JokaKuu
Mkuu kuna uvumi uliokuwepo katika kipindi cha maasi ya 1964 kuwa kulikuwa na ushindani wa vyeo kati ya Elisha Kavana na Sarakikya kiasi kwamba Mnyamwezi Kavana akachongewa kuwa alikuwa ndie engineer wa maasi. Kavana tokea pale hakusisikika tena na sijui yuko wapi msomi machachari huyu aliye pata first class ya units 9 - akifanya masomo 9 na kila somo unit 1 ambayo ilikuwa ndo VERY GOOD.
Pili: historia inataka potoshwa hapa kwamba Jeshi la Wananchi (JWTZ) liliundwa na waingereza waliokuja kuwa disarm wale wa KAR walioasi. Si kweli hapa lazima tujivune waafrika kuwa jeshi letu lilifundishwa na wa NIGERIA baada ya Mwalimu kuziomba nchi za kiafrika zijitoe kuchukua nafasi ya kuilinda tanganyika badala ya majeshi ya Mwingereza wakati tulikuwa tunaonekana kuunga kwa vitendo ukombozi wa africa.
Tatu: si kweli kabisa kuwa askari waasi walisalimu amri kirahisi kwa jeshi la uingereza. pale carito walipambana na mkurya aliewachachafya sana na resistance kubwa waliipata Tabora kwani walishapata taarifa hivyo wakawa na muda wa kujiandaa kuukabili uvamizi. kwa vyovyote vile walishindwa ukichukulia uduni wa vifaa vya kivita. wale wa carito walifanyiwa mbinu ya kuleweshwa usiku uliotangulia kwa kile kilichoelezwa ni tafrija ya kusheherekea mafanikio ya maasi baada ya "MAKUBALIANO" na Serikali kuhusu madai yao.
Nne: nchi hii ilikuwa na idadi ya watu takriban 9 milioni - na dar ilikuwa ndogo kiasi cha habari watu kupasiana kirahisi. watu watakumbuka hata Mwalimu aliweza isoma orodha ya watu "waongo" na TBC ikawa inayasoma majina hayo kila baada ya taarifa ya habari. inawezekana sarakikya kuhusika na moja ya uasi ambapo inasemekana nyerere alimwita na kumpa bunduki ampige yeye kuliko kuiharibu nchi. swala hapa ni je uasi katika phase ipi - baada ya maasi ya 1964 kulikuwa na phases za uasi au majaribio ya kuiangusha serikali ya mzanaki sio chini ya tatu mojawapo ikiishia kuhukumiwa Mahakama kuu. kina Ilonsi wako wapi jamani.
NB:
..jina kamili la mhusika mkuu wa mada hii ni MIRISHO SAM HAGGAI SARAKIKYA.
..wakati wa maasi ya 1964 alikuwa na cheo cha Captain. wakati huo hakukuwa na Mtanganyika aliyekuwa na cheo kikubwa zaidi ya hicho.
..sasa kwasababu Tanganyika Riffles ilikuwa chini ya Afisa wa Kiingereza aliyekuwa na cheo cha Brigadier. Cheo cha Brigadier General nimeanza kukisikia miaka ya karibuni.
..baada ya Tanganyika Riffles kuvunjwa na kuanzishwa JWTZ/TPDF, Mirisho Sarakikya aliteuliwa kuwa Chief of Defence Forces, na kupandishwa ngazi kuwa Brigadier.
..Mkuu wa utawala wa Jeshi, au Chief of Staff, wa kwanza wa JWTZ alikuwa ni Major.Elisha Kavana ambaye alikuwa na cheo cha 1st Lieutenant.