Nguruvi3,
..tatizo letu liko kulekule kwamba hatuna utamaduni wa kuweka kumbukumbu zetu za kihistoria wazi.
..kwenye nchi za wenzetu ungekuta tayari kuna vitabu vya maisha na experiences za makamanda wote waliopigana vita kubwa kama ile ya Kagera, au ya Msumbiji.
..juu ya hayo pia kungekuwa na kumbukumbu ya matukio au mapigano muhimu kama yale ya Lukaya, au urejeshaji wa eneo la daraja la kagera, etc etc.
..wakati wa vita vya Kagera, Major General.Ben Msuya[then Lt.Col] alikuwa chini ya kamandi iliyokuwa ikiongozwa na General.David Musuguri[then Major.Gen]. sasa Lt.Col.Msuya ndiye inaripotiwa kuwa ndiye kamanda wa kwanza wa Kitanzani kuingia Kampala!!
..unapozingatia kwamba wakati huo serikali moja ilianguka, na ikabidi kusimikwe serikali nyingine, ndiyo utagundua uweledi na ufanisi wa askari wetu pamoja na makamanda waliokuwa wakiwaongoza.
..hata hii habari tunaweza kuizungumzia kwasababu wapo waandishi wa Kiingereza waliokuwa embedded na vikosi vya JWTZ vilivyokuwa mstari wa mbele kuiteka Kampala. Waandishi na wanahistoria wa Tanzania have never shown any interest kuli-document tukio lile. Kitu cha kusikitisha ni kwamba sasa hivi makamanda wengi walioongoza vita ya Kagera wametangulia mbele ya haki.
NB:
..jina kamili la mhusika mkuu wa mada hii ni MIRISHO SAMA HAGGAI SARAKIKYA.
..wakati wa maasi ya 1964 alikuwa na cheo cha Captain. wakati huo hakukuwa na Mtanganyika aliyekuwa na cheo kikubwa zaidi ya hicho.
..sasa kwasababu Tanganyika Riffles ilikuwa chini ya Afisa wa Kiingereza aliyekuwa na cheo cha Brigadier. Cheo cha Brigadier General nimeanza kukisikia miaka ya karibuni.
..baada ya Tanganyika Riffles kuvunjwa na kuanzishwa JWTZ/TPDF, Mirisho Sarakikya aliteuliwa kuwa Chief of Defence Forces, na kupandishwa ngazi kuwa Brigadier.
..Mkuu wa utawala wa Jeshi, au Chief of Staff, wa kwanza wa JWTZ alikuwa ni Major.Elisha Kavana ambaye alikuwa na cheo cha 1st Lieutenant.
Joka kuu, nashukuru sana umenikumbusha hili la Mirisho. Ni kweli kama ulivyosema.
Pili, upo sahihi sana kwamba hatuna utamaduni wa kuweka kumbu kumbu. Ingekuwa ni kwa wenzetu vita kama ya Kagera ingekuwa na vitabu kama 10 au zaidi. Yupo ambaye angeandika kuhusu Maandalizi ya vita tu, mwingine kutangazwa vita, Kukomboa daraja, Lukaya, mbarara, Kampala n.k.
Inasikitisha sana kuona mtu kama Gen Mayunga na Gen Walden wametangulia mbele ya haki na sidhani kama zipo kumbu kumbu za kina kuhusu wao.
Mtu kama Lt Gen Tumaini Kiwelu ni muhimu sana katika kumbu kumbu. Inasemwa kuwa ndiye aliyewahi kuhoji kwanini RENAMO na FRELIMO mtu na mjomba wake wapigane halafu askari wetu washiriki vita. Kauli yake ilibadili sana mtazamo wa Tanzania kuhusu msumbiji na ikatia msukumo zaidi wa mazungumzo badala ya silaha
Labda tutoe changamoto kwa wana historia na waandishi wa habari kwenda kuongea na watu kama kina Kiwelu, Bayeke, Ben Msuya, Musuguri, Kiyaro, Mahufudhi, na wengine ili kuweka kumbu kumbu sawa.
Ukiangalia kwa makini kuna ajira nzuri sana hapo.
Waandishi wa habari hivi hamuwezi kuandika documentary. Kama kuna watu wana documentary ya 80-100 years na inaleta hisia kwanini ishindikane kitu cha miaka 30 tu iliyopita.
Mleta mada chukua dondoo ziwe 'lead' katika kazi yako na fanyia kazi kupata details na facts, wazo lako zuri sana keep it up.