
• Fanya kazi kwa bidii
• Jenga nidhamu
• Heshimu muda
•Acha masihara na maisha
•washkaji hawatakuwepo unapotaabika uzeeni!
Kwa sababu siku moja utaamka na kugundua ujana umebaki kwenye kumbukumbu tu.
Tumia ujana wako vizuri, maana uzee hausubiri mtu...na uzee usio na rasilimali za kutosha huisha kwa mateso makali zaidi.