Gen. David Musuguri apewe fadhila yungali hai

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Gen. David Bugozi Musuguri (103) rtd CDF amezawadiwa nini kwenye sherehe za miaka 62 ya uhuru? Miaka 44 ya vita ya Kagera? Miaka 46 ya utumishi jeshini (1942-1988)?

Vita alivyopigana:-

1. WW II 1942
-Battle of Madagascar

2. Uganda - Tanzania 1978-1979
-Battle of Simba Hills
-Battle of Masaka
-Battle of Lukaya
-Operation Dada Idi

NB.
Pana haja ya serikali kumpa alama ya kumbukumbu (souvenir) kufuatia pia kuwa ndiye Kamandaa pekee wa TPDF aliyepigana Kagera ambaye yungali hai na mwenye umri mkubwa kuliko muasisi wa taifa hili. Kiongozi huyu ni alama na fahari ya Tz, KAR na TPDF.

Ramani inaonyesha jinsi TPDF ilivyosambaza vita Uganda nzima na mishale kuonyesha njia za wapiganaji wa jeshi la adui la Uganda walipotorokea.

Screenshot_20231217-160919.jpg

Ramani kwa hisani ya Goran tek-en.
 
Mwaka jana ma CDF wote wastaafu walipewa magari mapya Landcruiser haya ya kisasa.
Huwa wanapewa mara kwa mara kwa vipindi maalum zikiwemo offer zingine kama samani, ukarabati wa makazi, free ticket, matibabu, ulinzi, posho mifukoni nk nk. Kuanzia Major General wanapewa privileges hizo, zamani ilikuwa ni kuanzia Brig. Gen nadhani, ambao sasa hivi ni wengi na bajet ya taifa inaelemewa.
 
Hawa wanajeshi wa zamani walikuwa ni wajeshi wa uwanja wa vita, sio maofisa wa darasani kama walio wengi wa wanajeshi sasa...

Mfano Jenerali Musuguri kashapigana vita vingi akiwa askari wa mstari wa mbele...

Hawa ni battle harden veteran, kutokana na mahitaji ya sasa waananzia darasani. Ila officers ambao wameshiriki battle wanakuwa na experience zaid kuliko wa darasani
 
Hawa wanajeshi wa zamani walikuwa ni wajeshi wa uwanja wa vita, sio maofisa wa darasani kama walio wengi wa wanajeshi sasa...

Mfano Jenerali Musuguri kashapigana vita vingi akiwa askari wa mstari wa mbele...
We ulikuwa naye?
 
Gen. David Bugozi Musuguri (103) rtd CDF amezawadiwa nini kwenye sherehe za miaka 62 ya uhuru? Miaka 44 ya vita ya Kagera? Miaka 46 ya utumishi jeshini (1942-1988)?

Vita alivyopigana:-

1. WW II 1942
-Battle of Madagascar

2. Uganda - Tanzania 1978-1979
-Battle of Simba Hills
-Battle of Masaka
-Battle of Lukaya
-Operation Dada Idi

NB.
Pana haja ya serikali kumpa alama ya kumbukumbu (souvenir) kufuatia pia kuwa ndiye Kamandaa pekee wa TPDF aliyepigana Kagera ambaye yungali hai na mwenye umri mkubwa kuliko muasisi wa taifa hili. Kiongozi huyu ni alama na fahari ya Tz, KAR na TPDF.

Ramani inaonyesha jinsi TPDF ilivyosambaza vita Uganda nzima na mishale kuonyesha njia za wapiganaji wa jeshi la adui la Uganda walipotorokea.

View attachment 2845166

Ramani kwa hisani ya Goran tek-en.
L/cruiser LC 300 anayotembelea ni kitu kidogo? Au ulitaka apewe dreamliner
 
Hiyo L/cruiser LC 300 anayotembelea ni kitu kidogo? Au ulitaka apewe dreamliner
L/cruiser LC 300 itaishi vizazi vingapi vijavyo kama alama ya kutambua mchango wake na uzalendo wake kwa nchi na jeshi? Kwa watendaji wenye matokeo makubwa ya kazi official car siyo motisha/motivation.

Majenerali/Makamanda wenzake wote alioongoza nao vita wametangulia mbele ya haki je, L/Cruisers walizopewa enzi za uhai wao zinaweza kuwatambua leo?!
 
Back
Top Bottom